Nimekutana na 'first boyfriend' anataka turudiane

Nimekutana na 'first boyfriend' anataka turudiane

Hehehe hata wakikushauri hapa uamuzi wa mwisho unao wewe kwa mtazamo tu very soon huyo F atakufanya.
 
FEW POINTS NOTED OVER YOUR LONG TESTIMONIAL LETTER.
1- UNATOKA FAMILIA BORA
2- UMESOMA S.A NA CANADA
3- UMEOLEWA NA UNA WATOTO WAWILI
4- X-BF WAKO ANATAKA KUWA NAWE JAPO NAYE KAOA
5-X-BF WAKO ANAISHI ARUSHA
6- WEWE UNAISHI DAR
7- MUMEO ANAKUZINGUA NDOANI
8- NDOA YAKO HAINA AMANI
9- UPO KWENYE DIALLEMA UFANYE NINI
10- ULIUNGAMA KANISANI KUWA HUYO WA SASA ANAYEKUZINGUA NDIO MUMEO JAPO HUKUMPENDA.

NAENDELEA KUIFANYIA KAZI FINDINGS ZAKO KUONA POSSIBILITY YA WEWE KUWA "Married But Availlable" ILI NAMI NIJIWEKE KWAKO.....ndio KWANI F aweze ana nini na mie nishindwe nna nini?
 
Aiseee sasa kati ya huyu mumeo na yule F yupi Hodari kitandani?!
maana kwa umri wako hakuna cha kupoteza hapo wewe furahisha roho yako tu
Kwani ana umri gani mama wa wawili? Hivi inawezekana nimemiss point ya umri wake katika findings zangu kweli? Famillah ngombe hazeeki maini na hainaga ushemeji tunakulagaaaa.

Punda afe MZIGO ufike
 
So saaaaad,!Muda so mrefu huyo jamaa atakufanya,coz umeshahalalisha.Ila kumbuka,majuto yatakayotokana na uamuzi huo hautakaa uyasahau.
 
Hauwezi kuchomoka hapo. Huyo lazima akutafune halafu atakutema sio mda. Utabaki unaugulia tu huku yeye, kama kawaida ya wanaume akijisifia kwa kukutafuna. haaaàahaaaaaa!!!!!!
 
Nijuavyo mimi Dagaa huliwa tuu tena saana, haijalishi analiwa na X, Y or Z as long as wewe ID yako tu ni Dagaaa sisi watu wa math tunaconclude kwamba kwa taarifa hii basi X amekwishakutafuna.. na onyo kali tunalokupa usiendelee kuwa Dagaa maana wale wanaliwa huku wanamtazama mlaji.
 
uchepukaji katika familia huanza taratibu, mwisho wa siku utamwona bwana yako siyo mtu sababu kuna mtu anakutumia meseji na kukupigia simu ukiwa kazini. Epuka balaa linalokuja mbele. kata mawasiliano haraka maana huyo F anaweza kukuchezea mchezo ambao hutakaa uusahau maishani.
 
Harufu Ya Watoto Kulelewa Na Mama Wa Kambo Inanukia Hapa. Watoto Wa Mtaani,God Forbid Nayo Inanukia. Ustawi Wa Jamii Jiandaeni.
 
Miaka kumi na nne bado unatuambie mambo ya x. Acha ujinga bwana tulia ulee familia.
 
Habari wapendwa wangu.

Mimi nipo hapa sihitaji ushauri ila nataka niwasimulie kidogo lililonitokee, sababu sijamwambia mtu imenibidi niwadokezee. Mimi ni mama wa watoto 2 na nimeolewa na ndoa ya kanisani, nina kazi yangu nzuri mshahara ni mzuri, maisha yangu ni mazuri tuna nyumba 2 na mume wangu na kila mtu ana gari yake, ila hapa kisa kilichonikuta ni kama ifuatavyo.


Baada ya Zaidi ya miaka kumi na 4 nimekutana na my first boyfriend, mi nashukuru nyumbani tulikua mambo safi, huyu boyfriend wangu tulikua tunasoma wote s.africa, mi nilikuja nikaama nikaenda kusoma Canada nikamwacha hapo ila tukawa tunawasiliana kwa ukaribu sana, mwisho wa siku tukapotezana, ila kiukweli nilikua nampenda na nina iman nae alikua ananipenda.


Sasa bwana mwezi uliopita nilikua nina meeting na kampuni moja nikakutana na rafiki yake, du tulifurahi sana, tukapiga story mbili tatu, akaniambia unajua F (jina la boyfriend wangu niliyepotezana nae) alikua anakutafuta sana, tukabadilishana namba, mi sikutaka kumwomba ata namba ya F sababu najua sasa nina familia yangu na nina Imani nae atakua na familia yake.

Mara nafika ofisin mida ya jioni naona namba ngeni inaita, kupokea mara ni mimi mume wako F, nikacheka na tabasamu la furaha. Akaniuliza uko wapi nikamwelekeza ofc yangu, yeye anaishi Arusha ndo anakofanya kazi, nikamwambia ok , cha kwanza aliniuliza ushaolewa nikamwambia ndio na nina watoto 2, nikamwomba nitampigia baadae sababu nilikua biz kidogo, saa kumi na moja natoka oficn akanipigia nikaongea nae kwenye gari mpaka nafika nyumbani, tukapiga story nyingi.

Ila siku zinavyozid kwenda ndo anazzidi kutaka kuwa karibu na mimi, mara nikapata parcel ya dhl ina zawadi iliyoambatanishwa na picha ipo katika frame tuliopiga mi na yeye enzi tupo s.africa kwakweli nilikumbuka mbali, nilipiga simu na kumwambia asante na nimeiweka ofcn kwangu. Ila nami nampenda na alinitamkia nimekupata tena sitegemei kukupoteza tena.

Juzi nimemtumia msg ndefu nikamweleza ukweli mimi siwezi kuendelea nae sababu mi nin familia yangu nae ana familia yake sasa kila mtu achukue time yake, kwakweli kanitumia msg nyingi sana kaniomba nisifanye ivyo, nimeamua ni mblock kila mahala ila cha kushangaza kanunua laini nyingi kwa ajili yangu nayo nimeblock, anatumia line nyingine, kwa sababu kila navyoendelea kuchati nae name nazidi kumpenda ili kuepusha imebid nifanye ivyo. Sasa jana nimeka nimewaza mengi sana juu yake na nina mpenda na nikiangalia upande wa mume wangu nae kanitenda sana ila mi sitaki kufanya ivyo sababu wakati wa kufunga ndoa niliungama pale mbele nikasema huyu ndo awe mume wangu mpaka kufa… kwakweli in short alikua chagua langu na nilikua nampenda ila wanavyosema ndoa upangwa na Mungu ndo maana tulipoteana.
Nunua line mpya full stop!Huyo kadhamiria kukuharibia
 
na hivi una stress za kutendwa plus mlikua na mahaba lundo enzi hzo wala nsikudanganye mama wewe utaliwa tu iwe leo au kesho....
 
Back
Top Bottom