ufumawicha
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 504
- 209
Leo asubuhi nimekutana na kitu cha ajabu. Mpaka sasa mwili unasisimka! Tofauti na binadamu wa kawaida yeye macho yake yako kifuani na siyo mawili bali manne!Ukweli miguu sikuiona ila kichwa kilikuwepo na hata mikono!Kadri nilivyozidi kumsogelea nilikuwa nikipigwa na upepo mithili ya beach.
Ilifika hatua uzalendo ukanishinda na kutimua mbio mpaka nilipofika barabara kuu ambapo nashukuru magari yalikuwa yakipita. Ajabu alikuwa kavaa nguo ambayo hadi sasa nimeshindwa kujua ni rangi gani maana ilikuwa ikibadilika. Macho niliweza kuyaona kwasababu mboni zilikuwa za kijani kali.