Nimekutana na mwanamke wa ajabu jioni ya leo. Jina la Bwana lihimidiwe

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Mbali na kuwa kwenye ndoa ya wake wawili waaminifu, nina mchepuko wangu anayeishi mtaa fulani. Mchepuko huyu nilimpatia mtaji, kwa kuwa yuko na akili ya maisha, alifanikiwa kufungua biashara na kuiendesha yeye kama yeye, biashara yenyewe ni ya uuzaji wa mboga i.e nyama za ndege, yaani kuku na bata

Mbali na kuwa na biashara yake inayompatia mamilioni ya pesa kwa siku, mchepuko huyu hana moyo wa huruma, kila siku huniomba pesa ya meza kana kwamba huwa ninakula kwake kila siku. Naumia sana ila najikaza kisabuni. Kuna muda mchepuko huyu hudiliki kuniomba pesa ya kujinunulia nguo au pedi, hapo ndipo huwa natamani kukipangua kibanda chake kwa mateke ya hapa na pale maake naona hakina msaada naye. Kuna siku nilitamani kumuwasha mbata hadharani pale aliponiambia eti tumtumie mama yake pesa ya sukari. Sasa biashara yake inamsaidia nini? Kwani mimi ni mumewe?

Mida ya saa kumi na mbili leo hii, amekuja binti mmoja mzuri na wa kuvutia, umbo lake lilifanana na chupa ya soda ya cocacola lililofunikwa na ngozi swaafi ya mzeituni, mkono wake wa kushoto uliushikilia mkono wa kuume wa kijana mmoja wa kufanana naye, nilidhani nimetembelewa na malaika wasio na mabawa

Basi bwana, nikaamua kuwalaki. Binti alikuwa si haba akaamua kuulizia bei ya nyama hizo, nikawa nimemtajia elfu tatu kwa elfu saba. Baada ya kushauriana, binti akaniomba nimfungie mboga ya 10k, muda huo yule kijana alikuwa akibubujikwa kijasho chembamba kuuzunguka mwili wake kuashiria hali ngumu ya maisha huku macho yake yakionesha wazi kuomba kikombe hicho kimuepuke

Kijana yule wa kiume ndipo kuniuliza totali ya mboga ile, baada ya kumwambia 10k aliingia kwa wallet na kuchomoa 10k iliyochakaa huku akiacha vumbi tu kwenye wallet ile. Binti alimuangalia kijana yule kwa huruma sana kisha kumwambia, "Usiwaze Denis, acha tu ntalipa". Mimi na Denis bila kumsahau mchepuko wangu tulipigwa na butwaa, ila mimi nilipigwa na butwaa kubwa kuwazidi wote huku nikiutazama ule mchepuko na kutikisa kichwa mithili ya mganga wa Yoruba kumwelekezea mchepuko kumaanisha kuwa mchepuko wangu ni kichwa box tupu la mbao

Niliipokea ile hela ya binti kwa heshima kubwa na taazima huku nikisindikizwa na mizinga mizito kutoka moyoni huku nikitoa matamshi ya kumchoma mchepuko wangu. Sauti ya Denis iliyonena, " Acha tu mpenzi, nitalipa mwenyewe tu" ilitaradadi kwa huruma ya hali ya juu pasi na kusikilizwa

Nilibaki nikimtazama binti akiwa anaishiria kuelekea kusikojulikana huku nikimuomba Mola anijaalie binti kama huyo ili awe mke wa tatu, au anipatie huyo huyo kama ikiwezekana

Ndipo kumuaga mchepuko huyo na kurejea nyumbani. Muda huu nipo kwa mke mdogo, tayari nimekwisha oga, nasubiri kuichapa baada ya makala kwa runinga
 
Sasa mchepuko akurumie kwa muamana upi, it's benefit based relationship na wanawake wanajua kustand their position, wewe utapata sex only nae atapata mahitaji yake yote kwako, Hela anayoingiza kwenye biashara ni yake.
We chakata mbususu sawasawa ukichoka kimbia.
Chukua chako mapema uchepukaji Hauna mafao ya uzeeeni
 
Sasa mchepuko akurumie kwa muamana upi, it's benefit based relationship na wanawake wanajua kustand their position, wewe utapata sex only nae atapata mahitaji yake yote kwako, Hela anayoingiza kwenye biashara ni yake.
We chakata mbususu sawasawa ukichoka kimbia.
Chukua chako mapema uchepukaji Hauna mafao ya uzeeeni
Na kweli mkuu, anapouona mpododo wake unazidi kunawili kila siku, anataka kuutumia kama silaha ya kunifilisi pesa zangu za ukoo. Wanawake hawana dogo kwa kweli
 
Back
Top Bottom