Nimekutana na binadamu wa ajabu alfajiri hii

Nimekutana na binadamu wa ajabu alfajiri hii

ungepiga picha..sasa mimi nitaamini vipi kama alikua wa ajabu? kama ulipiga piga weka picha
 
Inawezekana ni mauzauza lakini ulimwengu umejaa viumbe vionekanavyo na vingine vya maajabu.

Nimeshawahi kukutana na matukio kama hayo Mwenge Kanisani na kiwanja cha mpira mwenge. Mida ni saa kumi na moja kasoro. Matukio tofauti na venue tofauti, niliona kiumbe cha ajabu na kikatoweka ila sikuogopa wala kukimbia

Kanisa gani? Lile la Maxmillian Kolbe?
 
Mpotezee tu atakuwa kwenye issue zake huyo mwanamke, si unaona mpaka sasa hakuna lolote la maana
 
Mwaka 2004 ilikua saa11 alfajiri mkoani mbeya. Natoka sokomatola naenda stand kuu huku nakimbia. Ghafla nasikia vishindo vya mtu mwingine nyuma yangu nikasimama nikageuka hamna mtu, ghafla nikavisikia tena nyuma vikanipita kuelekea kule nilipotoka tena. Unajua nini kilichofuata?

Hahaha kilichofuata vumbi au
 
Alfajiri kunakuwanga na matukio ya ajabu sana.... Mm kuna siku mida ya saa 11 asbhi nikiwa naelekea kwenye mishe zangu kuna chochoro huwa napitia, ile kukunja tu nakutana na furushi la kiroba alafu linacheza cheza, kila nikijaribu kulikwepa nipite lenyewe nalo linasogea upande huo huo, nikaona isiwe taabu nikageuza nikapita njia nyingine... Mpaka leo najiuliza kilikuwa ni nn kile sijapata jibu mpaka leo.

Mkuu umenichekesa sana, ungeliruka.
 
Kumbe mwanamke akivaa hijabu nyekundu na akiwa na sauti nyororo anakuwa kiumbe wa ajabu?? Duuh noma sana
 
Hijabu !.JPG
 

Attachments

  • Hijabu.JPG
    Hijabu.JPG
    42.3 KB · Views: 395
halafu wewe uache kutuletea thread za kitoto kama hizi sawa nenda jukwaa la watoto hv wewe umuoni K4LIFE anavyoandika thread za akili kwa jamii ya watanzani? jifunze kutoka kwa K 4 LIFE

Bora za huyu kuliko zile zako unazoletaga humu ovyo ovyo!
 
Mwaka 2004 ilikua saa11 alfajiri mkoani mbeya. Natoka sokomatola naenda stand kuu huku nakimbia. Ghafla nasikia vishindo vya mtu mwingine nyuma yangu nikasimama nikageuka hamna mtu, ghafla nikavisikia tena nyuma vikanipita kuelekea kule nilipotoka tena. Unajua nini kilichofuata?

Bila Shaka Ulipiga Mayowe Ya Kuomba Msaada Huku Ukiwa Mguu Sawa Tuliiii.
 
Nikiwa njiani kuelekea kwenye mihangaiko ya maisha nikielekea kwenye shughuli zangu saa 11:15 alfajiri hii (mji nahifadhi) nimekutana na mwanamke akiwa kavaa hijabu nyekundu kanisalimia,sauti yake nyororo sana eneo nililokutana mwanamke huyu ni darajani,daraja nilikuwa nimeshalipita mita kadhaa,nilipogeuka nyuma nashangaa kumuona mwanamke yule anaingia darajani,siyo siri nimetoka mbio wanajamvi sijui ni kitu gani.

samahani mkuu naomba kuuliza,hivi alfajir hiyo ulikuwa hujagonga "kitu cha meru" kama kawaida yako?
 
Alikuwa anaenda kutimiza masharti yake ya makafara tu huyo. Ndiyo mida yao hiyo.
 
Mambo ya dunia hayo.
Nakumbuka nikiwa darasa la 5 kipind cha kuwahi namba shulen, niliamka mapema sana kwenye mida ya saa 10 afajiri. Nikiwa njian kuelekea shulen kuna sehem pana bonde la mto, hilo bonde lina urefu kama mita mia hvi. Sasa nikiwa nakatisha hilo bonde nikawa nawaona watu kwa mbele na naskia sauti zao wakiwa wanaongea ikabidi mm niongeze mwendo ili niungane nao kulivuka hilo bonde. Kila nikiongeza mwendo nikawa siwafikii nilipofika karibia na kulimaliza hilo bonde nikawa siwaon na wala sauti skuzisikia baadae nilipokaribia kulimalizia hilo bonde nikaanza kusikia tena sauti zao zikitokea nyuma nilikotokea nikageuka kuangalia nawaona wanakuja wananifuata kwa nyuma. Aisee nikakimbia na kila ninavyokimbia nikawa naanguka.
 
Huyo ni jini mahaba anakufuatilia.na ataendelea kukufuatilia hadi usingizini hadi uingie kwenye 18 zake.
 
Kwanza nikuulize uliitikia au hukuuitikia hiyo salamu km uliitikiaa tafuta halua na marashi nakitambaa chekundu ukilala vieke kwenye pembe ya chumba usiku ukiamka asubui ukivikuta havijafanywa lolote ni binaadam ukikuta kuna changing yoyote ujue unae😀😀😀😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom