Nimekumbuka zamani

Wakubwa walikuwa wanasema ni watu...



Kama ni 2014 kwenda nyuma basi ndio maana sijaona ni zamani ya ambayo mimi naiona zamani...
Kwamba watu wananyonyana damu looh๐Ÿ˜„,.

Kuna wale wengine chinja chinja eti wanakata vidude vya wanaume,. Ila wazazi walijua kututishia enzi zile
 
Siku zinasogea saaana aisee,. Ila maisha ya kuishi ndugu wengi pamoja ni raha sana
Hapa ndio uwa nawasifu wahindi na waarab, kuna namna hata bond inaimarika sana koo ikiwa pamoja, huwezi sikia sijui wamepigana kwenye michongo tofauti na sisi, unamuweka mtoto wa mjomba kwenye michongo ambaye mlikuwa mnawasiliana tu kwenye simu, lazima ukae.

Siku hizi kwa bibi ni mjini hawapati tena uzoefu kama huu, nashukuru mi kwetu angalau kwa mbinde uwa tunaonana kiukoo ingawa ndio hivyo babu na bibi walishatangulia.
 
Vingi ulivyosimulia ni kama unasimulia uzoefu wangu ๐Ÿ˜€, kweli Tanzania ni nchi ya kijamaa hapa unazungumzia uzoefu wa usukumani lakini mi narelate hayo mambo kwa 85%+ na ya unyakyusani.

Teknolojia imetuharibia sana lifestyle siku hizi madogo likizo wanaishi kama mazombie, ni Ps na tablet asubuhi mpaka usiku 24/7
 
Yes mara nyingi tamaduni zetu zinafanana sana mkuu. Ukweli muda mwingine nikifika huko Kwa bibi na Kuta mapori yameshafyekwa nalilia moyoni. Madogo wa Sasa hawana jipya la kututishia
 
Yes mara nyingi tamaduni zetu zinafanana sana mkuu. Ukweli muda mwingine nikifika huko Kwa bibi na Kuta mapori yameshafyekwa nalilia moyoni. Madogo wa Sasa hawana jipya la kututishia
Hawa wakina junior bure kabisa, siku hizi hata kuogelea wanaenda fundishwa kwenye swimming pool na walimu wao.

Ingawa mi kwabibi bado kupo ila wenyewe ndio hawapo, mara moja moja familia uwa tunakutana lakini siku haiwi na hekaheka nyingi kama zamani, siku hizi tunaokula tungi tunakaa na wenzetu, wazee wa kanisa kivyao vyao. Tabia zimebadilika na mambo yamebadilika ila nashukuru angalau tunaonana.
 
Sisi kwetu likizo ilikua kama camp ya mateso ni mwendo kwenda shamba hapo kulima, kuchimba mashimo ya kupanda migomba, kutifua & kupalilia pia kusomba majani hapo mpaka likizo iishe ushakua mweusi mweusi hivi
Hahahaa ila hiyo nzuri
 
Waw! Kumbe wapo watu humu jamvini hawaijui koroboi na taa za chemli. Heri zao.
 
Hakika
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi michezo yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Na kuchunga mbuzi na cha kufurahisha enzi hizo hakuna matukio ya ajabu ajabu.
 
Mnacheza huko hadi mbuzi zinapotea๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
kuna siku yalinikuta, michezo imetukolea mbuzi zikarudi zenyewe nyumbani, sasa shida sio kurudi nyumbani shida ilianzia babu kashaziona nyumbani alafu kaja kutuchora tulitafuta wote mbuzi zaidi ya lisaa ๐Ÿ˜‚
 
kuna siku yalinikuta, michezo imetukolea mbuzi zikarudi zenyewe nyumbani, sasa shida sio kurudi nyumbani shida ilianzia babu kashaziona nyumbani alafu kaja kutuchora tulitafuta wote mbuzi zaidi ya lisaa ๐Ÿ˜‚
Hahahahahahah na mbuzi zikipotea giza likiingia zinarudi nyumbani zenyewe nyie mtatafuta hadi vijiji vya jirani. Kwa babu yako ni mkoa upi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ