Nimekumbuka zamani

I miss those golden moments, kwa sasa watu wamekuwa wabinafsi kupitiliza, sio ajabu hata ndugu mnaokaa mkoa mmoja kutotembeleana, watoto wa ndugu hawafahamiani,
Teknolojia imeleta maisha ya ajabu sana, ule ukaribu wa zamani haupo tena.ni kawaida ukienda kusalimia kwa ndugu kuulizwa unarudi kwako lini?
Zamani ilikuwa ni burudani sana kukutana pamoja ndugu, watoto na wajukuu hasa mwisho wa mwaka maana ndo kipindi ambacho watu wengi walikuwa na nafasi hiyo.Babu na bibi wanafurahia kuona matunda ya watoto wao( kucheza na kuwa na wajukuu zao) .Haya yote yamebaki historia kwa jamii nyingi.
Asante sana mleta mada umenikumbusha mbali sana.Kwa sasa tunaishi nyakati za hivyo sana
 
Of course yes,. Teknolojia imeleta mambo ya ajabu sana,.. Ndugu hatutembeleani kama zamani
 
Ulipotaja mambo ya Simu na TV, CD ndipo nilipogundua kuwa, rafiki yangu hauna uzamani wa mbali sana na Dunia ya sasa.
Maana wa Zamani ya nyuma yako, hakukua na Simu hizi za kila mtu yake, bali simu za uma, na nyumba yenye kuvutiwa Simu hiyo nyumba ni mboga saba.
Zamani hiyo hakukua na TV mambo ya Tv yalianza mwishoni miska ya 80 miaka ya 90 ikanza kuenea Ungo wa wavu, ukiona nyumba ina Ungo ni mboga saba sanasana ungo unaona nyumba masaki huko, na 90 hiyohiyo ndipo mambo ya Simu za mkononi yakanza.
 
Huko zamani sana mkuu aisee,. Mie nazungumzia miaka kuanzia 2014 kurudi nyuma huko ndio nilikuwa shule ya msingi
 
Yaanii,. Sikuizi watoto hata hawana utaratibu kwa kwenda kusalimia kwa bibi
Mbona wanaenda! Wa kwangu kwa vile uoande wangu nilishawapoteza wazazi wote basi wamebaki wanaenda upande wa mama yao! Ni hivyo hivyo ulivyosimulia na wa kwangu wakienda kwa bibi yao!
 
Mkuu we ni wa mwaka gani kama mlikuwa mnatumia CD kucheki movie,ungekuwa wa zamani kidogo mngetumia VHS(yale mamikanda makubwa kama ka biblia)
 
Sema sijui hawa wazee hela walikuwa wanatoaga wapi?,. Maana kwenye suala la kula kuanzia asubuhi mpaka usiku na wanalisha wajuu na wanafamilia kibao aisee walijitahidi
Usishangae ilikuwaje. Nyuma ya pazia ni kwamba nyie mnapokuwa mpo huko mjini au Shuleni(bweni) huku wazee walikuwa ni kilimo kwa kwenda mbele. Likizo zenu Pasaka au June (nusu mwaka) baadhi ya mazao yanakuwa yamekomaa ile ya Desemba mavuno yote yanakuwa yameshatoka mashambani inabaki ni kuuza au kula huku wakisubiri tena mzunguko mwingine wa mazao uanze. Lakini siku hizi wazee eti wanaenda kijiweni nao kubishanIa Simba na Yanga- WAZEE WA KUWEKA MZIGO
 
Wananiita updated generation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…