Nimekumbuka tulivyovamiwa geto na wananzengo tukiwa chuo mwaka wa pili

Ironbutterfly

JF-Expert Member
Feb 5, 2023
3,044
8,165
Habari za mida hii wanajukwaa, nimekuja Dom kufatilia ishu zangu za kiofisi, niko Lodge sema usingizi umepaa. Ngoja niwape kisa hiki kilitokea miaka hiyo tukiwa chuo mwaka wa pili na shost yangu Cecy.

Kama mjuavyo miaka ile ilikuwa mkiingia second year kupata hostel chuoni ni mtiti aidha upate mtu akubebe, basi mie na shost yangu Cecy tulikuwa tunakipiga COET, tukapanga maeneo ya geti maji, maeneo ya wenyeji, jirani na yale majengo ya watumishi wa chuo. Tulikuwa tunaishi mimi, shost yangu Cecy na binamu yake Salome, yeye alikuwa anasoma Ualimu wa Msingi chuo fulan kulikuwa Kimara pale.

Ile nyumba tuliyopanga ilikuwa kama hostel, ikiwa na vyumba kama kumi hivi, na mostly tuliokuwa tumepanga pale ni wanafunzi wa chuo, mostly wakiwa wanaume. Ni vyumba viwil vya nje ndio alikuwa amepanga baba mmoja na mkewe.

Sasa pale palikuwa full uhuru, kila mtu anaingia na kutoka muda wake, kutokana na ratiba yake ya vipindi, hivyo lango kuu lilikuwa wazi muda mwingi.

Nakumbuka ilikuwa jumapili moja tulivu, mie baada ya ibada, nikamwaga Cecy nikarud geto, kupata msosi na kupumzika, yeye Cecy akabaki kanisani (ni makanisa haya wa walokole), nilikuwa wakati mwingine tunaongozana huko kusali, ingawa mie ni Mroma. Yeye alikuwa na kawaida ya kubaki kanisan kuongea na wachungaji na wanakwaya, then anarud kujisomea chuoni na wanagroup, si mwaelewa tena mziki wa COET.

Mie nikarudi geto, nikakuta binamu yake Salome kashakorofisha (alikuwa mpishi mzuri, na yeye alikuwa hachangi hela ya chakula, tulikuwa tunachanga sisi yeye anapika, na pia alikuwa free muda mwingi kutokana na alichokuwa anasoma) pia yeye alikuwa hapendi kuhudhuria ibada. Tukala na kuendelea kuangalia michezo runingani, na story za hapa na pale. Cecy akarudi kwenye saa 12 jioni akala, halafu akaaga kurudi chuo kwani alikuwa na test kesho yake.

Saa mbili tukapata dinner mimi na Salome, then mie nikatazama movie moja (mie ni mpenzi wa movies sana) thenby saa 3 usiku nikapanda kitandani, kuikamilisha siku.

Imefika kwenye saa 6 usiku Cecy akarudi, nikastuka usingizini, manake alikuwa na funguo, nikaendelea kujilaza huku nikiwa nusu usingizini, nusu kama niko macho, akaanza kutoa kubadili nguo, ghafla mlango ukagongwa.

Cecy akauliza we Joy kama hukuelewa tutamalizia kesho (joy tulikuwa tunasoma naye). Mara mlango ukasukumwa wakaingia wanaume watatu wamevaa mask, halafu mmoja kabeba gobole na mwingine kashika panga.

Mmie bado nimepigwa na bumbuwazi pale kitandani nilipojilaza, akilini nikawa najiuliza, huyu Cecy amekuwaje leo anawakaribisha hawa wanaume ndani nasi tumelala na yeye alikuwa na kyupi tu (nilidhan ni wanafunzi wenzetu wa kiume aliokuwa anadiscuss nao).

Kabla sijaongea lolote jamaa aloshika gobole akalielekeza kwa Cecy, halafu akafanya ishara ya kutaka tufumbe midomo, hapo ndio nikapata fahamu akilini kuwa tumevamiwa. Nikakumbuka kinokia changu cha batani nikapitisha mkono chini ya mto nikakifutika kwenye kyupi🤣.

Jamaa aliyeshika gobole akaniona, akanambia unaficha nini, nikamjibu hakuna kitu, wakaanza kuulizia laptop, wakakosa maana yangu nilikuwa nimeiweka chini ya kitanda, Cecy ya kwake aliiweka kwenye mikoba hii ya kike ya kitambaa akawa ameutundika mkoba kwenye kiti, hivyo hawakuiona.

Wakasema begi la laptop hili hapa, laptop iko wapi? Nikajibu haraka tumeziacha chuoni, basi wakadai fedha, Cecy alikuwa na kielfu kumi wakachukua, pamoja na simu yake na ya Salome.

Wakatutaka tuzime taa tufunge mlango, tusipige kelele yoyote, tukikiuka wataturudia, tukafanya hivyo. Basi waliiba kwenye ile hostel vyumba vyote kwa stahili hiyo ya kimya kimya. Asubuhi tukadamkia chuo, baada ya test na vipindi kadhaa, tukamtafuta dalali tukahama pale. Ilikuwa experience moja mbaya sana kwenye maisha yangu ya chuo.
 
basi hao walikua majambazi waliookoka😂
Isitoshe chumba chetu ndio kilikuwa Cha kwanza ukiwa unaingia kwenye nyumba Ile,so walianza kuiba kwetu ndo wakavamia na vyumba vingine,tena vilivyokuwa na wanaume tupu,but trust me wote waliizwa laptop zao na simu na hakuna aliyekaid,ilipita kama lisaa wakaanza kupiga kelele za mwizi ilhali wajuba walikuwa washasepa🤣🤣
 
Habari za mida hii wanajukwaa,nimekuja Dom kufatilia ishu zangu za kiofisi,niko Lodge sema usingizi umepaa.
Ngoja niwape kisa hiki kilitokea miaka hiyo tukiwa chuo mwaka wa pili na shost yangu cecy.

Kama mjuavyo miaka ile ilikuwa mkiingia second year kupata hostel chuoni ni mtiti aidha upate mtu akubebe,basi mie na shost yangu cecy tulikuwa tunakipiga coet,tukapanga maeneo ya geti maji,maeneo ya wenyeji,jirani na yale majengo ya watumishi wa chuo.Tulikuwa tunaishi Mimi, shost yangu cecy na binamu yake Salome,yeye alikuwa anasoma ualimu wa msingi chuo flan kulikuwa kimara pale.

Ile nyumba tuliyopanga ilikuwa kama hostel,ikiwa na vyumba kama kumi hivi,na mostly tuliokuwa tumepanga pale ni wanafunzi wa chuo, mostly wakiwa wanaume.Ni vyumba viwil vya nje ndio alikuwa amepanga baba mmoja na mkewe.

Sasa pale palikuwa full uhuru,kila mtu anaingia na kutoka muda wake,kutokana na ratiba yake ya vipindi,hivyo lango kuu lilikuwa wazi muda mwingi.
Nakumbuka ilikuwa jumapili moja tulivu,mie baada ya ibada,nikamwaga cecy nikarud geto,kupata msosi na kupumzika,yeye cecy akabak kanisani,(ni makanisa haya wa walokole),nilikuwa wakati mwingine tunaongozana huko kusali,ingawa mie ni mroma.Yeye alikuwa na kawaida ya kubak kanisan kuongea na wachungaj na wanakwaya,then anarud kujisomea chuoni na wanagroup,si mwaelewa Tena mziki wa coet.

Mie nikarudi geto,nikakuta binamu yake salome kashakorofisha(alikuwa mpishi mzuri,na yeye alikuwa hachangi hela ya chakula,tulikuwa tunachanga sisi yeye anapika,na pia alikuwa free muda mwingi kutokana na alichokuwa anasoma )pia yeye alikuwa hapend kuhudhuria ibada.Tukala na kuendelea kuangalia michezo runingani,na story za hapa na pale.Cecy akarudi kwenye saa 12 jioni akala,afu akaaga kurudi chuo kwani alikuwa na test kesho yake.

Saa mbili tukapata dinner Mimi na Salome,then mie nikatazama movie moja(mie ni mpenzi wa movies Sana) thenby saa 3 usiku nikapanda kitandan,kuikamilisha siku.
Imefika kwenye saa 6 usiku cecy akarudi,nikastuka usingizini,manake alikuwa na funguo, nikaendelea kujilaza huku nikiwa nusu usingizini, nusu Kama Niko macho,akaanza kutoa kubadil nguo,ghafla mlango ukagongwa,cecy akauliza we joy kama hukuelewa tutamalizia kesho,(joy tulikuwa tunasoma naye),
Mara mlango ukasukumwa wakaingia wanaume watatu,wamevaa mask,afu mmoja kabeba gobole na mwingine kaahika panga,mie bado nimepigwa na bumbuwazi pale kitandani nilipojilaza,akilini nikawa najiuliza,huyu cecy amekuwaje leo anawakaribisha Hawa wanaume ndani nasi tumelala?na yeye alikuwa na kyupi tu (nilidhan ni wanafunzi wenzetu wa kiume aliokuwa anadiscuss nao).

Kabla sijaongea lolote jamaa aloshika gobole akalielekeza kwa cecy,halafu akafanya ishara ya kutaka tufumbe midomo,hapo ndo nikapata fahamu akilin kuwa tumevamiwa,nikakumbuka kinokia changu Cha batani nikapitisha mkono chini ya mto nikakifutika kwenye kyupi🤣

Jamaa aliyeshika gobole akaniona,akanambia unaficha nini,nikamjibu hakuna kitu,wakaanza kuulizia laptop,wakakosa manake yangu nilikuwa nimeiweka chini ya kitanda,cecy ya kwake aliiweka kwenye mikoba hii ya kike ya kitambaa akawa ameutundika mkoba kwenye kiti,hivyo hawakuiona.

Wakasema begi la laptop hili hapa ,laptop iko wapi?nikajibu haraka tumeziacha chuoni,basi wakadai fedha, cecy alikuwa na kielfu kumi wakachukua,pamoja na simu yake na ya Salome.

Wakatutaka tuzime taa tufunge mlango,tusipige kelele yoyote,tukikiuka wataturudia,tukafanya hivyo.Basi waliiba kwenye Ile hostel vyumba vyote kwa stahili hiyo ya kimya kimya.Asubuh tukadamkia chuo,baada ya test na vipind kadhaa,tukamtafuta dalali tukahama pale.Ilikuwa experience moja mbaya sana kwenye maisha yangu ya chuo.
Pole sana mpenzi wangu, mbona hujawahi kuniambia?
 
Habari za mida hii wanajukwaa, nimekuja Dom kufatilia ishu zangu za kiofisi, niko Lodge sema usingizi umepaa. Ngoja niwape kisa hiki kilitokea miaka hiyo tukiwa chuo mwaka wa pili na shost yangu Cecy.

Kama mjuavyo miaka ile ilikuwa mkiingia second year kupata hostel chuoni ni mtiti aidha upate mtu akubebe, basi mie na shost yangu Cecy tulikuwa tunakipiga COET, tukapanga maeneo ya geti maji, maeneo ya wenyeji, jirani na yale majengo ya watumishi wa chuo. Tulikuwa tunaishi mimi, shost yangu Cecy na binamu yake Salome, yeye alikuwa anasoma Ualimu wa Msingi chuo fulan kulikuwa Kimara pale.

Ile nyumba tuliyopanga ilikuwa kama hostel, ikiwa na vyumba kama kumi hivi, na mostly tuliokuwa tumepanga pale ni wanafunzi wa chuo, mostly wakiwa wanaume. Ni vyumba viwil vya nje ndio alikuwa amepanga baba mmoja na mkewe.

Sasa pale palikuwa full uhuru, kila mtu anaingia na kutoka muda wake, kutokana na ratiba yake ya vipindi, hivyo lango kuu lilikuwa wazi muda mwingi.

Nakumbuka ilikuwa jumapili moja tulivu, mie baada ya ibada, nikamwaga Cecy nikarud geto, kupata msosi na kupumzika, yeye Cecy akabaki kanisani (ni makanisa haya wa walokole), nilikuwa wakati mwingine tunaongozana huko kusali, ingawa mie ni Mroma. Yeye alikuwa na kawaida ya kubaki kanisan kuongea na wachungaji na wanakwaya, then anarud kujisomea chuoni na wanagroup, si mwaelewa tena mziki wa COET.

Mie nikarudi geto, nikakuta binamu yake Salome kashakorofisha (alikuwa mpishi mzuri, na yeye alikuwa hachangi hela ya chakula, tulikuwa tunachanga sisi yeye anapika, na pia alikuwa free muda mwingi kutokana na alichokuwa anasoma) pia yeye alikuwa hapendi kuhudhuria ibada. Tukala na kuendelea kuangalia michezo runingani, na story za hapa na pale. Cecy akarudi kwenye saa 12 jioni akala, halafu akaaga kurudi chuo kwani alikuwa na test kesho yake.

Saa mbili tukapata dinner mimi na Salome, then mie nikatazama movie moja (mie ni mpenzi wa movies sana) thenby saa 3 usiku nikapanda kitandani, kuikamilisha siku.

Imefika kwenye saa 6 usiku Cecy akarudi, nikastuka usingizini, manake alikuwa na funguo, nikaendelea kujilaza huku nikiwa nusu usingizini, nusu kama niko macho, akaanza kutoa kubadili nguo, ghafla mlango ukagongwa.

Cecy akauliza we Joy kama hukuelewa tutamalizia kesho (joy tulikuwa tunasoma naye). Mara mlango ukasukumwa wakaingia wanaume watatu wamevaa mask, halafu mmoja kabeba gobole na mwingine kashika panga.

Mmie bado nimepigwa na bumbuwazi pale kitandani nilipojilaza, akilini nikawa najiuliza, huyu Cecy amekuwaje leo anawakaribisha hawa wanaume ndani nasi tumelala na yeye alikuwa na kyupi tu (nilidhan ni wanafunzi wenzetu wa kiume aliokuwa anadiscuss nao).

Kabla sijaongea lolote jamaa aloshika gobole akalielekeza kwa Cecy, halafu akafanya ishara ya kutaka tufumbe midomo, hapo ndio nikapata fahamu akilini kuwa tumevamiwa. Nikakumbuka kinokia changu cha batani nikapitisha mkono chini ya mto nikakifutika kwenye kyupi.

Jamaa aliyeshika gobole akaniona, akanambia unaficha nini, nikamjibu hakuna kitu, wakaanza kuulizia laptop, wakakosa maana yangu nilikuwa nimeiweka chini ya kitanda, Cecy ya kwake aliiweka kwenye mikoba hii ya kike ya kitambaa akawa ameutundika mkoba kwenye kiti, hivyo hawakuiona.

Wakasema begi la laptop hili hapa, laptop iko wapi? Nikajibu haraka tumeziacha chuoni, basi wakadai fedha, Cecy alikuwa na kielfu kumi wakachukua, pamoja na simu yake na ya Salome.

Wakatutaka tuzime taa tufunge mlango, tusipige kelele yoyote, tukikiuka wataturudia, tukafanya hivyo. Basi waliiba kwenye ile hostel vyumba vyote kwa stahili hiyo ya kimya kimya. Asubuhi tukadamkia chuo, baada ya test na vipindi kadhaa, tukamtafuta dalali tukahama pale. Ilikuwa experience moja mbaya sana kwenye maisha yangu ya chuo.
Poleni sana! Tz wezi mpaka kwa wanafunzi!!
 
Back
Top Bottom