Nimekumbuka makala za Kisa na Mkasa kwenye gazeti la Raia Mwema.

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Siku hizi hamu ya kusoma magazeti imeniishia kabisa. Siku za nyuma kidogo nilikuwa siwezi kukosa nakala ya Raia Mwema kila Jumatano, MwanaHalisi kila Jumatatu, Mawio kila Alhamis na Jamhuri kila Jumanne.

Magezeti yalikuwa yakiandika kweli kweli makala za kusisimua. Ukimaliza makala moja lazima upumzike kwanza kabla ya kuendelea na nyungine. Makala za kisa na mkasa zikinivutia kweli kweli kwani zilikuwa zikiakisi kesi mbali mbali zilizowahi Kutoe duniani hasa Marekani na Ulaya.

Kesi hizo zilikuwa ngumu kweli kuzichunguza kutokana na mazingira take.
Kuna kisa kimoja kilitokea huko Marekani mwanaume mmoja kumuua mkewe wakiishi miji tofauti kama km 900.

Mme alikodi gari nyingine akenda mji aushio mkewe kufanya mauaji usiku kwa usiku na akarudi usiku huo huo ili kupoteza ushahidi.

Uchunguzi ulipoamza ikawa vigumu sana kumhusisha yule mwanaume na mauaji ya mke wake. Lakini kwa ubobezi wa wapelelezi wa kesi ili wakajua muuaji alitumia gari la kukodi lile gari likafanyiwa uchunguzi kwenye Kabyureta kutafuta wadudu walionasa kwa mbele na kuwafananisha na wale wapatikanao kule mauaji yaliko tokea wakakuta wadudu wale wanafanana kwa kila kitu.

Muuaji kuja kubanwa akakili kuhusika.

Hapa ndoo huwa najiuliza kwanini kesi zetu hucheleweshwa sana mahakamani ni kwa kuwa hatuwezi kupeleleza vizuri au tuna upungufu wa vitendea kazi.
Kumbe inawezekana hata wasio julikana wakajulikana tukiwekeza kwenye taalum ya upelelezi. Tunaweza hata kuwajua waliojaribu kumuua Tundu Lissu. Tunaweza kuwajua wanaojaribu kuifisidi nchi yetu. Tunaweza kuwajua wanao waua Albinos. Tunaweza kuwajua wanaoua wazee na wanawake wa nchi hii.
 
mkuu kila kitu kinawezekana hasa kwenye dunia ya leo, ukiona tukio kubwa kama la lissu limepuziwa ujue mamlaka inawajua wahusika, chukulia mf mdogo tu, itokee polisi imeoyang'anywa bunduki mtaani, mbona hua haichukui round wanaipata?
 
mkuu kila kitu kinawezekana hasa kwenye dunia ya leo, ukiona tukio kubwa kama la lissu limepuziwa ujue mamlaka inawajua wahusika, chukulia mf mdogo tu, itokee polisi imeoyang'anywa bunduki mtaani, mbona hua haichukui round wanaipata?
Sijui tunashindwa wapi kwenye hilo
 
Back
Top Bottom