Nimekumbuka hii nikacheka sana; tuliowahi kukojoza kitandani tukiwa boarding njooni tutoe ushuhuda

3D6C14DE-F259-4C0F-AF8E-C01C99D3FBC4.jpeg
Ila inasemekana kikojozi hasinzii ugenini. Ya kweli hayo?!
 
Wakuu Kwema!

Leo Taikon nimekumbuka Maswahibu yaliyonikuta nikiwa Advance huko Matema Beach High School, Kyela mkoani Mbeya.

Taikon ni mtu wa Stori, mjanja mjanja, mcheshi, na mtu wa watu. Taikon ni mtu anayeongea na kila mtu. Hapendi mtu akwazike.

Siku zile nikafika shuleni, Kyela ikiwa ndio mara yangu ya Kwanza kabisa kufika Mkoani Mbeya.
Maisha Mapya yakaanza, nilifika kipindi cha baridi, ilikuwa mwezi wa tano, weeh! Kulikuwa na winter sio mchezo, kumbuka Mimi nimezaliwa na kukulia Makanya, huko Same ambapo Hali yake ya hewa ni joto Kali na jua linachoma mno. Hivyo ni Halali yangu kuona Hali ya hewa ya Kyela kuwa ya baridi na yenye kunikera.

Kwa Wale VIKOJOZI wote watakubaliana na Mimi kuwa hakuna kipindi kigumu kwao Kama msimu wa baridi, huwezi tenganisha msimu wa baridi na VIKOJOZI. Vikojozi wanaogopa na hawapendi msimu wa baridi kwani mfumo wa kukojoa hufanya kazi zaidi kuliko mfumo wa utoaji jasho.

Basi Taikon nikiwa tayari nimeshazoea mazingira, kijana msafi na mcheshi ambaye nilipenda Sana Stori za hapa na pale kwenye vijiwe au kutembelewa kwenye Cube/Room yetu na watu kuja kunisikiliza Stori zangu za uongo na kweli.

Siku hiyo isiyo na jina, nikawa nimelala, nikaota ndoto ya hovyo Sana.
Vikojozi watakubaliana na Mimi kuwa ili wakojoe yawapasa kuota ndoto aidha ya kutisha wanakimbizwa na majoka, au wanyama wakali au wanaota ndoto ya kujisaidia haja ndogo kumbe ndio wanalishusha kweli😎😎

Baada ya kuota ndoto Ile, nikashtuka. Maya weee! Nilikuwa nimekojoa tena mkojo ndio ulikuwa unamalizikia😪😪😪
Ulikuwa wamoto kweli, nikapapasa kitandani, Doooh! Jamani! Jamani! Nilikuwa limelishusha kojo jingi mno, bado lilikuwa linaelea kitandani kutokana na kuwa Godoro sikutoa lile nailoni.

Mashuka na blanket yalikuwa tepe tepe!😫😫
Sasa nikafikiri nifanyeje🤔🤔🤔 Kojo ndio Hilo, nimeshakiharibu. Nikacheka saa ilikuwa saa tisa inaelekea saa kumi usiku hiyo.

Nikatulia tuli kusikilizia movement yoyote ndani ya lile bweni, nikaona kimya, nikachungulia dirishani nikaona pametulia mpaka Kule madarasani.

Nikatoka kitandani na kutoka nje kukagua Mandhari, nikaona Hali ni shwari. Upesi upesi nikarudi nikafungasha Yale mashuka na blanket nikayachukua kuyapeleka Bafuni. Nikafanikiwa kuyaweka kwenye beseni, na kuyaloweka kwenye maji. 🤗🤗

Nikarudi kuchukua sabuni ya unga, mambo hayo yanafanyika haraka haraka Wazee😂😂😂, sitaki kukutwa na yeyeto.
Basi nikiwa narudi nikapishana na mshikaji mmoja Kidato cha sita.

Nilihakikisha hanipitii karibu si unajua sijabadili nguo bado, yaani nimelowa mamikojo😂😂 na ninanuka kweli. Nikafanikiwa kumpita, naye alikuwa anaenda chooni, aliponipita nikamgeukia yeye akiwa anaendelea kwenda chooni asijue namtazama, nikasema watu wengine nao, kuamka amka kila saa🤣🤣🤣 yaani nilikuwa na gubu kweli.

Nikabadili nguo nilizokuwa nimevaa nilizozikojolea, nikavaa zingine. Nikachukua Sabuni ya unga, nikawa namsubiri yule jamaa arudi ili niendelee na mishe zangu.

Dakika zinaenda naona harudi, kucheki saa imeingia saa kumi za usiku. Na hapo watakaoamka wataongezeka kujifanya wanapenda kusoma😏😏😏,
Nikaziwe zile nguo kwenye mfuko na Ile sabuni nikatoka nazo, muda huu nikiwa na tahadhari kwani najua Yule kijana yupo Uani.

Nafika namkuta anaongea na simu, Saa kumi hiyo, alikuwa anaongea kikurya. Aliponiona akashtuka, pia akashangaa ule mfuko nilioubeba. Mimi sikumjali Sana nikaingia upande wa pili wa bafu, Kwa waliosoma Matema Beach watakubaliana na Mimi kuwa Bafu la chini lilikuwa kubwa mno.

Nikatoka tena, nikaenda kuchukua Redio ili nimkere Yule jamaa aondoke nifanye shughuli zangu Kwa Uhuru😛😛😛 nikarudi nikiwa na Redio, nikaiwasha. Nikaweka mziki mkubwa.
Hila yangu ikafanikiwa, akaondoka.

Nikatoka zile nguo nikaziloweka na kuzisuuza pamoja na Yale mashuka na blanket Kwa Sabuni.
Sikutaka kuyafua nilikuwa nafanya hima ili nisikutwe na mtu mwingine. Nikamwaga maji, nikasuuza mara tatu mpaka harufu ya Kojo ilipotoka. Kisha nikaziacha nimeziloweka.

Muda wote nafanya hayo nilikuwa namuomba Mungu nisiaibike Walahi😉😉😉😂
Yaani ndio Kwanza nimeingia hata miezi miwili sina naangusha Kojo, nitaishije Mimi na ninavyopenda kutania watu🤣🤣🤣.

Nikafanikiwa, nikarudi Bwenini, sasa Ile Cube/Room yote ilikuwa na harufu ya miikojo licha ya Kupunguza manguo yenye mikojo.
Nikatandika shuka jingine nikafunguq dirisha hewa iingie japo kulikuwa na baridi Sana lakini Bora baridi kuliko Fedheha 😊😊😊
Nikatoka perfume nikapuliza kitandani kisha nakupuliza hewani😂😂 baada ya Nusu saa, Wanafunzi wa kiislam wakaanza kuamka kama unavyojua. Hata hivyo hawakuwa na athari.
Taikon miguu juu ninatathmini tukio zima namna lilivyoenda.

Wenzangu kwenye Ile room walikuwa wakikoroma mno na hiyo ndiyo nafuu yangu.
Awali mikoromo Yao ilikuwa kero kubwa kwangu siku za nyuma, Ila Kwa siku Ile ilinipa daraja kubwa, niliiona Kama mziki mzuri wa USHINDI🤣🤣🤣 kwani nilikuwa najua Kwa kukoroma Kule hakuna mwenye afadhali, wote walikuwa kwenye usingizi mzito ambao hata ningeamua kuwahamisha kitanda ningeweza.

Kulikucha!

Nikiwa wakwanza kuondoka eneo la tukio kwenda darasani😀😀😀 kuepusha hatari yoyote ya ishu kubumbuluka.
Wiki Ile sikushinda Room yangu tofauti na siku za nyuma ambapo room yangu ndio ilikuwa kijiwe kikuu cha Stori na Mimi ndiye Host😎😎
Nilikuwa nakuja Kwa kuchelewa mida ya saa nne tena kuja kulala tuu😀😀

Lengo lilikuwa ni kuyapa mazingira ya kitanda changu muda wa ku-recover yarudie Hali ya awali, harufu iondoke kabisa

Nilifanikiwa, na hakuna aliyewahi kunshtukia.

Nilimshukuru Mungu Sana.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Je wewe ulifanyaje siku uliyoangusha Kojo?
Tiririka chini.

Taikon wa Fasihi.
Mshusha Kojo
Kwa sasa, Mikumi.
0693322309
Aisee hakuna kitu kimenusumbua kama hicho nillikuwa napigwa bakora na bro acha kabisa.
Ila nakumbuka darasa la tano Mother alimuambia bro aache kunichapa kwa sababu sio kosa langu hakuna anayependa kukojoa ila inatokea bahati mbaya.

Mother kuna ushauri alinipa ambao pia niliwasaidia wengi wakaacha kukojoa
Ngoja niwape hapa ili msiwachape watoto wenu ila muwashauri kama alivyonishauri mimi Mother wangu na kunisaidia kabisa kuacha kukojoa nikiwa darasa la tano.

Aliniambia ya kwamba nihakikishe kuanzia asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ninywe maji mengi ya kutosha.
Itapofika kuanzia saa moja usiku nisiguse maji wala kimiminika chochote
Nifanye hivyo ndani ya mwezi then niendelee na utaratibu wangu wa zamani.
Nilifanya hivyo ndani ya mwezi kama alivyonishauri bi mkubwa toka siku hiyo naanza huo utaratibu sikuwahi kukojoa tena kitandani kitu ambacho nilijifunza kukojoa ni saikoloji hata zile ndototo pia ni saikoloji pia.

Ndio maana mimi nilifuata ule utaratibu wa mother ndani ya mwezi means ili kuujengea ubungo mazoea na hata baada ya mwezi kuisha nilivyoanza kunywa maji usiku pia sikuwahi kukojoa tena coz tayali nilishaweka mazoea kwenye akili yangu.
 
Aisee hakuna kitu kimenusumbua kama hicho nillikuwa napigwa bakora na bro acha kabisa.
Ila nakumbuka darasa la tano Mother alimuambia bro aache kunichapa kwa sababu sio kosa langu hakuna anayependa kukojoa ila inatokea bahati mbaya.

Mother kuna ushauri alinipa ambao pia niliwasaidia wengi wakaacha kukojoa
Ngoja niwape hapa ili msiwachape watoto wenu ila muwashauri kama alivyonishauri mimi Mother wangu na kunisaidia kabisa kuacha kukojoa nikiwa darasa la tano.

Aliniambia ya kwamba nihakikishe kuanzia asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ninywe maji mengi ya kutosha.
Itapofika kuanzia saa moja usiku nisiguse maji wala kimiminika chochote
Nifanye hivyo ndani ya mwezi then niendelee na utaratibu wangu wa zamani.
Nilifanya hivyo ndani ya mwezi kama alivyonishauri bi mkubwa toka siku hiyo naanza huo utaratibu sikuwahi kukojoa tena kitandani kitu ambacho nilijifunza kukojoa ni saikoloji hata zile ndototo pia ni saikoloji pia.

Ndio maana mimi nilifuata ule utaratibu wa mother ndani ya mwezi means ili kuujengea ubungo mazoea na hata baada ya mwezi kuisha nilivyoanza kunywa maji usiku pia sikuwahi kukojoa tena coz tayali nilishaweka mazoea kwenye akili yangu.
Nimawatoto wanakojoa mno, ngoja nijaribu kuwalea kwa hii mbinu nione..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom