Nimekukubali jembe kula 5 hukohuko uliko.Last week nilikuwa Dodoma kwa wiki nzima. Nikahamasishwa na mshikaji wangu nifikie kwake, anafamilia yake hapo Dom.
Asubui najidamka kwenye mizunguko yangu nakuta wenyeji wangu Kama Kuna kitu wanadiscuss kwa mashaka mashaka hivi. Kumbe shemeji yangu wakati anataka kufanya usafi nje akakuta mlangoni kuna mayai sita na Nazi ambayo haijavunjwa na kikaratasi kilichoandikwa kiarabu. Wanaogopa hata kuvishika. Kuuliza vipi? Naambiwa tangu jana yake wanaona mauza mauza tu kwani walikuta madirishani sijui kumeandikwa maandishi gani. Wakamwita mchungaji gani sjui akayafuta na kupiga maombi ya nguvu. Ila chaajabu asubui wamekuta mayai.
Wakataka wapige simu kwa huyo mchungaji, nikamwambia waache kwanza. Nikayacheki Yale mayai nikaona ni mazima tena ya kienyeji. Nikawaambia tu sijala mayai ya kienyeji siku nyingi naona haya yatanifaa. Hawakunielewa kabisa.
Nikamwomba Shem ayakaange ile wanaita Spanish ila asiweke chumvi nyingi. Akaruka futi Mia kukataa. Nikasema isiwe shida. Jiko? Hili hapa. Mzee nikaingia studio nikatoa kitu cha Spanish kinanukia hatari. Jamani karibuni. Wanaogopa. Mshikaji wangu ananiambia oya umekula ushirikina, uko kwenye mizunguko ukiona mawengewenge nipigie ili tumwite mchungaji. Nikawa nawacheka kwa zereeeu. Nikayagonga yote. Nikasepa. Kila mda jamaa yangu ananicall nadhani alikuwa anatrace naendeleaje. Siku ikapita.
Asubuhi Tena mauza uza. Hamadi njiwa wawili wapo mlangoni wamefungwa vitambaa vyekundu miguuni. Nikaitwa kushuhudia na kuulizwa Leo tunafanyaje. Jamani si njiwa Hawa? Ndio. Naombeni kisu kikali. Wananitolea macho. Kama kawaida nikazama kicheni nokatoka na kisu. Nikawachinja na kuwapasua vizuri. Nikauliza Kama Kuna oven, nikaambiwa ipo. Nikaingia Tena studio kuproduce kitu cha nguvu. Nikawabanika fresh. Wananukia hatari. Ugomvi ukawa kwa watoto wanataka nyama wazazi wao wanawakataza. Nikashauri watoto watengenezewe kuku wa kwenye friji ili kuleta amani. Siku ikapita.
Asubuhi nikaamshwa Tena na shemeji kwa makelele. Nikatabasamu nikajua Leo Kama sio kuku wa kienyeji basi ni mbuzi au hata kitimoto. Hamadi. Hamna kitu. Nikasonya. Shemu anafuraha kwamba nimewasaidia kuwakomesha hao washirikina.
Imepita wiki Sasa. Mpaka naandika hapa hakuna mauza uza yaliyowapata.
My Take: Hao wanaoweka is either wanataka tu kucheza na akili yako uishi kwa hofu na kukutoa kwenye focus yako ya maisha au nao wametapeliwa na waganga njaa mjini na hivo kufanywa wa wajinga ndiwo waliwawo.
Ushauri: Ukikuta Nazi imevunjwa kaungie wali au mboga, mayai wewe kaanga chemsha, njiwa sijui kuku chinja. Ilimradi tu imani yako kwa Mungu isiwe haba.
Umetisha mkuuNimekukubali jembe kula 5 hukohuko uliko.
Hawa wahuni sio wa kuwaogopa mafala tu.
Mara nyingi wanasema wahindi upenda kuwapa wafanya kazi wao nazi za kishirikina kuwapumbaza na ukikataa hawakupendi. Sijui km huwa kunaLast week nilikuwa Dodoma kwa wiki nzima. Nikahamasishwa na mshikaji wangu nifikie kwake, anafamilia yake hapo Dom.