Nimekosa msichana kisa ndevu

Nimekosa msichana kisa ndevu

Ulikua unaepushwa janga labda. Fuga tu ndevu. Marafiki zangu wa kike wengi hawatapendi madevu
 
Ujitahid bas hata kuzipunguza maana watakukumbia sasa
Kuna siku nilikwenda saloon kuzipunguza urefu kidogo sasa jamaa akazikomba, aliniudhi sana na sikumlipa kabisa......tangu siku hiyo naona bora zibaki hivi hivi
 
Hahaha,fisi kakosa zoga....!,anaumiiia,bro karibu kwenye team Ndevu ila ziwe zinamuonekano wakigentleman sio zile kama mwarabu wa wapi cjui,na we ni fisi kama fisi wengine sasa usiwaze,wenzio akakikosekana swala mmoja we go to the next one!,so be On to the Next one!,
 
Kunyoanyoa ndevu ni uboya unapunguza ugentlemen ndio maana vijana weng mchelemchele sana
 
Habari ndugu zangu

Mimi ni mkazi wa Dar ila wiki hii nilipata fursa ya kikazi kwenda Jijini Tanga, hakika nilifurahi haswa nikizingatia kuwa sijakwenda huko tangu enzi ya Kalembo.

Nilifika salama katika jiji hilo tulivu na nikakutana na stori za mwembe 'uliogeuka' Nyerere pamoja na story mbali mbali za matukio mengine, nikafanya kilichonipeleka na nilipomaliza nikaona si vibaya nikatafuta mwenzangu katika mji huu wa stara na mahabati.

Usiku nilipokuwa katika ukumbi mmoja nikipata muziki mororo huku nikiburudika na chaza, pweza nk, mara ghafla macho yangu yakagongana na ya binti mmoja matata sana.

Haikuchukua mda kumfuata na kumueleza matatizo yangu ya moyoni na alionyesha kama kunielewa hivi na kuwa karibu na mimi japo alikuwa akiniangalia usoni sana, tukaafikiana kutoka na kwenda sehemu nyingine na tulipofika nje nikamfungulia mlango wa gari (Vx la ofisi ambalo ni matata sana) ili tuende tulipopanga ila aligoma ghafla.

Akaniambia basi ameghairi na nisimfuate tena na huyo akatokomea!!! Pembeni kuna kijana mmoja ambae alikuwa akiona yote hayo, nikamfuata kama mwanaume mwenzangu tujadili, akaniambia broo umekosea hayo madevu mwanangu, hapa kuna watu walichinjwa sasa wasichana wana hofu sana na watu wa aina yako tena bora mngekwenda na miguu kuliko unaleta mambo ya vioo vyeusi tena.

Nikavuta picha na nikakumbuka ni kweli yule dada alikuwa ananiangalia sana usoni na kweli nina madevu kama urembo toka kubalehe na nimeshazoea hivyo.

Ndugu zangu tumefikia huko kweli? Yaani tubaguane kisa ndevu!!!

Imeniuma sana
hajakubagua bali amepata hofu kutokana na matukio yaliyotokea.....elewa hali halisi tu pole kwakukosa mtoto mzuri katoka mdomoi mwako
 
Kifo mkuu kinaogopwa sana. Mtu akiona viashiria hata kama siyo vya ukweli lazima hofu imjae.
Nyoa...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom