Wanaume wananitoroka kwa sababu ya ndevu

lwambof07

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
4,593
5,203
Mara nyingi ,Faith Macharia hukutana na wakati mgumu anapokutana na watu njiani, wengi hugeuka kumtazama tena.

Hii hutokea kwa sababu ya jambo ambalo hawezi kuligeuza, kwamba yeye ni mwanamke ila na ana ndevu kama mwanaume.

Ni jambo ambalo yeye mwenyewe lilimpa kiwewe mwanzoni na ilichukua muda kulikubali.

Jinsi mabadiliko yalipoanza
Mnamo mwaka 2004, alipojitazama kwenye kioo na kuziona ndevu zilivyoota kama za mwanaume kuzunguka kidevu chake, alishangaa na kujiuliza, "Je, ninakuwa mwanaume ?'.

Alikuwa na umri wa miaka 24 wakati huo na ni umri ambao alitazamia angelikuwa binti 'aliyeiva' na mwenye urembo kama tausi.

Katika umri huo wanawake wengi hutazamia mwanzo wa mkondo mpya wa maisha baada ya mabadiliko ambayo hutokana na mawimbi ya kubalehe.

Kwa hivyo matarajio ya mwanamke huyu yalikuwa mengi, alitegemea kuwa angekuwa wa kupendeza na pengine kutongozwa kwa uzuri wake.

Ujasiri aliokuwa nao wa kuwa mwanamke mrembo ulishuka maumbile ya uso wake yalipoanza kubadilika.

Mwanzoni, aliutafuta wembe na kunyoa ndevu katika kidevu, na kupumua kwa kutosheka kuwa hatimaye ameondoa kile kilichokuwa kinampa wasiwasi.

Wiki moja baadaye, Faith aligundua kidevu chake kilikuwa kimeota ndevu zaidi, hata kwa kasi zaidi kuliko awali.

Kila alipojaribu kuzinyoa kwa wembe ndivyo zilivyomea zaidi .

Mwanamke huyu alifanya kila kitu kuzificha ndevu hizo. "Nilizinyoa kila baada ya siku chache kwa bidii ya mchwa - kamwe niliogopa watu wafahamu siri yangu ," anasema Faith

Mwanadada huyu anasema kuwa ilifika wakati akachoka kunyoa ndevu kila siku .

Na hapo ndipo watu walipoanza kugundua kwamba alikuwa na siri aliyoificha. Mtu wa kwanza kugundua alikuwa shangazi yake.

"Ni hali moja kukubali una kasoro ya maumbile lakini inazua uoga mno unapoanza kufikiria kuwa watu wengine wataanza kufahamu siri hii," Faith anasema .

Mwanadada huyu anasema kuwa hakujua jinsi ya kukabiliana na hisia za watu kuhusu ndevu zake.

Wakati mmoja akiwa kwenye pilika pilika za kawaida anakumbuka akiwa akitafuta huduma kwenye benki mmoja.

Aligundua kuwa wanaume wawili waliokuwa kando yake walikuwa wanamsema, huku wakinyoosha mikono yao yakimwelekea huku wakimkejeli.

"Nilifahamu wananicheka lakini sasa ningefanyaje? Maisha ya wanawake wenye ndevu yana kejeli zinazoandamana na unyanyapaa" Faith anasema

Mwanamke huyu anasema kuwa kabla ya kukubali hali yake, aliona aibu juu ya ndevu zake, ila ilibidi apige moyo konde na kuendeleza maisha yake.

Visa vingi vilivyoandamana na unyanyapaa vimemzonga, hadi karibu akate tamaa ya kutangamana na watu na kuhisi kana kwamba hana pumzi za kutosha kusimama mbele ya watu wengi kwa kukosa ujasiri.

Wakati mmoja aliamua kwenda hospitalini, kutafuta suluhu.

Hospitali ya kwanza aliyoizuru daktari alimtuma kwa wataalam wengine katika hospitali nyingine kupata huduma spesheli kuhusiana na hali yake .

"Nilipopimwa, matokeo yalikuwa kwamba nimekosa usawa katika homoni zangu. Nilielekezwa kwa mtaalamu wa ngozi ambaye alinipa ushauri kuhusu mafuta ya kupaka kusaidia kuondoa mandevu yanapomea, pia alinieleza kuwa nitanyoa ndevu hadi mwisho wa maisha yangu," Faith anakumbuka

Ushauri mwingine aliopewa ni kufanyiwa matibabu spesheli ya homoni, ila ni matibabu ghali mno yaliyomshinda Faith.

Aliamua kurudi nyumbani na kuwa akizinyoa ndevu zake kama alivyozoea.

Kero la kutafuta mpenzi
Ndevu zimeekuwa kikwazo katika maisha yake ya huba. Wanaume wengi wamekuwa wakiogopa ndevu hizo, na kila wanapogundua hilo humtoroka.

Kwanza alikutana na mwanamume ambaye walikuwa pamoja kwa miaka minne lakini alitoroka ghafla asijulikane alikokwenda

"Nadhani alitamaushwa na ndevu, nafikiria kuwa ndani yake alikuwa anapigana na ile hali ya kujiuliza kama angemuoa mwanamke mwenye ndevu mwishowe akaona kheri anitoroke. Alibadilisha hadi nambari za simu zisimpate tena," anakumbuka Faith

Mwanamke huyu anasema umekuwa kama mtindo kwa wanaume kumkimbia.

Baadaye, alimpata mwanamume mwengine ambaye wakati wa kwanza kukutana alihakikisha alikuwa amenyoa ndevu vizuri.

ila shida ilitokea walipokuwa wanakumbatiana kwa salamu, mabubutu ya za nywele za kidevu yalimchoma mwenzake. Hilo lilimfanya yule mwanamume kutupa jicho la pili katika kidevu chake na ndipo akagundua shida yake.

Huo ulikuwa mkutano wa kwanza na wa mwisho kwao, mwenzake alikata mawasiliano.

Kujaliwa mtoto
Faith alijifungua mtoto wa kiume 2011, ambaye pia amegundua mama yake ana ndevu.

Anasema mwanawe amekuwa pia akikabiliwa na unyanyapaa

"'Mama, kwani una ndevu kama mwanamume, aliniuliza hivi maajuzi'. Nilimjibu naam baadhi ya wanawake wanaota ndevu kama wanaume , lakini sio kusema kuwa mimi sio mwanamke," Asema Faith

Mwaka wa 2018 , Faith aliunda chama ni cha kuwaleta wanawake wenye ndevu nchini Kenya pamoja (BWO).

Lengo ni kuhakikisha kuwa wanawake kama yeye wana jukwaa ambalo wanaweza kulitumia kuhimizana na kushuariana.

Matumaini yake ni kuwa wanawake kama yeye watapata nafasi ya kutafuta suluhu ya kuishi na changamoto za ndevu.

Mmoja wao ni Bi Elizabeth ambaye amejizatiti na kujipa moyo baada ya kujiunga na kikundi hiki.

Mwanamke huyu pia analaumu kidevu chake kwa kuporomoka kwa ndoa yake.

"Ilifika pahali kwenye ndoa kila tulipokosana na aliyekuwa mume wangu alifoka na kuniuliza, je kwa kuwa una ndevu unataka kuwa mwanamume mwenzangu?" anasema.

"Aliamini kuwa ujasiri wangu ulikuwa unaletwa na ndevu,ilinivunja moyo sana."

Nini huchangia wanawake kumea ndevu?

Katika baadhi ya matukio, ukuaji wa ndevu za kike ni matokeo ya ukosefu wa usawa wa homoni (kwa kawaida androgen excess), au shida adimu ya maumbile inayojulikana kama hypertrichosis.

Katika baadhi ya matukio uwezo wa mwanamke kuota ndevu unaweza kutokana sababu za urithi.View attachment 2089072
IMG_20220120_101125.jpg
IMG_20220120_101115.jpg
IMG_20220120_101104.jpg
IMG_20220120_101052.jpg
 
Katika baadhi ya matukio uwezo wa mwanamke kuota ndevu unaweza kutokana sababu za urithi.View attachment 2089072View attachment 2089073View attachment 2089074View attachment 2089076View attachment 2089078
Trako unalo?
 
Back
Top Bottom