Nimekosa msichana kisa ndevu

Nimekosa msichana kisa ndevu

Mkuu mambo haya yalinifikirisha sana na yote hii ni wale waliochinja wenzao ndio waliosababisha, yaani yule mtoto mpaka leo hii roho inaniuma sana nikikumbuka lile shepu
ha ha ha

mkuu, hukychukua hata namba ya simu, huenda akakupa next chance ujitetee aiseee.
 
ha ha ha

mkuu, hukychukua hata namba ya simu, huenda akakupa next chance ujitetee aiseee.
Kijinamba ninacho ila hakifai kitu maana sipokelewi na hata nikitumia line nyingine ni bila bila, sasa kwa hasira haya madevu nitayaacha yaongezeke zaidi
 
Hahahaha Mkuu sio kukandia ila kwa hali hiyo ni hatariiii
Madevu namna hii nikiingia sehemu yeyote naonekana hili jitu sio la mchezo.....zina faida yake mkuu usiangalie upande mmoja
 
Habari ndugu zangu

Mimi ni mkazi wa Dar ila wiki hii nilipata fursa ya kikazi kwenda Jijini Tanga, hakika nilifurahi haswa nikizingatia kuwa sijakwenda huko tangu enzi ya Kalembo.

Nilifika salama katika jiji hilo tulivu na nikakutana na stori za mwembe 'uliogeuka' Nyerere pamoja na story mbali mbali za matukio mengine, nikafanya kilichonipeleka na nilipomaliza nikaona si vibaya nikatafuta mwenzangu katika mji huu wa stara na mahabati.

Usiku nilipokuwa katika ukumbi mmoja nikipata muziki mororo huku nikiburudika na chaza, pweza nk, mara ghafla macho yangu yakagongana na ya binti mmoja matata sana.

Haikuchukua mda kumfuata na kumueleza matatizo yangu ya moyoni na alionyesha kama kunielewa hivi na kuwa karibu na mimi japo alikuwa akiniangalia usoni sana, tukaafikiana kutoka na kwenda sehemu nyingine na tulipofika nje nikamfungulia mlango wa gari (Vx la ofisi ambalo ni matata sana) ili tuende tulipopanga ila aligoma ghafla.

Akaniambia basi ameghairi na nisimfuate tena na huyo akatokomea!!! Pembeni kuna kijana mmoja ambae alikuwa akiona yote hayo, nikamfuata kama mwanaume mwenzangu tujadili, akaniambia broo umekosea hayo madevu mwanangu, hapa kuna watu walichinjwa sasa wasichana wana hofu sana na watu wa aina yako tena bora mngekwenda na miguu kuliko unaleta mambo ya vioo vyeusi tena.

Nikavuta picha na nikakumbuka ni kweli yule dada alikuwa ananiangalia sana usoni na kweli nina madevu kama urembo toka kubalehe na nimeshazoea hivyo.

Ndugu zangu tumefikia huko kweli? Yaani tubaguane kisa ndevu!!!

Imeniuma sana
kweli nimezeeka hivi usawa huu bado huwa watu mnaviziaga wanawake kwenye giza khaaaaaaaaaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom