Nimekosa msichana kisa ndevu

Nimekosa msichana kisa ndevu

hajakubagua bali amepata hofu kutokana na matukio yaliyotokea.....elewa hali halisi tu pole kwakukosa mtoto mzuri katoka mdomoi mwako
Hakika mkuu umeongea maneno ya ki utu uzima sana, hata mimi ndio nilichokiona maana tulishakubaliana vema kabisa
 
Habari ndugu zangu,

Mimi ni mkazi wa Dar ila wiki hii nilipata fursa ya kikazi kwenda Jijini Tanga, hakika nilifurahi haswa nikizingatia kuwa sijakwenda huko tangu enzi ya Kalembo.

Nilifika salama katika jiji hilo tulivu na nikakutana na stori za mwembe 'uliogeuka' Nyerere pamoja na story mbali mbali za matukio mengine, nikafanya kilichonipeleka na nilipomaliza nikaona si vibaya nikatafuta mwenzangu katika mji huu wa stara na mahabati.

Usiku nilipokuwa katika ukumbi mmoja nikipata muziki mororo huku nikiburudika na chaza, pweza nk, mara ghafla macho yangu yakagongana na ya binti mmoja matata sana.

Haikuchukua mda kumfuata na kumueleza matatizo yangu ya moyoni na alionyesha kama kunielewa hivi na kuwa karibu na mimi japo alikuwa akiniangalia usoni sana, tukaafikiana kutoka na kwenda sehemu nyingine na tulipofika nje nikamfungulia mlango wa gari (Vx la ofisi ambalo ni matata sana) ili tuende tulipopanga ila aligoma ghafla.

Akaniambia basi ameghairi na nisimfuate tena na huyo akatokomea!Pembeni kuna kijana mmoja ambae alikuwa akiona yote hayo, nikamfuata kama mwanaume mwenzangu tujadili, akaniambia broo umekosea hayo madevu mwanangu, hapa kuna watu walichinjwa sasa wasichana wana hofu sana na watu wa aina yako tena bora mngekwenda na miguu kuliko unaleta mambo ya vioo vyeusi tena.

Nikavuta picha na nikakumbuka ni kweli yule dada alikuwa ananiangalia sana usoni na kweli nina madevu kama urembo toka kubalehe na nimeshazoea hivyo.

Ndugu zangu tumefikia huko kweli? Yaani tubaguane kisa ndevu!

Imeniuma sana
Pole sana mkuu!! Ulimwambia kwenu ni Daslam mji wa lawama nini?? Nahisi tatizo sio ndevu mkuu huenda hapendi tu wanaume wa dar si unajua matatizo yenu
 
Kifo mkuu kinaogopwa sana. Mtu akiona viashiria hata kama siyo vya ukweli lazima hofu imjae.
Nyoa...
Hahah ni kweli maana hata nilipokuwa nikipishana na maafwande walikuwa wakiniangalia kwa jicho la husda
 
Pole sana mkuu!! Ulimwambia kwenu ni Daslam mji wa lawama nini?? Nahisi tatizo sio ndevu mkuu huenda hapendi tu wanaume wa dar si unajua matatizo yenu
unataka kuongeza tatizo juu ya tatizo wewe
 
Hujui Mungu alikuepushia nini hapo! wewe mshukuru Mungu kuwa yote ni Heri!!
 
Huyo anaona ndevu tatizo wakati wenzake pia wanazo
e6011d58c0effdf902e3e2f87c09752f.jpg
01e2052be6ac1121ef922df14f516543.jpg
4ee2dd18ffe4f3708ca528e7e6d8f145.jpg
53c48629b5893048df043e590b756bc7.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom