Nimekoma jamani! Hiki chumba ni balaa tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimekoma jamani! Hiki chumba ni balaa tupu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Sunshow, Feb 20, 2012.

 1. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nimekuja zangu kikazi katika mji huu jina kapuni. Baada ya kufika nikapokelewa na rafiki yangu. Tukiwa standi, nilimwambia anisaidie kutafuta hotel nzuri ya kulala na yeye akajibu nisiwe na shaka nitaenda kulala nyumbani kwake. Basi tukaenda hadi nyumbani kwake na baada ya mazungumzo akanipeleka kwenye chumba nitakacholala.

  Tukatakiana usiku mwema na yeye kwenda kulala chumbani kwake. Mimi baada tu ya kuzima taa ndipo balaa lilipoanza. Chumba kimejaa panya sijawahi ona! Panya vurugu mtindo mmoja hadi wanataka kunitafuna miguu.

  Zaidi ya hapo, chumba kimejaa mbu japo kuna neti lakini kelele za mbu huwezi kulala hata uwe umelewa vipi. Sasa najiuliza hivi huyu rafiki yangu amenifanyia makusudi au ni ukarimu tu maana hapa natamani niende nikalale ndani ya gari.
   
 2. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Hapana hajakufanyia makusudi kwa sababu kwake hii hali keshaizoea. Unapoyazoea mazingira yako unaona ni kawaida ila kwa mwingine ni tofauti. Huna jinsi mkuu vumilia mpaka asubuhi hao panya nasikia wakikung'ata unakuwa bonge la tajiri
   
 3. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Yaani asubuhi naiona kama wiki. Kusema kweli najuta na nimekoma.
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Ndo uanaume huo.
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tafuta konyagi au chochote ulale . Kwani hao mmbu watamaliza damu yote uliyonayo ? Wao watakula wapi ? Au haujui tunategemeana ? Vunga na ulale .
   
 6. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kuwasha taa na kulala lakini hawa panya ni wa ajabu kweli kweli wanafukuzana hivi hivi nikiwa nawaona.
   
 7. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Natafuta neno la kumwambia asubuhi hadi nakosa. Je nimshukuru kwa ukarimu wake au nimchane live?
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu usilipe wema wake kwa kumdhalilisha, huo ndio uwezo wake, kama ulitaka bure basi bure umeifaa, ila kama ulitaka nafuu, basi nafuu na nafuu yake pia

  kama hujapenda ondoka kalipe hoteli, unachofanya si kizuri, kudhalilisha aliyekupa nafasi yake kwa uwezo wake, kama angewez angeishi masaki na wewe usingeleta hii fookin post hapa

  KWELI TENDA WEMA WENDE ZAKO
   
 9. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu wala sijamdhalilisha na bado nasema huo ndiyo uwezo wake lakini kumbuka hapo awali nilimwambia anitafutie hotel nzuri. Neno hotel nzuri linatosha yeye kujua ni aina gani ya chumba nilikimaanisha. Na isitoshe alikuwa na nafasi ya kunionyesha chumba mapema kabisa na kuniuliza kama kingenifaa kuliko kusubiri mpaka muda wa kulala.
   
 10. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Mhh hii inanana kama rafiki yangu alipangisha nyumba jijini dar akajikuta anaalala na panya na mende usiku wengi blaaa.akamwambia mama mwenye nyumba mzee akawa anacheka basi jamaa akajua wale ni wadudud wa mzee anawafuha.akamwambia anataka kuhama akamwabia nenda tu hela hampi manake mkatanba haujaishas.soo yawezekana hao wadudu ni Viumbe vya watu
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nzuri inategemea uwezo wa mtu, kumbuka "maji ya kifuu ni bahari ya chungu"
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu naturally tuna culture moja, we dont observe trends

  ikitokea umehamia nyumba ikaanza kuwa na mende mara nyingi huwa hatuoni hadi wanapoanza kupita sebuleni wakati mnakula au kusali, na wakati mwingine pia hiyo hamuoni mwisho wanahamia panya, mwisho inakua a house of rodents, ndivyo hali ilivyo

  cha maana ni kutoa ushauri wa usafi au hata kusema madhara in a friendly way

  wenye nyumba wana tabia ya kudharau hoja za wapangaji, lakini ni jukumu la mpangaji kuishi sehemu safi
   
 13. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu rafiki yangu siyo kusema ni mtu wa dhiki kivile sema tu kwamba yeye ni mtu wa kupenda kubana saana mtaani wanaita anapenda ku make. Yuko radhi alale kwenye gari wakati night allowance yake ni ya kutosha kumfanya alale sehemu nzuri.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  now you know, he thought you would save at any cost... sorry charlie
   
 15. k

  kajunju JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hayo ndo maisha yake.yeye asikii panya si ana mke! Kama umeenda kikaz,ndio tatizo la kupewa vi-per diem kiduchu.mtu naenda kujibanza kwa mtu ili apate japo pesa.wengine kama umeenda kikaz unalewea pesa yote then unaenda jiegesha kwa mtu.asubuhi hama nenda guest. Chumba kina ceiling board?kama hakina,huku mmekuja mmejitwika kinywaji..anaanza mchezo na shemeji wewe hoiii
   
 16. N

  Njangula Senior Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole rafiki lakini jamaa ana ideology yake kukufanya usave money si unajua ukikwetelism2011 maisha magumu hao panya ni ziada..............napita tu sasa navuta blanketi kurudia usingizi mnono na ndoto tamu za maisha mazuri. ANGALIZO: Jamaa yako hayumo JF? Isije ikawa sirte sasa hivi.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,600
  Likes Received: 82,161
  Trophy Points: 280
  Bure ghali Mkuu...Pole sana...Sasa utunge story ya kumridhisha mwenyeji wako kwanini unataka kuhamia hotel....au kama huoni noma mwambie tu kwamba panya na mbu wa humu ndani siwawezi kabisa...sikulala usiku kucha.
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,815
  Trophy Points: 280
  Kwa mfano kama huyo rafiki yako aliyekukirimu ni member humu na anasoma huu udhalilishaji unaomfanyia hapa?

  Kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo.

  **** na Ovyooo!
   
 19. ambili

  ambili JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ila wa tz inabidi tubadilike huwezi kuacha nyumba yako ikawa ni makazi ya panya wakati wanadhibitika, kwani panya ni hatari sana kwa afya ya familia yako kama kueneza vimelea vya taun, kuharibu mazao, kukata nyaya za nyumba, nguo n.k. Huyo anahitaji kuelimishwa madhara ya hawa viumbe asiwachukuliea poa kabisa .Narudia huwezi ukafanya matatizo ndio sehemu ya maisha yako, tutafute solutions jamani , tusimbeze mtoa mada.
   
 20. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sawa ana nia njema lakini ndiyo kuniweka sehemu ambayo nitashindwa kufanya kazi kwa ufanisi siku inayofuata? Hapa najisikia kichwa kuzunguka zunguka sababu ya kushindwa kulala na tayari keisha niharibia siku. Inabidi nitafute hotel nikalale walau hadi saa tano.
   
Loading...