Mount Kibo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 1,956
- 553
yani huyo hakupendi hata chembe
akupendae haangalii pesa kama kigezo!!
huko ni kupenda usipopendwa!!utaumia bureee!!
Kijana usilalame ,,,, fanya kazi tafuta pesa ukipata kamtongeze ufaidi mahabati.
Mapenzi kweli kizungumkuti,yanayonikuta yanautesa sana moyo wangu.
KUna msichana ambaye ninampenda sana toka siku nyingi na yeye aanalijua hilo,ila kila nikimueleza juu ya hisia zangu uu yake yeye huishia kusema NAKUPENDA ILA HATUWEZI KUWA PAMOJA KWAKUWA HAUNA KAZI,HUNA PESA.
Hiki kitu kinaniumiza sana kwani kukosa kwangu kazi na kukosa pesa kunanifanya nimkose mtu ninayempenda kwa dhati,pia najiuliza hivi siku hizi ndio mapenzi hayawezakani tena mtu aspokuwa na pesa/kazi?ndugu mwana-jamvi,fikiria kama wewe ndio ungekuwa umepata na situation kama hii inayonikumba mimi ungefanyaje?(kumbuka hii ni very true story)
ndo pakutafuta kazi upate hela ili umnase umtakaye.
kimsingi mwanaume asokuwa na kazi kuwa nae kwenye mahusiano ni mzigo wa gunia la misumari. utamtesa sana huyo dada kwasababu utamnyima raha kila muda utanung'unika tuuuuuuuu kisa yy anafanya kazi ww ni kama kochi tu humo ndani
Hivi mwanamme haswa anakosa kazi ya kufanya? Unanshangaza!
Hebu panga hata ndizi nje ya unapoishi utaona kama si kazi yenye kukuingizia pesa.
Inasikitisha sana kwa mwanamme kutangaza kuwa huna kazi. Huyo dada aliekupiga chini, kishaona hufai, nampa heko sana.
Mwanamme labda useme hujafanikiwa kupata kazi uitakayo na unajishughulisha kwa kazi nyingine yoyote na huku unaendelea kuitafuta uipendayo. Lakini hilo la mwanamme kutokuwa na kazi ya kufanya linasikitisha sana.
Janadume linalojisifia eti halina kazi, lina faida gani hilo?
mwanaume majukumu babu!huyo hakupendi wewe... yeye anapenda utakachokua nacho!
cha muhimu muweke pending halafu tafuta kazi ukishapata tu ndo mfuate tena ila sio kwa kukaa bali kupita tu.
ili roho yako iridhike.
dont wory,,,1 day yes.............
Ubaya ni kwamba hajatangaza ndoa ila anataka kugegeda tu. soma thread Mkuu.
kwa maana hiyo wanaume wote wasiokua na pesa wala kazi hawana wanawake?
ni adhabu kupenda usipopendwa. Hivi kwanin umng'ang'anie? Mwanamke ni yeye peke yake? Wako wanaokesha kuomba kupata wakumpenda. Usismame kwenye mlango mmoja uliofungwa, ilihali ipo mingne 100 wazi.