Nimekataliwa kisa........!

Nimekataliwa kisa........!

Mr Yes

Senior Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
153
Reaction score
29
Mapenzi kweli kizungumkuti,yanayonikuta yanautesa sana moyo wangu.
KUna msichana ambaye ninampenda sana toka siku nyingi na yeye aanalijua hilo,ila kila nikimueleza juu ya hisia zangu uu yake yeye huishia kusema NAKUPENDA ILA HATUWEZI KUWA PAMOJA KWAKUWA HAUNA KAZI,HUNA PESA.

Hiki kitu kinaniumiza sana kwani kukosa kwangu kazi na kukosa pesa kunanifanya nimkose mtu ninayempenda kwa dhati,pia najiuliza hivi siku hizi ndio mapenzi hayawezakani tena mtu aspokuwa na pesa/kazi?ndugu mwana-jamvi,fikiria kama wewe ndio ungekuwa umepata na situation kama hii inayonikumba mimi ungefanyaje?(kumbuka hii ni very true story)
 
ndo pakutafuta kazi upate hela ili umnase umtakaye.

kimsingi mwanaume asokuwa na kazi kuwa nae kwenye mahusiano ni mzigo wa gunia la misumari. utamtesa sana huyo dada kwasababu utamnyima raha kila muda utanung'unika tuuuuuuuu kisa yy anafanya kazi ww ni kama kochi tu humo ndani
 
siyo wako huyo ndo mana anatumia vigezo vya kazi na pesa kukutosa........ambaye ni wako hatakuletea hvyo vigezo.........
 
Akunyimae kunde anakupunguzia mashuzi. Achana nae utapata wako atakaekukubali. Maisha ni kupanda na kushuka, ndoa inataka kuvumiliana in the sense ya kuaccomodate each other. Tafuta hela umdolishie na sio kumnasa
 
Umenena vyema sister,mgekuwa kama kumi tu humu JF basi hata zile thread za sijui wote wanauza zisingekuwepo!Mahusiano mazuri na matamu ni yale ya kila mmoja kujitahidi kumfanyia mazuri mwenzie sio kutaka kufanyiwa mazuri na mwenzio!Kila mmoja atake na ajitahidi kila mara kumfurahisha mwenzie sio kutafuta furaha yake binafsi!.Big up sister,nitafute nikupe zawadi!
 
Last edited by a moderator:
Pole kijana sasa hivi hamna mapenzi kuna biashara na ndio maana mtu anaefika bei ndio anapata bidhaa.Wala usilalame maana kuna mwenzio nilikutana nae yeye amemsomesha chuo binti halafu binti kamuona kenge baada ya kumaliza .Ni jambo jema la kumshukuru mungu maana hujui kama huko mbeleni ingekuaje halafu ni wakati wa ww kutafuta pesa ukachukua bidhaa nzuri sokoni.
 
Dah!! hili sijui ni tusi?sijui ni bango?yaani limenichanganya kabisa.
 
Pole kijana sasa hivi hamna mapenzi kuna biashara na ndio maana mtu anaefika bei ndio anapata bidhaa.Wala usilalame maana kuna mwenzio nilikutana nae yeye amemsomesha chuo binti halafu binti kamuona kenge baada ya kumaliza .Ni jambo jema la kumshukuru mungu maana hujui kama huko mbeleni ingekuaje halafu ni wakati wa ww kutafuta pesa ukachukua bidhaa nzuri sokoni.

Duhh,yameishakuwa hivi kumbe!!
 
ndo pakutafuta kazi upate hela ili umnase umtakaye.

kimsingi mwanaume asokuwa na kazi kuwa nae kwenye mahusiano ni mzigo wa gunia la misumari. utamtesa sana huyo dada kwasababu utamnyima raha kila muda utanung'unika tuuuuuuuu kisa yy anafanya kazi ww ni kama kochi tu humo ndani
aaah Gfsonwin huna hata haya..asubuhi yote hii kumpa za mwezio kavu kavu za uso manake nini?Yaani umempa black and White..Ila kwa ukweli anachotakiwa kujua kukubaliwa na kukataliwa vyote vina chance sawa,akubaliane na chochote kinachijiri ktk hayo.ambao labda nao walimtaka yeye hakuwapenda hivyo linapokuwa lake naye alibebe pia.Zaidi ajue kuishi na mwenzio ni gharama zaidi kuliko kuwa single utashindwa kumhudumia matokeo atatunziwa na wengine.Cha kushukuru bi-dada kaamua kuwa mkweli...akunyimae mbaazi kakupunguzia mashuuz..
 
bwana eeee ukitaka kumkanya mtu mwambie ukweli mchungu!
 
Mapenzi kweli kizungumkuti,yanayonikuta yanautesa sana moyo wangu.
KUna msichana ambaye ninampenda sana toka siku nyingi na yeye aanalijua hilo,ila kila nikimueleza juu ya hisia zangu uu yake yeye huishia kusema NAKUPENDA ILA HATUWEZI KUWA PAMOJA KWAKUWA HAUNA KAZI,HUNA PESA.

Hiki kitu kinaniumiza sana kwani kukosa kwangu kazi na kukosa pesa kunanifanya nimkose mtu ninayempenda kwa dhati,pia najiuliza hivi siku hizi ndio mapenzi hayawezakani tena mtu aspokuwa na pesa/kazi?ndugu mwana-jamvi,fikiria kama wewe ndio ungekuwa umepata na situation kama hii inayonikumba mimi ungefanyaje?(kumbuka hii ni very true story)
huyo hakupendi wewe... yeye anapenda utakachokua nacho!
cha muhimu muweke pending halafu tafuta kazi ukishapata tu ndo mfuate tena ila sio kwa kukaa bali kupita tu.
ili roho yako iridhike.
 
Umenena vyema sister,mgekuwa kama kumi tu humu JF basi hata zile thread za sijui wote wanauza zisingekuwepo!Mahusiano mazuri na matamu ni yale ya kila mmoja kujitahidi kumfanyia mazuri mwenzie sio kutaka kufanyiwa mazuri na mwenzio!Kila mmoja atake na ajitahidi kila mara kumfurahisha mwenzie sio kutafuta furaha yake binafsi!.Big up sister,nitafute nikupe zawadi!

asante.........hyo zawadi ngoja nitafute helmeti kwanza....nisije nkamwagiwa tindikali.......
 
Last edited by a moderator:
asante.........hyo zawadi ngoja nitafute helmeti kwanza....nisije nkamwagiwa tindikali.......

Hahahahaaaaa,wala husijali,mi mwenyewe nitakuja na helmet!Tena na buleti proof husisaau,si unajua watu wengi wanafanya kazi Sudan na huko DRC kwa M23!
 
ndo pakutafuta kazi upate hela ili umnase umtakaye.

kimsingi mwanaume asokuwa na kazi kuwa nae kwenye mahusiano ni mzigo wa gunia la misumari. utamtesa sana huyo dada kwasababu utamnyima raha kila muda utanung'unika tuuuuuuuu kisa yy anafanya kazi ww ni kama kochi tu humo ndani

lakini dada mapenzi si kuvumiliana katika hali zote,leo sina kesho nitakua nacho,na hakuna condition amabyo ni permanent
 
siyo wako huyo ndo mana anatumia vigezo vya kazi na pesa kukutosa........ambaye ni wako hatakuletea hvyo vigezo.........
sasa kama ni hivyo si bora aniambie wazi tu kuliko kuendelea kunitesa kijana mimi na kunipa mawazo meengi sana kichwani mwangu
 
Akunyimae kunde anakupunguzia mashuzi. Achana nae utapata wako atakaekukubali. Maisha ni kupanda na kushuka, ndoa inataka kuvumiliana in the sense ya kuaccomodate each other. Tafuta hela umdolishie na sio kumnasa
nashukuru kwa courage na ushauri ndugu
 
Si wako huyo, hata ukipata kazi akikubali si kwa sababu anakupenda...shaur yako uking'ang'ania
ni kweli ila kupenda ndiko kunakonitesa sababu nampenda kiukweli kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom