Poleni na hofu ya gonjwa hatari la corona.
Habari zenu,
Kama mtakumbuka vyema hivi karibuni nilileta ombi la kutafuta mke mwema. Mambo yakawa yanajipa taratibu sana tofauti na malengo yangu, basi wakatokeza wawili ila kuna vigezo havikukidhi. Juzi hapa nikapata mtu tukapanga tukaonana sehemu la landmark ya Ubungo.
Nilienda kama nimetoka kuchunga mbuzi sikutaka kabisa kujiweka wa juu. Tukaagiza vya kuagiza sina shida na vihela vidogo hivi. Kuku choma na mishikaki ya pale ina ubora wa kiwango cha juu. Nilivaa kiatu kimelika upande kwenye kisigino.
Kwa ufupi nilikuwa hovyo. Ikaja bili nikalipa tukaongea kupeana hadithi ya kila mmoja. Akaniuliza umejenga nikasema hapana nimepanga(jibu la uongo), akashituka nikamwambia nimenunua kiwanja Segerea ndio nimeanza kujenga! Akaniuliza una usafiri nikamwambia sina(jibu la ukweli) nikaona kabisa kashapotea.
Nikamwambia gari nilikuwa nalo ila hivi sasa nimewekeza nafuga na pia kuna ujenzi wa mashine ya kusaga na kukoboa wazo langu niwe na brand ya unga wangu.
Nikamwambia gari litakuja soon ila natarajia mke wangu atakuwa anaendesha mashine ya kusaga[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapa nikaona kabadilika kbs akasema ngoja niite uber maana kuna sehemu nawahi. Akaomba nimboost nauli nikampa 20 tukamalizana.
Asubuhi nikakutana na ujumbe toka kwake" samahani mpendwa nimeitikia wito wako ila wewe sio mwanaume wa ndoto yangu hauna nyumba hauna gari.
Halafu unasema mkeo atakuja kuendesha sijui mashine ya kusaga. Mimi nataka kuendesha Vanguard sio mashine ya kusaga. Mungu atakupa wa kufanana nawe".
Nikasema heri mtu miaka 33 anawaza kinyume na mbele. Kumbe gari ni moja ya CV ya kuonekana una hela. Siku nikiwa na miadi naomba mwenye passo aniazime.
Sent using
Jamii Forums mobile app