Nimekataliwa kisa sina gari

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,796
8,771
Poleni na hofu ya gonjwa hatari la corona.

Habari zenu,

Kama mtakumbuka vyema hivi karibuni nilileta ombi la kutafuta mke mwema. Mambo yakawa yanajipa taratibu sana tofauti na malengo yangu, basi wakatokeza wawili ila kuna vigezo havikukidhi. Juzi hapa nikapata mtu tukapanga tukaonana sehemu la landmark ya Ubungo.

Nilienda kama nimetoka kuchunga mbuzi sikutaka kabisa kujiweka wa juu. Tukaagiza vya kuagiza sina shida na vihela vidogo hivi. Kuku choma na mishikaki ya pale ina ubora wa kiwango cha juu. Nilivaa kiatu kimelika upande kwenye kisigino.

Kwa ufupi nilikuwa hovyo. Ikaja bili nikalipa tukaongea kupeana hadithi ya kila mmoja. Akaniuliza umejenga nikasema hapana nimepanga(jibu la uongo), akashituka nikamwambia nimenunua kiwanja Segerea ndio nimeanza kujenga! Akaniuliza una usafiri nikamwambia sina(jibu la ukweli) nikaona kabisa kashapotea.

Nikamwambia gari nilikuwa nalo ila hivi sasa nimewekeza nafuga na pia kuna ujenzi wa mashine ya kusaga na kukoboa wazo langu niwe na brand ya unga wangu.

Nikamwambia gari litakuja soon ila natarajia mke wangu atakuwa anaendesha mashine ya kusaga hapa nikaona kabadilika kbs akasema ngoja niite uber maana kuna sehemu nawahi. Akaomba nimboost nauli nikampa 20 tukamalizana.

Asubuhi nikakutana na ujumbe toka kwake" samahani mpendwa nimeitikia wito wako ila wewe sio mwanaume wa ndoto yangu hauna nyumba hauna gari.

Halafu unasema mkeo atakuja kuendesha sijui mashine ya kusaga. Mimi nataka kuendesha Vanguard sio mashine ya kusaga. Mungu atakupa wa kufanana nawe".

Nikasema heri mtu miaka 33 anawaza kinyume na mbele. Kumbe gari ni moja ya CV ya kuonekana una hela. Siku nikiwa na miadi naomba mwenye passo aniazime.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂 😂 😂 😂
Sasa mkuu ulitegemea kabisa aendeshe mashine ya kusaga kweli?? yaani aendeshe mashine kutoka Buza mpaka Landmark hotel.?

On a serious note; kila mtu ana lengo lake, wewe ulikuwa na lako naye hajakidhi vigezo na yeye ana lake nawe hujakidhi vigezo.!! true meaning of L.I.F.E..!!
 
Ume philosophize vyema sana, ila sauti yako inafanana na sweetlee
 
Kama umekataliwa huna gari si ununue ili usikataliwe tena,
Achana na wakina msaga sumu, mwanaume machine, ukanunua machine yako ya kusagia mahindi umpe mtoto wa kike aendeshe, inawezekana kwa kanda ya ziwa huko juu "Wasonga ugali mgumu" sio dar au pwani.
Mbona kama povu hii🙏🙏🙏🙏🙏
 
Aiseee sasa mkuu unamwambia mtu aje kuendesha mashine tena ya kusaga unga unajua kelele zake kweli

Nkupongeze kwa kuwa muwazi ila Mungu atakupa itaji lako endelea kupambana mke atafutwi anakuja mwenyewe kwenye life cycle utashangaaa tu ushamtia mtu mimba anakua mkeo wengine ndo tumeoa ivo japo sio kila mtu ataoa ivo

#Stayhome safe COVID-19 is everywhere
 
Mkuu yani wewe umeenda ukiwa fake na anakuuliza maswali baadhi unatoa majibu ya uongo halafu unataka yeye ndio awe real.?
Ulipaswa kumpa haki ya kukufahamu ndipo ajichanganye.
Hata kama wanawake wana uchu wa kupata waume bado naamini wanapenda kupata walio wa kweli na smart.
 
Poleni na hofu ya gonjwa hatari la corona.

Habari zenu
Kama mtakumbuka vyema hivi karibuni nilileta ombi la kutafuta mke mwema. Mambo yakawa yanajipa taratibu sana tofauti na malengo yangu, basi wakatokeza wawili ila kuna vigezo havikukidhi. Juzi hapa nikapata mtu tukapanga tukaonana sehemu la landmark ya ubungo.

Nilienda kama nimetoka kuchunga mbuzi sikutaka kabisa kujiweka wa juu. Tukaagiza vya kuagiza sina shida na vihela vidogo hivi. Kuku choma na mishikaki ya pale ina ubora wa kiwango cha juu. Nilivaa kiatu kimelika upande kwenye kisigino.

Kwa ufupi nilikuwa hovyo. Ikaja bili nikalipa tukaongea kupeana hadithi ya kila mmoja. Akaniuliza umejenga nikasema hapana nimepanga(jibu la uongo), akashituka nikamwambia nimenunua kiwanja Segerea ndio nimeanza kujenga! Akaniuliza una usafiri nikamwambia sina(jibu la ukweli) nikaona kabisa kashapotea.

Nikamwambia gari nilikuwa nalo ila hivi sasa nimewekeza nafuga na pia kuna ujenzi wa mashine ya kusaga na kukoboa wazo langu niwe na brand ya unga wangu.

Nikamwambia gari litakuja soon ila natarajia mke wangu atakuwa anaendesha mashine ya kusaga hapa nikaona kabadilika kbs akasema ngoja niite uber maana kuna sehemu nawahi. Akaomba nimboost nauli nikampa 20 tukamalizana.

Asubuhi nikakutana na ujumbe toka kwake" samahani mpendwa nimeitikia wito wako ila wewe sio mwanaume wa ndoto yangu hauna nyumba hauna gari.

Halafu unasema mkeo atakuja kuendesha sijui mashine ya kusaga. Mimi nataka kuendesha Vanguard sio mashine ya kusaga. Mungu atakupa wa kufanana nawe".

Nikasema heri mtu miaka 33 anawaza kinyume na mbele. Kumbe gari ni moja ya CV ya kuonekana una hela. Siku nikiwa na miadi naomba mwenye passo aniazime.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiloo Ni gume gume ivi unaweza kupata Mwanamke kwa mitandao Nina imani kubwa ila imani haijafika huko.
 
Siamini Kama mpenzi anatafutwa kwa namna hiyo kana kwamba mnasaini mkataba wa makubaliano!!

Mapenzi ni taratibu mambo kujipa mtu anakupenda kwa kukuelewa jinsi ulivyo ndio wakudumu huko unatafuta kinachotafuta hakika kupatana itakuwa inategemea na desh desh..

Endelea kutafuta watafutwa.
 
😂 😂 😂 😂
Sasa mkuu ulitegemea kabisa aendeshe mashine ya kusaga kweli?? yaani aendeshe mashine kutoka Buza mpaka Landmark hotel.?

On a serious note; kila mtu ana lengo lake, wewe ulikuwa na lako naye hajakidhi vigezo na yeye ana lake nawe hujakidhi vigezo.!! true meaning of L.I.F.E..!!
sound kool
 
Huyo ni masikini wa fikra. Pia atakuwa amekulia kwenye maisha magumu. We una tu hana ata pesa ya uber, ila bado anataka kupanda uber badala ya bodaboda au daladala.Achana nae huyo, piga kazi, halafu ipo siku utampita na gari lako akiwa kwenye Uber au kwenye kituo cha daladala au nae kwenye gari lake.
 
Back
Top Bottom