Nimekataa kumpongeza Mrisho Gambo

Mada hii inaonesha hakuna ushirikiano kati ya akili, moyo na sehemu nyingine ya mwili. Akili inasema humfahamu Gambo lakini mdomo unaimba sifa za Gambo.
 
Ubunge wa Asante bwana mkubwa ndo madhara yake haya akili inakuwa haitoi ushirikiano kuchanganua mambo..unasifia kitu ambacho hukijui afu kwa unafiki una quote hadi vifungu vya biblia..msiwe mnapenda sifa za kijinga fanyeni kazi
 
Toka DR.SLAA aondoke CDM hakuna wakuaminika tena.Nilikuwa nafikiri Prof. angetusaidia kueleza ukweli na yeye kimya,basi.........................................................................................................
 
Kimsingi mimi simfahamu sana na sina maelezo mengi kuhusu mtu niliyeamua kumzungumza leo............

Kuwa Kada wa CCM kweli yahitaji kujitoa fahamu to the maximum
 
“TUNATAKA kuona taifa hili likiwa na vijana jeuri na wenye kujiamini, wasiwe vijana waoga aina ya ‘ndiyo’ bwana, mkubwa; vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania. Tunataka vijana wenye misimamo thabiti dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika taifa,”

Haya ni maneno aliyopata kuyanena, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Siku moja wakati nasoma Biblia nilikutana na ujumbe wa Mwanzo 45:5, ulisema “Yusufu akawaambia kaka zake, ingawa ninyi mliniuza ila Mungu alikusudia kunitanguliza ili niwasaidie”

Maendeleo ama mabadiliko katika nchi yoyote yanaletwa pale kunapokuwapo na watu walio tayari kuishi maisha ya kujitoa, watu ambao wanaamini kuwa wanao wajibu mkubwa kwa jamii yao.

gambo.JPG


Kimsingi mimi simfahamu sana na sina maelezo mengi kuhusu mtu niliyeamua kumzungumza leo mwenye jina la MRISHO MASHAKA GAMBO, maana yeye akiwa kwenye Umoja wa Vijana wa CCM kama mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM 2008 – 2012 kutoka Mkoa wa Arusha, mimi nilikuwa BAVICHA, wakati mimi nikijiunga na UVCCM na CCM mwaka 2013 mwanzoni yeye alikuwa ameshateuliwa kuwa DC wa Korogwe (akiwa DC wa Kwanza kwa wakati huo kubeba matofali na kushiriki kujenga shule na zahanati na Wananchi). Hivyo ni mtu ambaye nimekuta maneno yaliyovumisha sifa yake lakini sikupata bahati ya kumfahamu vizuri.

Lakini maneno niliyoyakuta ambayo yanamuelezea GAMBO yalishabihiana sana na maneno ya Mwalimu niliyoyanukuu, kuwa GAMBO ni Kijana JEURI, JASIRI na ANAYEJIAMINI.

Nimeambiwa katika historia ya maisha yake, halijawahi kutumika neno la MUOGA, kumuelezea juu ya wajihi wake na sifa yake…wala yeye mwenyewe hajawahi kusikika katika maisha yake akitamka neno NAOGOPA, ni Kijana anayehoji kwa HOJA.

Lakini hayo ni tisa, Kumi Mrisho Gambo ni Icon kamili ya Mwanamapinduzi anayechukia mifumo kandamizi, mifumo ya Ubwana na UFISADI. Historia yake inatueleza hivyo, alimkataa Mhe Lowassa ingawa alikuwa anatoka nae Mkoa mmoja tangu akiwa UVCCM kwa sababu moja kuu UFISADI.

Kwenye title ya andiko langu nimesema nimekataa kumpongeza Gambo, ni kweli nimekataa..!! Maana sio kwa juhudi za Mrisho pekee ndizo zilizomfikisha hapo bali malezi mazuri yanayotolewa na CCM na UVCCM kwa vijana wake ndio yaliyofanikisha kuwapata Mawaziri kama akina Makamba, Mavunde, Masauni na wengineo, ni mazao ya UVCCM yaliyotuletea wakuu wa Mikoa mahiri kama akina Makonda, Gambo, Mtaka na wengineo pamoja nao Ma-DC katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu. Kwa malezi haya nimeamua kuipongeza UVCCM na CCM na kukataa kumpongeza GAMBO.

Ni CCM pekee inayojenga Vijana majasiri wanaoweza kuwahoji Viongozi wao hadharani, katika historia yake GAMBO alipishana mawazo na kuhoji hadharani juu ya Lowassa, alihojiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na wakubwa wengine pale alipoona wanaenda kinyume na matakwa na matarajio ya jamii yetu, Jamii yetu ina kiu ya Maendeleo, Kiongozi yeyote anayekwamisha maendeleo katika eneo ambalo GAMBO yupo basi huyo amejitangazia Vita na Uadui mkubwa na Kijana huyu. Daima alitaka kuona haki ikitendeka na wananchi wanahudumiwa. Hata hivi karibuni Yule jamaa wa M4C wa Arusha Mjini alipotaka kupima ubavu, alijikuta kadondokewa na kitu kizito chenye ncha kali (maana sasa hivi Serikali imepiga marufuku zile posho zao za kifisadi) Ni CCM na UVCCM sio CHADEMA, sio BAVICHA wenye uwezo wa kutoa Vijana makini na wasio waoga na mabwana ndio Mzee. Wao ni Vijana wa kusubiri maelekezo na kutumwa kubweka.

Mungu amemchagua na kumuinua GAMBO, akamtenga mbali na dhulma na wafitini. Ni kama ilivyo kwa Yusuph, MUNGU ameamua kumtanguliza Gambo ili awasaidie. Mkoa wa Arusha unakufa, biashara zimesimama, utalii unadorora, mahoteli yanafungwa kwa sababu za kipuuzu na upuuzi wa mtu mmoja na kijikikundi chake, MUNGU amemuinua GAMBO ili awasaidie kuirudisha heshima ya ARUSHA.

Nimekataa kumpongeza GAMBO lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru na kumpongeza Mhe John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwapa nafasi, hakika mimi nachukua ahadi kwako kwa niaba yao kuwa HATUTOKUANGUSHA.
UKUTA unawapa shida sana....nazidi kuamini kuwa Chadema imekua kimkakati tofauti na zamani.
 
Mkoa wa Arusha unakufa, biashara zimesimama, utalii unadorora, mahoteli yanafungwa kwa sababu za kipuuzu na upuuzi wa mtu mmoja na kijikikundi chake.

Kusimama biashara,utalii kudorola,kufungwa kwa mahoteli ni janga la Taifa haliko mkoa wa Arusha pekee yake,aliyesababisha kutokea kwa hali hiyo ana julikana na sababu zake zinajulikana huyo ndiye uliyemtusi pamoja na kijikundi chake.
 
Hueleweki,Mara unaipongeza CCM na UVCCM ,Mara unampongeza Mungu!
Hujui kwamba Mungu Mwenyezi hajangamishwi na siasa ? Mungu aapenda wema,Upendo na haki.
CCM mnapenda siasa,ghasia na dhulma ambazo ni chukizo kwa Mungu
Hahahahahahaha umenichekesha Sana Mkuu,eti anampongeza Mungu!!!
 
Yaani mwenye sifa zote ulizomwaga hapo ni mtu unayekiri kuwa haumfahamu! Naomba basi unielekeze kitabu kinachomuhusu kinaitwaje ili na mimi nimfahamu kupitia historia yake!
Labda una mahaba nae lakini Hugo Gambo hamfikii hata kidogo Mdee,Mnyika, Katani s.Katani, Heche, n.k. Acha sifa za kitoto.
 
Hivi ni kweli kwamba ndani ya CCM yoote,fisadi alikuwa ENL pekee??

Kwakweli msipojitambua wanasiasa watavipasua vichwa vyenu sana!
 
CCM bwaaaaaana LOWASA tu ndio fisadi kwao hapa tu ndio uwa nashindwa kuwaamini kabisa na sitaweza kuja kupiga kura kwa mtu yoyote wa CCM wala sitaweza kuja kujitolea kwa kitu chochote kwa CCM mana ntakuwa nafanya unafiki na mimi sio mnafiki majizi yamejaaa uko kama yule wa bariadi, wale wa ESCROW, chenji ya radar, nyumba za serikali, lugumi at least wangekuwa wanayataja na mengine kama wanavyomtaja LOWASA ningekuwa na imani ila wao fisadi lowasa wakati kuna wakina lowasa umo na zaidi ya lowasa kibao.

Mkuu umeniwakilisha. Mawazo yangu ni sawa na yako. Hao watu ni wanafiki wa kiwango cha juu. CCM ndio ngome ya ufisadi na wengine mtukufu ameapa kuwalinda kwa gharama zote.
 
tetesi la kuivunja uvccm,sasa ndo naamini ni kweli.arusha hawakai wajinga kama wa songwe.kule ni madume tena ya mbegu.subiri uone
 
Kwakweli mimi ndio maana siwezi kujitokeza na kujiita mwana CCM na kujiunga UVCCM, nitabaki tu naipigania CCM yangu kwenye eneo langu japo ni kijana, kila nikisoma bandiko la mtu ayejiita UVCCM huwa napatwa na aibu japo nipo peke yangu, hivi nyinyi UVCCM huwa mnasoma article zozote ili ziwasaidie kwenye kujenga hoja zenu ili muwakilishe kitu kinachoeleweka na kuvutia kudraw as an example, aisee kama kweli nyinyi ndio mnaoandaliwa kuja kushika nyazifa za juu huko mbeleni naona giza au kuna haja ya kuwaombea nadhani.
 
Hakika,umenena kweli.CCM bado itaedelea kutoa viongozi mbalimbali wa nchi hii kwa karne nyingi zijazo...na hata kwa upande wa upinzani wataendelea kupata wagpmbea wa nafasi mbalimbali kuanzia mashinani hadi uraisi kutoka CCM...hili halina ubishi.
unadadavua kwa kutumia kiungo gani cha mwili?
 
Back
Top Bottom