Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

aisee pole sana sana hebu kimbilia kwa Mungu hakuna kinachoshindikana kwake mwamini Mungu atakutokea hapo ulipo don't giveup mkuu hebu soma hii link hapa

 
Ndugu yangu kwa kifupi tu Ni kwamba watu wengi hawawezi kufunguka ila kiukweli wengi wanatamani wajifie tu, maana sio kwa shida hizi za dunia

Km kweli Yesu nae atarudi bora angerudi Ili tujue moja kuliko kutuweka roho juu juu tu,

Mbaya zaid kuna wengine duniani wanapigika na bado Mbinguni au peponi hawaingii,Ndo ujue kwamba mwanadam anakabiliw na shida kila kona
Huu msoto tunaoishi nao nadhani jehanamu cha mtoto
 
Maisha sio rahisi kila kona ndugu yangu, zidisha ibada zidisha juhudi.
Laana yeye mwenye anazitafuta. Tazama picha aliyoweka. Mwanaume kasuka
Atakapofanya ibada hii picha aondoe picha hii ni Machukizo mbele za Bwana
 
Tulishapita huko mkuu, kujiua sio suluhisho ila kama ameamua , Sisi katika kikao tumempa ruhusa.Kuna hukumu baada ya kifo.Na hukumu yenyewe haitabiriki.
Khaa mkuu huwezi jua anayoyapitia

Pengine nawewe kuna siku utayapitia so usijibu hivi
 
Yaani kuna jamaa kwanza kafukuzwa kazi mwezi wa nne huu, mke kaondoka na mtoto, alipata ajali ya bodaboda mguu wamekata mmoja sasa kabaki na mguu mmoja, na bado mke alibeba kila kitu, lakini anakueleza akipona kidonda cha mguu atapambana hadi dakika ya mwisho ahakikishe anarudi barabarani, NEVER GIVEUP, FORWARD. EVER BACKWARD NEVER. usikate tamaa maana halisi ya maisha ni furaha kidogo na majaribu mengi yaani unapambana na majaribu ili uifikie furaha.
 
huwezi kufa kirahisi hivyo mzee, halafu watoto wako utamwachia nani awalee? kumbuka kwamba, maisha ni zawadi Mungu anatoa, angeliweza kuwapa zawadi hiyo watu wengi sana ambao wameshafuka lakini akakupa wewe unaishi hadi leo. Mungu anakuona na anajua maisha yako yoooote. na anajua future yako.

kwenye maisha ukiona umefikia hatua kama ya kwako, hapo ndipo unamhitaji Mungu kuliko wakati wowowte ule. amini usiamini, sasaivi ninavyoongea nipo hotel nzuri nimesafiri kibiashara, lakini nilikotoka bora hata wewe una maisha mazuri.

Ukiona umefikia hatua ya maisha magumu na huoni njia, hapo Mungu huwa anakuwa karibu sanaaa, sana sana, ukimwomba anakuitikia ,kwasababu gani? ni kwasababu breakthrough utakayoipata atakayetukuzwa ni Mungu moja kwa moja na sio vitu vingine. ukipata breakthrough ukiwa na pesa kadhaa, ndugu kadhaa wanaokusaidia au kitu chochote, utasema nimefanikiwa kwasababu ya huyu au yule au kile, ila ukipata mafanikio kama muujiza hakuna atakayejidai alikusaidia ila Mungu, utukufu wote utaenda kwa Mungu ndio maana wakati kama wa kwako ni wakati muhimu sana, huoni njia, njia yako ni kwa Mungu tu, huoni wa kumlilia, wa kumlilia ni Mungu tu. hiyo ni opportunity kubwa itumie, wakati wako wa kufanikiwa umefika kama ukiitumia.

pili, Mungu amekupa zawadi ya uhai, ukiutoa/ukijiua utaenda kukutana naye, atakuhukumu na utaungua moto wa jehanum milele na milele. usifanye hivyo, kwasababu utakakoelekea ni kubaya na there is no turning back, hakunaga kule kudanganyana kwamba ukifa wenzako huku duniani watakuwa wanakuombea Mungu atakusamehe hukohuko, uongo. Baada ya kifo ni hukumu hakuna kutubu, kumbuka pia story ya yule Tajiri na masikini (sijajua dini yako)....

Mungu huwa anasikia, alisikia kwangu. ila anasikia tu kwa njia ya Yesu Kristo. Ukimkiri Yesu Kwa kinywa chako na kuamini kuwa Mungu alimfufua kwa wafu utaokoka. nenda chumbani au tafuta msaidizi wa kiroho mkiri Yesu, okoka. Mungu atajua. hili nikuambialo linaweza kuwa gumu kwako pengine, lakini jaribu, kama vile watu wanavyojaribu kwa waganga wa kienyeji na kwengine kutafuta solutions, wee pia hat akama hauamini kwa imani yako jaribu kufanya hivi nilivyokwambia ili uone inakuwaje. akili yako itaona na kupambanua kitakachofuata.

miaka kama 13 iliyopita, mara tu baada ya kuoa, niliishi maisha magumu kiasi kwamba nilikuwa natembea kwa mguu toka ubongo hadi posta na kurudi, kuna siku zingien nilikuwa na shilingi mia tano tu mfukoni siku zingine mia 200 kuna siku mimi na mke wangu tulilalia kipande kimoja cha mhogo, niliamua kumpa wife ale kwasababu mimi ni mwanaume alikataa tukamegana, ilifika kipindi sioni njia yoyote ile, kile anayekuona anakucheka badala ya kukusaidia, hakuna msaada wowote hata kwa wale uliowasaidia. tukabaki na Mungu tu. hapo ndipo nilipojifunza kusali na kuomba kwasababu hapakuwa na solution nyingine, hapakuwa na pengine pa kugeukia ila kwa Mungu tu, tulizunguka makanisa mengi mengine walitudanganya mengine ni ya kweli hadi tukasettle, tulifunga na kuomba mara nyingi sana, na Mungu akatuonekania, tumefanikiwa,wale waliotucheka wanaomba msaada kwetu, waliokuwa wanaona hatuna heshima sashaivi wanasimama kwenye kiti tukifika ili tu wapate bahati ya kutusalimia.

huyu Mungu huyu, anao uwezo kubadilisha bendera wakati wowote, God is able, he is able to change your situation within a minute utashangaa. wakati mrefu tuliishi hatuna kazi na sote tumesoma, ila kuna siku mambo yalibadilika tukapata cha kufanya na tuna maisha mazuri na watoto wazuri na wanasoma na kuishi vizuri. utukufu tunampa Mungu.

huu ushauri niliokupa umetoka kwenye kilindi cha moyo wangu, ni wa kweli, ukiufanyia kazi utakusaidia, usipoufanyia kazi nimenawa mikono.
Mkuu si umlipie hata pesa ya landlord !!!

Coz jinsi ulivyoandika ni kana kwamba unaelewa anachokipitia kutokana na uzoefu wako. Mlipie tu ili apate mahali pa kurudi jioni akitoka mishemishe zake
 
Hata nashindwa nianzie wapi! Kila nachojaribu naishia kuharibu, madeni kila kona. Linaisha hili linaibuka hili,huku watoto wagonjwa, kule mwenye nyumba hataki maelezo anadai pesa yake. Sehemu yangu ya kazi nayo wameuziwa wawekezaji wa kichina. Kwa kifupi sana nahitaji kufa.
pole sana. shukuru Mungu una viungo vyote. Jitoe ufahamu ndugu ufanye juu chini kupata hela. Ujijiua aibu haitakuacha. PAMBANA!
 
JF hakuna kabisaa watu wanaptoa practical solution. Wengi tunapiga mastory tu Kama ya church .

Mkuu husiogope wala nini, hafi mtu hapo. Hao wa wanaokudai hawana lolote la kukufanya .

Pambana tafuta Kodi tu na endelea ku fight.

Kata mshipa wa haibu .

Usirudi kijijini utakwishwa . Kama uko Dar usihame . Dar ndo mji mwepesi kuliko miji yote kuishi.
 
Ndugu yangu kwa kifupi tu Ni kwamba watu wengi hawawezi kufunguka ila kiukweli wengi wanatamani wajifie tu, maana sio kwa shida hizi za dunia

Km kweli Yesu nae atarudi bora angerudi Ili tujue moja kuliko kutuweka roho juu juu tu,

Mbaya zaid kuna wengine duniani wanapigika na bado Mbinguni au peponi hawaingii,Ndo ujue kwamba mwanadam anakabiliw na shida kila kona
Hasa mwanaume🤔🤔
 
Mkuu tuonee huruma sisi wanaume wenzako ukifa sisi ndio tutabaki tunamhudumia mke wako, kaza roho.

anasahau kwamba anakwenda kuongezwa jukumu hilo wanaume wengine ambao pia wana majanga tena kuzidi yeye.

baba yake,mama yak,wadogo zake na watoto wake wanakwenda kuwa wategemezi wa mtu mwingine.
 
Mkuu si umlipie hata pesa ya landlord !!!

Coz jinsi ulivyoandika ni kana kwamba unaelewa anachokipitia kutokana na uzoefu wako. Mlipie tu ili apate mahali pa kurudi jioni akitoka mishemishe zake
kama alichosema ni kweli, anatakiwa amtafute Mungu, Mungu ndiye atampa majibu na utukufu atampa Mungu, anatakiwa kutafuta msaada toka kwa Mungu na sio kwa wanadamu, hiyo hela ya landlord anatakiwa aiombe kwa Mungu sio kwa wanadamu, na Mungu akiamua kama itampendeza, ataongea na wanadamu kwa namna anavyojua yeye awatumie kwa namna atakayotaka yeye. Mungu hajaniambia nimlimpie, labda hajamwomba au pengine atamwambia mwingine amlipie sijui, ila upande wangu bado sijapata msukumo toka kwa Mungu. msaada wetu u katika Bwana aliyeziumba mbingu na nchi sio katika watu. huwa tunakosea tunapohitaji msaada kwa watu na kumwacha Mungu anatuangalia tu anatamani tungemwomba anaona hatumwombi tunaona wanadamu wanaweza kutoa majibu kwetu kuliko Mungu. kumbe Mungu ukimwomba, anazo njia nyingi nzuri na za msaada kuliko za wanadamu. msaada utakaopatikana kwa wanadamu kama hauna mkono wa Mungu hata hautadumu na hautakupatia suluhisho la kudumu.
 
  • Thanks
Reactions: hnp
Mawazo ya hivi nadhani huwa yanawakuta sana watu wasio waongeaji na wasioweza kujichanganya sana na watu.

Kuna watu wanaishi kwa madeni, anakopa hapa analipa pale, anaenda kopa kule analipa hapa. Na yuko fresh kama kama hana shida vile. Ila wasio waongeaji kazi ikizingua tu basi stress kama zote.

Pole mkuu usiruhusu mawazo ya kifo yakutawale, ni ujinga, upumbavu kujiua.
 
if you can make it through the night there is a brighter day
~2pac

Kaza mkuu hujui kesho unaweza kua ndio siku yako ya mwanzo wa mafanikio
 
View attachment 1995083
Leo nimetumiwa ujumbe na huyu binti. Pepole are going through tough times mkuu. Usikate tamaa. Persevere through all hardships mkuu.

Unaweza ukata tamaa lakini kuna mtu ambaye yupo kwenye tight spot zaidi yako na hajakata tamaa.

I wish you all the best.
Changamoto ni nyingi sana hapa duniani, watu wanapitia magumu mno, wengine hawana hata watu wa kuwatupia mizigo yao ili kupunguza misongo, huyu dada hadi anaomba kufa usingizini jua mambo yanaenda vibaya, iwe kiuchumi, kijamii au hata kiroho.

Muhimu mtu kama huyu inamuweka karibu, ujue nini anapitia na umsaidie, sio lazima iwe monetary, hata mawazo tu yanatosha...kufikiria kujiua ni Jambo la mwisho kabisa kwa binadamu, amefika limit.
 
Kaka kiukweli najua hali uliyo nayo kwasababu mwez huu wa kumi nimepitia kipindi kigumu Sana ..ilifikia wakat nkaona Kama nakaribia kuwehuka,..nna madeni,.mshahara Sina,Bado familia inahitaji kula,.Bado michango ya jamiii..aseee..nikapatwa depression ghafla..nikamchukia Kila nnaemuona Kama vile ndie aliesababisha matatizo yangu...
 
Pambana chief, usione wengine wanafuraha kila siku unaweza kuta wanamagumu kuliko wewe ila ni kujikaza tu mkuu..

Maisha ni vita, Kaza buti, Omba Mungu, tengeneza plan watoto wale, walale, wavae wasome....

Ni vyema ukaweka taalum yako au uzoefu wako hapa JF unahitaji msaada wa kazi basi InshaAllah unaweza kupata wepesi...
Mkuu hata ungeweka ujuzi wako hakuna atakaye kusaidia maana jf ya sasa sio ya miaka hiyo, nilisha jaribu kuweka ujuzi wangu mara nyingi tena kwa kuweka picha za kazi zangu hakuna aliye nipa kazi hata mmoja
 
Kukabiliana na hali, watu hutengana na familia zao kimkakati. Mke na watoto hurudi kwao, mwanaume anatokomea mji mwingine wenye maisha nafuu kuanzisha misingi ya himaya.
Baadaye anakwenda kuchukua familia, wanaendelea kuishi.
 
Back
Top Bottom