Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

mwenye shamba

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
1,028
Reaction score
1,892
Hata nashindwa nianzie wapi! Kila nachojaribu naishia kuharibu, madeni kila kona. Linaisha hili linaibuka hili,huku watoto wagonjwa, kule mwenye nyumba hataki maelezo anadai pesa yake. Sehemu yangu ya kazi nayo wameuziwa wawekezaji wa kichina. Kwa kifupi sana nahitaji kufa.
 
Pole dunia ndivyo ilivyo

FB_IMG_1635780338311.jpg
 
Ndugu yangu kwa kifupi tu Ni kwamba watu wengi hawawezi kufunguka ila kiukweli wengi wanatamani wajifie tu, maana sio kwa shida hizi za dunia

Km kweli Yesu nae atarudi bora angerudi Ili tujue moja kuliko kutuweka roho juu juu tu,

Mbaya zaid kuna wengine duniani wanapigika na bado Mbinguni au peponi hawaingii,Ndo ujue kwamba mwanadam anakabiliw na shida kila kona
 
Hata nashindwa nianzie wapi! kila nachojaribu naishia kuharibu,madeni kila kona. Linaisha hili linaibuka hili,huku watoto wagonjwa, kule mwenye nyumba hataki maelezo anadai pesa yake. Sehemu yangu ya kazi nayo wameuziwa wawekezaji wa kichina. Kwa kifupi sana nahitaji kufa.

Usikate tamaa... Kumbuka haupo peke yako ktk shida na matatizo...

Ukifa itasaidia nini.. pambana usichoke kutafuta fursa
 
Gari huwa ikishindwa kupanda mlima, huwa inarudi nyuma na kubadilisha gia na kuanza kupanda tena kwa mwendo wa taratibu.
Bado hujachelewa, rudisha familia kijijini...nawe urudi mjini upambane.
 
Pambana chief, usione wengine wanafuraha kila siku unaweza kuta wanamagumu kuliko wewe ila ni kujikaza tu mkuu..

Maisha ni vita, Kaza buti, Omba Mungu, tengeneza plan watoto wale, walale, wavae wasome....

Ni vyema ukaweka taalum yako au uzoefu wako hapa JF unahitaji msaada wa kazi basi InshaAllah unaweza kupata wepesi...
 
Hata nashindwa nianzie wapi! kila nachojaribu naishia kuharibu,madeni kila kona. Linaisha hili linaibuka hili,huku watoto wagonjwa, kule mwenye nyumba hataki maelezo anadai pesa yake. Sehemu yangu ya kazi nayo wameuziwa wawekezaji wa kichina. Kwa kifupi sana nahitaji kufa.
Pole sana ndungu yangu njoo pm tuyajenge tambua mungu yupo
 
Pole mkuu ila nakushauri usiwaze hicho unachokiwaza,Kusema "nataka nife" ni jambo moja na "kukikabili kifo" ni habari nyingine kabisa...Acha na habari ya kifo mzee,huko sio kuzuri sana kama umeondoka duniani vibaya.

Unachotakiwa ukifanye jaribu sana kuomba Mungu akuondoshee hyo mitihani lakini pia huenda kwa mitihani hyo unayopitia Mungu anataka akufungulie neema,Hicho unachopitia ni kipindi cha mpito tu na kiza kinene na hapo kunakaribia kucha,Vumilia na pia tambua kuna mwenzio ana ana magumu kuliko yako.

Kuwashirikisha watu kwenye shida zako ndyo nafuu kwako usikae na majambo kifuani always huwa yanatafuta upenyo yalipuke...kuwa na roho ya kiume bro shida anazo kila mtu.

Kikubwa kinachokutesa wewe ni madeni,madeni kila mtu anadaiwa mkuu sema hutakiwi kuyakimbia unatakiwa wanaokudai uwe nao karibu ukiwakmbia na wewe presha ndo inazidi,kuwa nao karibu waambie ukweli kuhusu hali yako usiwafiche na waahidi utawalipa,huku ukiendelea kuomba Mungu sana.....Nakupa siku 10 utashangaa kila balaa limeyeyuka kwa njia ambayo hata wewe utashindwa kuhadithia......Yalinikuta mimi mkuu ndomana nakwambia hivyo.

Usiwaze kujiua huko ndo kubaya zaidi mkuu.
 
Back
Top Bottom