Kingdom Finder
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 1,118
- 1,398
Kuna Mungu wa mbinguni mwenye msaada wa karibu. Mwombe atakusaidia ndugu yangu. Atakonyesha njia ya kwenda.
Ushauri kuntu sana!Pole mkuu ila nakushauri usiwaze hicho unachokiwaza,Kusema "nataka nife" ni jambo moja na "kukikabili kifo" ni habari nyingine kabisa...Acha na habari ya kifo mzee,huko sio kuzuri sana kama umeondoka duniani vibaya.
Unachotakiwa ukifanye jaribu sana kuomba Mungu akuondoshee hyo mitihani lakini pia huenda kwa mitihani hyo unayopitia Mungu anataka akufungulie neema,Hicho unachopitia ni kipindi cha mpito tu na kiza kinene na hapo kunakaribia kucha,Vumilia na pia tambua kuna mwenzio ana ana magumu kuliko yako.
Kuwashirikisha watu kwenye shida zako ndyo nafuu kwako usikae na majambo kifuani always huwa yanatafuta upenyo yalipuke...kuwa na roho ya kiume bro shida anazo kila mtu.
Kikubwa kinachokutesa wewe ni madeni,madeni kila mtu anadaiwa mkuu sema hutakiwi kuyakimbia unatakiwa wanaokudai uwe nao karibu ukiwakmbia na wewe presha ndo inazidi,kuwa nao karibu waambie ukweli kuhusu hali yako usiwafiche na waahidi utawalipa,huku ukiendelea kuomba Mungu sana.....Nakupa siku 10 utashangaa kila balaa limeyeyuka kwa njia ambayo hata wewe utashindwa kuhadithia......Yalinikuta mimi mkuu ndomana nakwambia hivyo.
Usiwaze kujiua huko ndo kubaya zaidi mkuu.