Usifike huko ndugu!!
Mimi nilitamani kufa mwaka fulani kutokana na mlundikano wa stress usiokoma tangu nikiwa mdogo.
Nilifikia hatua ya kutoboa tundu kwenye dari kwa lengo la kufunga kamba ikiwa ni hatua ya kujiandaa kujitundika lakini baada ya kutafakari kwa kina na kugundua kwamba hakuna asiepitia changamoto duniani niliona ningemkosea Mungu kukatisha uhai wangu, nilijipa moyo na kuendeleza mapambano.
Huwezi amini kutoka kukata tamaa na kuwa tumaini hata kwa waliokata tamaa;- leo hii nina elimu, nina kazi, mke, watoto wawili na nimesaidia ndugu zangu wengi kufikia malengo yao.
Kinachonisumbua kutekelezea tukio la kujiondoa uhai nikiiona ile nyumba huwa nakumbuka mbali sana.
Hata wewe unayo nafasi ya kuendelea kuishi na kufanya makubwa zaidi, usijiue Mungu bado ana jambo na wewe. .