Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

Nimekata tamaa ya kuendelea kuishi

Tiba yako ni kupata shughuli ya kufanya, tumeshakupatia neno la kiroho tayari, weka CV yako na kazi unazoweza kufanya ili wenye connection waone namna ya kukusaidia. Kulia lia tu haisaidii, maisha yanatakiwa yaendelee, na maandiko yanasema mwanaume atakula kwa jasho, na mwanamke atazaa kwa uchungu.
 
Watu wengi wanapitia magumu sn tukisema kla mtu aseme itakuwa sasa n mashindano ya shida lkn kwa ground watu weng sn tunachezea bakora za mtaa, wengi tunataman kurudi kwa Sir God ila ukifikiria napo ugali na maharage mtamu unajikuta unaghairi,

Mm cha kukwambia usijiue ukatuacha tulia tuteseke wote ipo siku uenda yakawa na mwsho,
 
Hata nashindwa nianzie wapi! kila nachojaribu naishia kuharibu,madeni kila kona. Linaisha hili linaibuka hili,huku watoto wagonjwa, kule mwenye nyumba hataki maelezo anadai pesa yake. Sehemu yangu ya kazi nayo wameuziwa wawekezaji wa kichina. Kwa kifupi sana nahitaji kufa.
Unachotakiwa kujua hayo unayoopitia ni kwa mda tu hayapo na wewe milele.
Unafikiria kutoa uhai wako kwa changamoto ambazo zipo kupita kuna watu wanaishi
na ulemavu wa kudumu na hawajawahi kuwaza hayo.
Utajiri wa kwanza ni afya njema hayo mengine ukiwa na afya unaweza yapatia ufumbuzi.
Fikiria kuhusu watu utakao waacha wanaokutegemea je utakuwa umewapunguzia matatizo au
umewaongezea?
kama ni mpenzi wa vitabu naomba unijuze nikupatie atleast unaweza pata kitu.
 
Ukianguka lazima unyanyuke, Leo unaona maisha yapo chini kesho utakuwepo juu. Ukifa wewe unawawacha watoto kwenye shida wanataka kuona tabasamu la baba yao.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Unachotakiwa kujua hayo unayoopitia ni kwa mda tu hayapo na wewe milele.
Unafikiria kutoa uhai wako kwa changamoto ambazo zipo kupita kuna watu wanaishi
na ulemavu wa kudumu na hawajawahi kuwaza hayo.
Utajiri wa kwanza ni afya njema hayo mengine ukiwa na afya unaweza yapatia ufumbuzi.
Fikiria kuhusu watu utakao waacha wanaokutegemea je utakuwa umewapunguzia matatizo au
umewaongezea?
kama ni mpenzi wa vitabu naomba unijuze nikupatie atleast unaweza pata kitu.
angalau mnanifariji ndugu zangu.
 
anasahau kwamba kuna watu ni matajiri, watoto wao wanasoma shule nzuri, wana nyumba nzuri, magari mazuri, lakini hawana afya hiyo ambayo yeye anayo. uzima aliokupa Mungu ni zawadi ya kwanza na tunao wajibu kuulinda (ndio maana tunatunza miili kwa kula, kuivalisha, kuipeleka hospital etc ili iendelee kuishi ni wajibu Mungu ametupatia kwa neema tu angewapa wengine na kuna wengien amewanyima zawadi ya uhai). pia, watoto ni zawadi toka kwa Mungu, na tunao wajibu kuwatunza na kuwalea, ukiji-delete wajibu wa kulea watoto unawmachia nani, hata huko unakoenda ukiulizwa utasejaje, na mateso watakayopata watoto wako yana sababu yeyote ya msingi?
 
Usimpe shetan utukufu ni dhambi mbaya Sana kukata tamaa
Hata maisha yawe vipi bado unazo sababu nyingi zaidi za kuishi kuliko kufa watazame wanao watabaki vipi bila wewe usiwe mnyonge wala usiogope madeni maisha hayahitaji woga KAZA BRO!
 
Afu ukifa tuu unakutana na master mwenyewe anakudai roho yake uloitoa woiii,.bro kifo kikufuate chenyewe sio wewe ukifuate ohooo,..
 
Pole sana mkuu, Usikate tamaa.

Kiukweli wengi wetu tunapitia changamoto nyingi ni uvumilivu tu, mahospitalini huko Kuna watu wanateseka sana kwa magonjwa na shida nyingi, Jela huko Kuna watu wamesingiziwa makosa Ila wapo wanavumilia wakijua ipo kesho yao njema.

Lazima tuendelee kusonga mbele, huku tukijipa matumaini ya kupata ushindi siku moja.
 
Kama unahitaji kufa sasa namba ya simu ya nini au wataka wakuletee sumu ya panya ama kitanzi [emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
anasahau kwamba kuna watu ni matajiri, watoto wao wanasoma shule nzuri, wana nyumba nzuri, magari mazuri, lakini hawana afya hiyo ambayo yeye anayo. uzima aliokupa Mungu ni zawadi ya kwanza na tunao wajibu kuulinda (ndio maana tunatunza miili kwa kula, kuivalisha, kuipeleka hospital etc ili iendelee kuishi ni wajibu Mungu ametupatia kwa neema tu angewapa wengine na kuna wengien amewanyima zawadi ya uhai). pia, watoto ni zawadi toka kwa Mungu, na tunao wajibu kuwatunza na kuwalea, ukiji-delete wajibu wa kulea watoto unawmachia nani, hata huko unakoenda ukiulizwa utasejaje, na mateso watakayopata watoto wako yana sababu yeyote ya msingi?
Ni jana tu nimetoka kusoma kitabu kinaelezea kwa nini japan kuna idadi kubwa ya wahanga wakutoa uhai wao.
Kule wanatoa uhai wao wakiamin hata akifa bima ya maisha itatoa fidia kwa familia kama wanafincial crisis.
Lakini pia hawaamini katika dini hizi wao wanajua ukifa umekufa, na ndio anachoelekea mtoa mada
hana imani katika lakini dini sio mbaya kuwa na imani katika Mungu ukiamin katika Mungu huwezi fikria kutoa uhai wako.
Pia haya maamzi niya kukurupuka tu.
kitu kimoja tu nacho kipenda kwenye dini ni kufundisha msamaha jisamehe na wasamehe wengine kama unadhani
ndio source ya matatizo yako.
Miaka mingi iliyo pita tulikuwa tukisoma na mwanafunnzi mwenzetu kidato cha tatu
huyo mtu alikuwa akipitia changamoto flani ambazo zilimpelekea kuacha shule
baada ya mda kidogo kupita tuliskia ametoa uhai wake kufuatilia sababu ni changamot flani
ambazo hata mimi nilikuwa nikipitia but approach yake ikawa ni kutoa uhai wake mimi nilichukua approach nyingine na bado
maisha yanaendelea nahiyo changamoto imekuwa history.
kwa tatizo moja kuna approach nyingi hiyo ya kutoa uhai sio approach sahih.
chagua approach sahihi ambayo unaona inafaida pana kwako na wapendwa wako.
Hizo changamoto wewe sio wa kwanza kupitia .
 
Back
Top Bottom