Nimekamatika!!!

Mkuu mbona Kuna wasichana wa kikiristo ni wengi na wazuri nenda kahudhurie ibada kanisani maeneo ya ostabey, upanga na Mikocheni, acha kufata fata wanawake wetu wa kiislamu....!


anza kuhudhuria kanisani upate saizi yako
Wewe ni mgonjwa.
 
Ndugu yangu Mimi ni mkristo mwenzio, nakushauri badili wewe ufuate huyo umpendae, kuwa muislam wala haupungukiwi chochote kutoka kwenye ukristo, sanasana huko ukriston upo tu kwavile baba na mamako wako huko, lkn wala hauna usahii wa hiyo Dini.
 
Wewe oa muislam wakati ww ni mkristo, baada ya miaka sio mingi utakuja ujute! Mimi Nina mifano hai, sio mmoja.
hata ukibadili dini kiukweli kweli kutoka moyoni kwako haitakuacha salama! Utaendelea kuishi kama mateka, na kujinasua hutaweza tena!
Kwa sasa huwezi elewa ila baada ya miaka michache na ukajaaliwa kupata watoto ndo ufahamu utakurudi! Na hutakuwa na nafasi ya kurekebisha tena!
Utaishi kwa majuto maisha yako yote yaliobaki'

Tafuta mkristo mwenzio oa hiyo muislam Mimi ndo ananifaa, ni pm namba yake"
 
Naomba Mods waufute huu uzi nimeshapata uamuzi, nitamuoa huyu mrembo......

Ahsanteni nyote mliochangia.
 
Nathani mapenzi mwisho wake ni hapa duniani tu ambapo labda niaka 10p,27 au na zaidi kidogo lakini dini ni imani inayoongoza hata maisha after death,na labda mpaka siku ya kiama na siku ya malipo.
Why urisk imani yako kwa sababu ya kitu cha muda mfupi ? Tena ambacho hakina guarantee ya kwamba mtakufa wote pamoja au mmoja wenu hatokuja kumgeuka mwenzake ? Je mmoja akija mgeuka mwenzaanke ni stress na pressure ya aina gani atamsababishia mwenzake ambaye alibadili dini kufuata yeye na si Mungu ?
Mimi naamini mapenzi huwa hayaji at first sight,at first sight huwa ni tamaa ya kingono,ila mapenzi hujengwa,kadiri unavyokuwa karibu na mwenzako na kadiri mnavyofanyiana wema na ikhsani ndvyo mapenzi pia hujengwa.
Tafuta msichana wa imani yako uoe kwani ktk mapenzi pia imani ya muumba inasaidia sana ktk kuimarisha penzi.
Alafu pia fikiria ushiriki wa ndg na familia ktk kuombea baraka za ndoa hiyo,si busara kuoana na mtu wa imani nyingine wakati wazazi wake na ndg wamegoma kushiriki.
Tafuta wa imani yako mkuu ili ukale sakramenti iliyoshiba imani siyo mtu anakula sakrament huku ndani ya nafsi yake anaona kama kioja
 
Mkuu hivi unaamini ridhaa ya mzazi kwa mwanawe ni sehemu ya mafanikio ya mtoto hapa duniani ?
 
Ndoa katika uislam ina misingi yake.
Kitendo cha kucheza na imani kwa kuingia uislam kisha baada ya dakika kadhaa kurudi ukristo tayari kunabatilisha ndoa. Kwahiyo mtabaki mnazini tu.
 


Huu ni ujinga mwingine sasa. Hizi dini za kuletewa ndizo zinatufanya sie waafrika tuchukiane na kutopendana kisa dini za watu zisizotuhusu. Inasikitisha sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…