Nimejitwika mabomu, handaki jichimbieni.

Nimejitwika mabomu, handaki jichimbieni.

hatutachimba handaki, biti usitupigie
karibu sasa sitaki, baki nje jionee
njoo hata na fataki, hofu hututii sie
lishindwa wabunge feki, nape na wake perege
yavue uje ule keki, ndani kuna raha teleeeeeeeeee!!!
!
La kuchimbia handaki, si biti kulipigia,
Hapa Jiefu ni haki, mamemba kufurahia,
Mentor kaleta keki, Invizibo lete bia,
lewapo fahamu baki, sija jitia udhia.
 
La kuchimbia handaki, si biti kulipigia,
Hapa Jiefu ni haki, mamemba kufurahia,
Mentor kaleta keki, Invizibo lete bia,
lewapo fahamu baki, sija jitia udhia.

Nafurahia kuona, amani umeiomba
nyama zizonona, umesahau kuomba
soda juisi na sayona, na pilau ya kukomba
karibu tena na tena, jisikie u kwa nyumba!
 
Nafurahia kuona, amani umeiomba
nyama zizonona, umesahau kuomba
soda juisi na sayona, na pilau ya kukomba
karibu tena na tena, jisikie u kwa nyumba!
Kila kitu nitaomba, katu siyo sayona,
JK asija tamba, shamba la bibi kuvuna,
Jua sayona ni gamba, ukiona kula kona,
Bora machozi ya simba, kikosa kunywa banana
 
Kila kitu nitaomba, katu siyo sayona,
JK asija tamba, shamba la bibi kuvuna,
Jua sayona ni gamba, ukiona kula kona,
Bora machozi la simba, kikosa kunywa banana

ala!
hilo sikulijua, asante macho fungua
jeifu fulu darasa, leo nimelitambua
sayona situgusa, wala macho itupia
mpaka gamba wajivue, au kishawatimua!
 
Duuh!!!!
JF bonge la shule, asante Sigma na Mentor kwa mashairi mazuri...
Karibu tena jamvini Sigma.
Asante profu gamba, jamvi kunisogezea
Ndugu zako wanakomba, wapi tutaegemea,
Wanabeba hadi pumba, mifugo wateketea,
Wao wanacheza rumba, gilasi wakigongea.
 
ala!
hilo sikulijua, asante macho fungua
jeifu fulu darasa, leo nimelitambua
sayona situgusa, wala macho itupia
mpaka gamba wajivue, au kishawatimua!
Tongotongo we ondoa, macho yaweze kuona,
Magamba wanadokoa, kila wanachokiona,
Jeikei anaboa, inji raisi hatuna,
Natamani kumkoa, kila nonapo sayona.
 
Tongotongo we ondoa, macho yaweze kuona,
Magamba wanadokoa, kila wanachokiona,
Jeikei anaboa, inji raisi hatuna,
Natamani kumkoa, kila nonapo sayona.

Magamba na wamezidi, kila siku wale wao
wananchi yetu bidii, jasho letu wale wao
kukataa yatubidi, kama vipi twende kwao
kujivua yawabidi, -kama vipi- sisi tuwavue wao!!!
 
Magamba na wamezidi, kila siku wale wao
wananchi yetu bidii, jasho letu wale wao
kukataa yatubidi, kama vipi twende kwao
kujivua yawabidi, -kama vipi- sisi tuwavue wao!!!
Magamba yameshabambwa, hapatoshi kwa Dodoma,
Kama Ngeleja kabebwa, ni Kikwete sio chama,
Mwisho nasema mkubwa, mizani imesimama,
Njo Mentor tule ubwabwa, pamoja na nyama choma.
 
Magamba yameshabambwa, hapatoshi kwa Dodoma,
Kama Ngeleja kabebwa, ni Kikwete sio chama,
Mwisho nasema mkubwa, mizani imesimama,
Njo Mentor tule ubwabwa, pamoja na nyama choma.

Yetu kuskilizia, hawatafanyiwa kitu
kwani si tumezoea, tume unda kila kitu
gamba mwaka wanavua, na hajang'olewa mtu
msituni kukimbilia, ndo dawa ya hawa watu!
 
Back
Top Bottom