Nimeolewa miaka kumi iliyopita na nina watoto watatu.
Tatizo nikiumwa huyu mume wangu hajali, yaani hata kukuulza unaendeleaje akuulizi, mwaka jana nilijifungua kwa operationi alikaa wiki moja siku zilizofuata akawa anarudi saa saba usiku na kuendelea, nakumbuka siku msimu wa Crismas aliondoka terehe 24 na kurudi 26 asubuhi ukimuuliza eti alikua na marafiki zake wanapiga story bora ingekua akirudi anakuja na pesa, hakuna.
Mimi ndiye ninaehudumia familia tulikua tumepanga, kodi ya nyumba umeme maji ada za watoto mimi mama mkwe nae alikua ana makazi kodi umlipie nikaamua kumchukua na tunaishi nae kupunguza gharama za maisha. Nikamwambia ahudumie chakula tu nacho hawezi.!
Lakini bado mume wangu hanithamini kurudi usiku wa manane, juzi kawahi kurudi kwenye simu yake nimekuta msg moja tu "najua haupo nyumbani mbona hujanitumia" nikamjibu yuko nyumbani nami ni mkewe unashida gani pia anamahusiano gani na mume wangu? Anielekeze kwake ili nikaongee nae! Akaniambia "muuluze mumeo anajua pa kunipata"
Najua kipato chake ni kidogo, mimi sitaki aniabudu ila nahitaji heshima na upendo tu.
​
Nimeleta huku kwakua ndani ya miaka kumi nimekua nikimwabia bila mabadiliko na wala hajibu chochote, siku 2, ya 3 anarudia vilevile.
Naomba ushauri wa kujenga wanajamvi.