Hata nikisema nimchukie haitanisaidia kitu, nimemsamehe na kumwacha aende zake

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,689
8,843
MY STORY: Tulikua tunalala chini, tumejenga nyumba 2 maduka 3, kaenda kuoa mwanamke mwingine!

Alishaanza kubadilika, anachelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine analala hukohuko, nikiongea niliishia kupata matusi, mara sina akili, anaishi na mimi kwaajili ya watoto.

Niliumia sana kwakua huyu mwanaume tulitoka naye mbali, wakati nakutana naye alikua hana kazi, tulilala chini, tukahangaika mimi nachoma vitumbua yeye kibarua wa ujenzi wakati wote tulikua na shahada lakini kwakuwa tulikua tunapendana sikuona shida.

Tulihangaika mpaka kufungua duka la vitu vya nyumbani, mimi nikiwa nauza yeye anaenda kuhangaika kwenye vibarua, alikua anajiita injinia wakati kasomea uhasibu. Alijikita kwenye ujenzi, akawa fundi mzuri.

Sikumoja nilimshauri kwakua tayari ana jina ni rahisi kupata wateja, kwanini tusibadili duka kutoka la vitu vya nyumbani tukauza vifaa vya ujenzi, alinipinga sana kuwa hatuna mtaji, tutafilisika ila kwakua nilishaona fursa na nilihisi mafanikio nililazimisha mpaka tukafungua.

Hapo ndipo kila kitu kilibadilika, akawa anapata wateja ananiletea, yaani mtu anaanza kujenga kuanzia msingi mpaka kupaua kila kitu anachukua kwetu. Kwakuwa alikua anajuana na matajiri wengi nilimshauri tuwe tunachukua vitu kwa mali kauli na kweli ilisaidia kwani baada ya miaka 5 tulikua na maduka yetu makubwa mawili, nyumba na usafiri.

Hatukufunga ndoa lakini Mungu alitubairiki watoto 3, nilipoenda kujifungua mtoto wangu wa 3 ndiyo kila kitu kilibadilika. Kwanza aliniambia kuwa nisirudi dukani, nilipohoji kwanini ikawa ugomvi, unanipangia wakati mimi ndiyo mwanaume, acha kunipanda kichwani. Hujaja na kitu chochote hapa, nishasema sikutaki dukani, sikutaki! Kuchunguza kuna mwanamke alimleta pale ndiyo awe anasimamia.

Akaniambia ni ndugu yake kumbe ni mwanamke wake, sijakaa sawa akawa hahudumii familia, matusi mengi, hanishirikishi chochote, nilikuja kushtuka baada ya mwaka kunikataza kwenda dukani nyumba zetu mbili ambazo alichukulia mkopo zinauzwa. Kufuatilia kumbe alilikua ni dili kuwa ziuzwe na Benki mimi nisipate chochote yeye aende kujenga na huyo mwanamke mwingine.

Nilipojaribu kuongea akaniambia kachoka kelele, nimuache niendelee na maisha yangu. Niliumia sana kwani tuliteseka sana, namaamisha tunapata mali anakula na mwanamke mwingine. Kwakua kila kitu kilikua kwenye majina yake na ni kama alishakiuza mimi nililazimika kukomaa na nyumba tuliyokua tukiishi, nikasema hii ni ya wanangu, alijaribu kuiuza lakini ilishindikana.

Nilihangaika mpaka TAKUKURU wale watu wa Benki aliyopanga nao wakaogopa na kuachana na ile nyumba.

Mwisho aliondoka, nilianza kazi ya kulia, kila siku kwangu ni kulia, sina kazi, sina bisashara, kahamia kwa huyo mwanamke mwingine amabye baada ya kuchunguza nikaja kugundua kuwa alikuwa ni mke wa mtu. Mume wangua kamteka akamuacha mke wake hivyo walikua wamepangisha nyumba nzima wanaishi na watoto wa huyo mwanamke, wakati wanawe hata kuhudumia hahudumii.

Kipindi chote hicho nilikua nakusoma, nilianza kukusoma tangu 2016 mwishoni, kila kitu ulichokua unaandika nilidhani ni uongo mpaka yaliponikuta. Nilikuwa shamba darasa, kwani nilikua namuamini sana mume wangu najua chake chetu, changu chetu, lakini baada ya kupata mchepuko akabaidlika. Nilinunua Kitabu cha "NDOA YANGU" nikasoma lakini hakikunisiadia, kwa wakati huo nilikua nilishaachika mwanaume anaishi na mwanamke mwingine.

Yule mwanamke alipeana talaka na mume wake, wakafunga ndoa na mume wangu mwaka jana mwezi 12. Hapo ndipo nilijuwa nimeachika, biashara zote akampa yule mwanamke. Niliumia sana kwani matumizi nililazimika kumpigia huyo dada ndiyo nitumiwe, mume wangu hakutaka hata kuongea na mimi, nililia sana.

Kilichokuwa kinanitesa zaidi ni watoto, yule mwamamke alikuwa ananitishia watoto wakikua anakuja kuwachukua. Nilikutafuta mwezi 2 dada yangu ndiyo aliniunganisha kwako, ukaniambia nina machagua maiwili, kukubali kuachika au kuendelea kulia na kuomboleza nikisubiri kunyang’anywa watoto.

Kaka nashukuru kwa kuniamsha, baada ya kuongea na wewe niliacha kujionea huruma. Niliamua kuanza biashara ya mali kauli, nilichokua nafanya ni kuzunguka katika hardwear, nakusanya tenda za mzigo na kwakua nafahamiana na wauzaji wa jumla basi nawaunganisha, nikawa kama msambazaji.

Sikuwa na mtaji hata shilingi kumi lakini kaka nashukuru. Ni mwezi 5 sasa nimeweza kusimama tena. Nimeanza upya nimejikusanya nina kamtaji natafuta fremu, nitakushirikisha ili nisikosee. Mwanume baada ya kuona nina kamaisha sasa hivi anajifanya kutaka kuja kuwaona, sina shida na hilo ila nimemwambia nitampelekea wanawe, si kuja kwangu kama vile ni mume wangu wakati tayari ana mke wake.
 
MY STORY; TULIKUA TUNALALA CHINI, TUMEJENGA NYUMBA 2 MADUKA 3 KAENDA KUOA MWANAMKE MWINGINE!

Alishaanza kubadilika, anachelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine analala hukohuko, nikiongea niliishia
Angalau umetuongezea ufahamu
 
Kuna mwamba aliwahi kuposti hii story kwamba yeye alikutana na mwanamke ambae alikuwa ni housegirl na ikawa Kama ulivyohadithia, unataka kusema ww ndie yule manzi? Au umeigeuza tu story?
 
Back
Top Bottom