Nimejitoa kwake lakini hanithamini na ananisaliti

WALUKO1

Member
Jun 22, 2015
25
5
Nimeolewa miaka kumi iliyopita na nina watoto watatu.

Tatizo nikiumwa huyu mume wangu hajali, yaani hata kukuulza unaendeleaje akuulizi, mwaka jana nilijifungua kwa operationi alikaa wiki moja siku zilizofuata akawa anarudi saa saba usiku na kuendelea, nakumbuka siku msimu wa Crismas aliondoka terehe 24 na kurudi 26 asubuhi ukimuuliza eti alikua na marafiki zake wanapiga story bora ingekua akirudi anakuja na pesa, hakuna.

Mimi ndiye ninaehudumia familia tulikua tumepanga, kodi ya nyumba umeme maji ada za watoto mimi mama mkwe nae alikua ana makazi kodi umlipie nikaamua kumchukua na tunaishi nae kupunguza gharama za maisha. Nikamwambia ahudumie chakula tu nacho hawezi.!

Lakini bado mume wangu hanithamini kurudi usiku wa manane, juzi kawahi kurudi kwenye simu yake nimekuta msg moja tu "najua haupo nyumbani mbona hujanitumia" nikamjibu yuko nyumbani nami ni mkewe unashida gani pia anamahusiano gani na mume wangu? Anielekeze kwake ili nikaongee nae! Akaniambia "muuluze mumeo anajua pa kunipata"

Najua kipato chake ni kidogo, mimi sitaki aniabudu ila nahitaji heshima na upendo tu.
​
Nimeleta huku kwakua ndani ya miaka kumi nimekua nikimwabia bila mabadiliko na wala hajibu chochote, siku 2, ya 3 anarudia vilevile.

Naomba ushauri wa kujenga wanajamvi.
 
Ok ngoja akuletee UKIMWI ndio utajua maamuzi gani uchukue kwa sasa hivi endelea kupenda
kwani navyosikiaga mapenzi ni upofu ila hii haiapply kwangu
 
Dah!
Pole sana, utakuwa unaumia sana, mmewahi kukaa chini na wakuu anaowaheshimu mkajadili hii ishu?
Ndo ule wimbo wa Kassim Mganga wa subira nawasihi mabinti wausikilizage na kuuelewa.
 
Siku ukipata ujasiri wa kutosha ondoka, maana inaonyesha sasa hauna ujasiri wowote

Kuondoka siwezi, kwakua ili kuepuka garama za kodi ilibidi ninunue pagale ambalo tunaishi sasa nilimshirikisha wakati wa kununua ingawa niliandika jina langu baada ya kuona mwenzangu aheleweki
 
Pole sana mami mambo ya wawili ni magumu kushauri lakini kwa hapo ulipofikia hatuna budi kushauri

mami ndoa iliwekwa ili wawili wapendanao waishi kwa upendo furaha na amani,uaminfu na wasadiane pia je wewe unapata vyote hivyo kutokana na ndoa yako?

mwanzilisha wa ndoa yaani Mungu kupitia mwongozo wa kitabu chake biblia ameruhus ndoa kuishi ikiwa mmojawapo katika ndoa si mwaminifu au msaliti?wewe ni kipi kinakuzuia kuivunja ndoa yenu?bado unampenda sana mume wako licha ya matatizo yote anayoyanfanya?
 
Eti mama mkwe ukashindwa kumlipia ukamleta kwako muishi nae..

wewe labda viboko ndo vitakusaidia..........

tafuta psychologist kwanza matatizo yako yako so deep

huyo mume hata akikuacha utaenda kutafuta 'kimeo' kingine hatari kuliko hiko

'una slavery mentality'......unataka uwe mtumwa kwa mtu ndo ujione 'unapendwa'
na jitahada zako za 'kitumwa' ndo unaona sifa na uvumilivu...

tatizo lako liko so deep......wanawake wa aina yako huwa wanaolewa na kimeo kama chako
ndugu wakijitahidi uachane nacho huja kuolewa na kimeo kikali kuliko hiko

ndo wale unasikia 'alipigwa na mumewe hadi akavunjwa mguu'

au wengine anapigwa hadi kifo na 'mumewe'

.
 
Miaka kumi ndo muda wake wa kubadilika, atabadilika mwenyewe...we usimjali hata chakula usimpikie.

Elekeza nguvu na upendo kwa watoto washakuwa wakubwa ila usiachane naye, muda wa kuachana umeshapita labda akuache yeye.

usiruhusu akupige au akufokee, ila akirudi usiku wa manane mfungulie kimyakimya watoto wasijue kama kuna bifu.
 
Dah!
Pole sana, utakuwa unaumia sana, mmewahi kukaa chini na wakuu anaowaheshimu mkajadili hii ishu?
Ndo ule wimbo wa Kassim Mganga wa subira nawasihi mabinti wausikilizage na kuuelewa.

Sijawahi binafsi naona ni kujidhalilisha kwa watu na kuwapa faida ndo maana nimeona nilite uku alafu nifanye maamuzi uku nikimuomba Mungu.
 
Si ulisema utampenda katika shida na raha? Sasa huu ni wakati wa shida we komaa tu! Hata kama ni mleviii...
Huyo nichaguo lakoooo.....
 
As pathetic as she sounds, you've got to give it up to the lady. She still has respect and love for the mudhafool. And he deserves none of that.
 
Sijawahi binafsi naona ni kujidhalilisha kwa watu na kuwapa faida ndo maana nimeona nilite uku alafu nifanye maamuzi uku nikimuomba Mungu.

Sasa ukikaa kimya 'utaoza' ndani. Miaka kumi ni mingi, kama habadiliki, wewe fanya maamuzi magumu na sahihi kwa ajili yako na watoto.
 
Kuendelea kulia katika Moto Huku Ikiwa Uwezo wa Kujitoa Upo ni Kuidhulumu nafsi na Moyo Wako... Jiangalie Wewe na Uwaangalie Watoto wako kisha jiulize Mwenyewe ni Vipi utaishi na Familia Iwapo Atakuletea Magonjwa Hasa Ukimwi.?

Maisha Yako Yana thamani Zaidi Ya Mwanaume Msaliti na Asiyejali.. Na Siwezi kukwambia Uachane nae kwa Kuwa Sijui Ni wapi Mlipotoka na nikwakiasi gani unampenda, bali nataka nikwambie

JIFIKIRIE, JIHURUMIE NA KUJIPENDA

UKIONA ANAPASWA KUACHWA FANYA HIVYO KABLA HUJAHARIBU MAISHA YAKO..
 
omba mungu....mitihani hii ni mingi....ulivyoanza hadithia nilijua ni mimi mhusika...manake stori yangu imeshahabiana sana na yako...nami nilimtesa sana mama watoto watatu wangu ndani ya miaka kumi...ingawa mimi ndiye nilikuwa ninahudumia kila kitu lakini sijui ujana au la!....lakini ikafika mahali nikajitambua..sijajua alitumia mbinu gani lakini hakukata tamaa....nami nilijirudi...nikawa nimefika mwisho wa vitimbi kwake......sasa ninaeleweka home....ukipenda ni pm kwa maelezo zaidi...
 
Back
Top Bottom