Nimejifunza mengi katika muda mchache

Lighton

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
2,072
Reaction score
3,482
Wakuu..... imepita kama mwezi 1 na nusu tokea nipitie changamoto ambayo baadae ilinipa funzo kuhusu namna ya kuishi kwa mipango. Nilipuuzia sana kuhusu pesa ya akiba, sikuwa na bajeti ya matukio ya imejens.

Basi siku hiyo ikafika, nikamgonga mlevi mmoja alikuwa anakatisha barabarani, mlevi alikuwa ana hali mbaya mpaka waliweka mahabusu usiku huo, ilikuwa kwa mara ya kwanza. Bahati nzuri kesho yake nilitoka nikafatilia hali ya mgonjwa nikaambiwa ameamka, taratibu za matibabu ziliendelea ndugu walipata pa kupiga pesa, kiufupi niliyumba kiuchumi.

Nikaanza kufatilia gari polisi, yaani wale ndo wehu kabisa, lakini nashukuru nilimaliza salama na polisi na wale ndugu wa mgonjwa.

-Polisi wana tamaa sana, huku mitaani kuna ujinga mwingi sana.
-Chombo kuwa na bima ni muhimu sana.
-Ni muhimu pia kuijua sheria na nimejifunza kwamba next time nimemgonga mtu ni full kutembea walimwengu wa mitaani humu ni miyeyusho sana.
-Wakuu akiba ya imejens ni muhimu sana, hata ukipata pesa mingi sana bora ijaze kwenye akaunti yako itakuja kuwa na umuhimu sana baadae.

Nasisitiza polisi wana tamaa sana.
 
Kweli mkuu, hili ni funzo ambalo mtu anaweza kulipata kwa gharama kubwa. Akiba ya dharura, bima na kuijua sheria ni vitu ambavyo tunavipuuzia mpaka changamoto itokee. Muhimu zaidi ni kwamba ulimaliza salama na umechukua somo. Maisha yanafundisha sana.
 
Mambo ya kawaida hayo, usiwe na wasiwasi na maisha na changamoto ndo maisha.Si unaona hukua na akiba, lkn si umesolve, na umetoka licha ya kutokuwa na akiba, HAPO UJIFUNZE KUWA KILA KITU AU TATIZO LINA MAJIBUA...kwamba uishi kwa kuweka akiba ili siku ukigonga mtu umlipe ama???
Akiba huwa zinakupa confidence tu lkn inaweza isisaidie sana.Uneweka akiba ya 20M linakuja liugonjwa upelekwe India etc...inakua hewa tu.Tuombe Mungu atusaidie tu
 
Akiba ni kwaajili ya kupunguza mambo si kuyasolve kwa 100% ila usipokuwa nayo kabisa ni hatari
 
kudhibiti tamaa za polisi na kundi lingine lolote, cha kwanza ni kuhakikisha wewe upo upande sahihi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
mfano umedakwa na polisi alafu huna leseni, hapa ni lazima uchanganyikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…