Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

Nimejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu

nmekaa kitambo sijasoma uzi wangu huu. nilikua naogopa mno. mwanzon nimepata disappointments saana na comments za watu. zikawa zinanifanya najisikia vibaya. so nikakata shauri sitatembelea tena kusoma lolote katika uzi huu. sababu me ni aina ya wale watu hatuwezi vumilia kasha kasha za kusemwa na watu. unakutana na comment mtu anasema MKUU SASA HAPO UTASEMA UNAISHI KTK NYUMBA AU KTK PAGALE. daaah noma saana maraia.

kuhusu maji ya kujengea na kumwagilia ktk bajeti nilitenga 400k tsh. lkn kwa bahati nzuri mzee wa nyumba ya jirani ana kisima so akanambia nitumie tuu. so nikapata maji bure. mafundi walikua wanaenda kuchota sio mbali.

kuhusu fundi ni huyo huyo mmoja. kutoka kuchimba msingi, kuezeka. kujenga choo. kuweka ma grill ambayo nilinunua. vitasa sijaweka bado mkuu soma maelezo fresh. nmeweka geti tuu then nmeli cover na nyavu kuzuia mbu. u know.
Safi sana mkuu huna haja ya kuwa mnyonge la msingi unapiga mswaki kutokea uwanjani kwako.
 
Hongera huo ndio uanaume, picha tafadhali!!!!. Nimepata kawivu ka maendeleo. Nilikuwa na pesa kama hiyo ila imepukutika kwa kujihudumia nilipokuwa naumwa, nimeudhika sana, kuanza moja kuitafuta tena ni neema za kiMungu sasa!. Hongera sana kwa mara nyingine.
Pole sana mkuu, jitahidi uwe na bima ya afya inasaidia sana, sisi sote ni wagonjwa watarajiwa katika siku yoyote katika maisha yetu.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nimejenga kibanda vyumba vi3 stoo,kijsebule na choo. Hapo kuna, haijafika miez mingi mbao zinaliwa, chini mwa Mkanda Wa nyumba kabla kwenye Msingi Mchwa wamechimba handaki. Naumwa hapa nilipo
Doh wadudu nuksi hao. jitahd upate wataalam wachimbe apo chini wawatoe watakusumbua sana. hao wadudu hawafai wanaharibu sana nyumba. siku ingine utashangaa wametafuna kila kitu (meza, vtanda,milango,madrisha).
 
Hiyo bati gauge 32 ni kama hiyo hela umetupa mkuu. Hamna bati hapo kabisaaa. Halafu mwaka 2018 kwa bei ya hicho kiwanja na ukubwa wake na eneo mbona ghali?
 
Clinker belite,

Safiiii kamanda..! Huu uthubutu mzuri

Ila JF bana kwenye ule uzi wa ujenzi kila mtu anajimwambafai kujenga mpaka uwe na million 50... mwingine kupaua tu katumia 15 million.
Kutishana tu, ila kiukweli kujenga ni usimamizi shapavu na uwe na pesa ya lumpsum ukianza basi usogeze hatua kubwa kama alivyofanya jamaa huyu..

Huyu jamaa akija kutia tena million 7 nyingine kwenye hii nyumba inakuwa ishaisha kila kitu na ya kisasa zaidi..
 
Kwanza nikupe hongera sana kwa kujenga nyumba ambayo wengi wanaita ni banda

Amini kuwa ni wengi wanataman kufika hapo ulipo fika lakn hawana huo uwezo

Amini kuna watu wapo dar es salaam sio chini ya miaka kumi ila hawana hata kiwanja

Amini kuna watu wamezaa na watoto wao wako darasa la saba ila wamezaliwa kwenye nyumba za kupanga

Amini kuwa nyumba yako ni bora sana na itakusaidia kufanya mambo mengi kwa Uhuru ( nilitaka nisimulie kisa cha mimi kufuga mbwa kwenye nyumba ya kupanga na kufukuzwa kisa niligoma kumtoa mbwa wangu)

Amini kuwa unafanya jambo ambalo wengi wameshindwa kulifanya ( achana ha hao wanaojenga mijengo ya gharama /migorofa ukajiona wewe sio kitu )

Mwisho nikupongeza na nikushukuru kwa kutupa moyo wengi wetu humu wew ni mfano bora kwetu na tumejifunza kutoka kwako na tutachukua hatua kama ulivyochukua mda mwingine tunahitaji watu wa kututia moyo kama ww .
 
Kuna jukwaa la ujenzi,mods hamishia hii thread huko

Hata kwa mil.2 unaweza inategemea unajenga nyumba au kibanda
 
Wakuu, poleni na janga hili la corona. I hope mnachukua tahadhari zote ili kubaki salama. Basi leo nimeona vema nishee namna nilovokamilisha ujenzi wa kijibanda changu. Najua kuna mtu ntakua nmemsaidia na kumtia moyo kwamba kwa kidogo alichonacho, inawezekana kuepukana na adha za ma faza house.

Nyumba nimejenga ni ndogo ila inanitosha. Ni vyumba viwili vya kulala, sebule, choo na korido fulani ambapo ndo kuna jiko kupikia. Kiwanja nilinunua 25 kwa 25 nilinunua mwaka juzi 2018 kwa sh milion4.5 locationi ni madale mwisho. So nkaona kujenga nyumba kubwa itanichukua muda mrefu kulinganisha na kipato changu, so nkajenga nyumba hii ndogo pemben kabisa ya uwanza, na kuacha nafasi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kubwa hapo baadae. Nyumba hii imeanza kuchimbwa msingi tar 22 feb 2020 na baada ya siku 29 me nkahamia.

Baada ya kuezeka milangoni na madirisha nmewekaMa drill. Na nyavu za kukinga mbu. Bado cjaweka plasta. Na chini ni rough floor. Sijaweka ceiling board , namaanisha dari. Hii nmeweka chooni tuu. Milango ya mbao ni miwili wa chooni na wa sebuleni. Umeme pia bado ila nmeshalipia nawasubiri jamaa wakuje kuwasha.

So nyumba hii cjacomplicate saana. Nmejenga simple tuu. Maana kuna bandiko niliona humu jf jamaa alisema ujenzi ni ww na maamuzi yako unatakaje. Unaweza jenga kwa m10 ramani ile ile ambayo mwingne kajenga kwa m20.

Gharama za ujenzi.
Vifaa vya ujenzi vyote vilinunuliwa siku moja. Tar 22 feb 2020. Lengo la kununua kwa siku moja ni kupunguza gharama za usafiri kununua kimoja kimoja. Nilinunua na nikaweka hapa kwa jirani yangu.

Vifaa vyote vilinunuliwa maduka ya madale mwisho. Actually kabla sijanunua nilienda maduka ya town tegeta kule, nkaulizia bei baada ya kupiga tathmin nkagundua cjakwepa kitu. Nei ni zile zile tuu. So nkaona bora ninunue madale ntasave kidogo kweenye usafiri. So gharama ni kama ifuatavyo.

Bati geji 32 @ 18,500 = 740,000
Cement 37 @13,500 = 499,500
Mbao papi 18 @ 10,000 = 180,000
Mbao kenchi 40 @ 5,800 = 232,000
Mbao zege 15 @ 7,500= 112,500
Misumari nchi 4 kg 10 @ 3,000 = 30,000
Misumari bati kg 9 @ 6,000 = 54,000
Misumari nchi 3 kg 2 @ 3,000 = 6,000
Koa 2 @ 3,500= 7,000
Nondo 10 @ 18,000 = 180,000
Sink la choo 1 @ 18,000
Bomba 2 nchi 4 @ 13,000 = 26,000
Bomba nusu nchi 1.5 @ 7,500 = 3,500
Pitrap 1 @ 2,500
Elbow 2 @ 3,500 = 7,000
Usafiri 40,000
Kuchimba shimo la choo 230,000
Mchanga tipa 4 @55,000 = 220,000
Kokoto tipa 1 @ 150,000
Tofali 1650 @ 1025 = 1,691,250
Grill madirisha 4 @ 150,000= 600,000
Grill mlango 1 @ 200,000
Grill dirisha choo 1 @ 30,000
Mlango wa sebule 150,000
Nyavu za mbu na zile zingne nilisahau kurekodi. Lets say 100,000

Fundi 1,300,000 ( alifanya kila kitu)
Saidia fundi 29 days @10,000 = 290,000
Chakula mchana 29 days @ 3,000= 87,000
Jumla niliyopata kwa gharama zote hizo juu ni
7,200,000


Sent using Jamii Forums mobile app

Hongera sana.
Penye nia pana njia.
 
Back
Top Bottom