Nimeita mmoja wamekuja wanne

Usikute huyo aliye mwita ndo anataka awe girlfriend sasa kaja na team nzima kama TP Mazembe.

Hahahah lol
Kama ndio hivyo
asinge mwita bar
Ampeleke beachsehemu
ambazo hawata spent fedha..

Na akitaka
kumtoa out
amwambie ukweli
"I will prefer if you come alone
I will take you home any time you want"
kama msichana ni mwelewa basi atafanya hivyo..
some time is good to be straight forward..
 
wakija wengi usiogope kabla hawajaagiza piga funda la mwisho toa excuse ya kuhamia venue ingine we na unayemkusudia
 
Mwacheni huyo sharobaro imgharimu huwa wanataka wenyewe hawa kuchunwa...si unajua moja ya vigezo vya sharobaro ni kujifanya tawi la juu siku zote....usije kulia upumbavu hapa kama una issue ya maana tuletee tujadili na sio hizi show off zako Ebo!
 
Nilishawahi kusema humu ndani na nitarudia tena,dawa ya watu wa hivyo ni ndogo sana,wakaribishe unapoishi hata waje kumi poa tu kisha unawasongea ugali wa nguvu unawawekea mezani,mkimaliza kula ndio unafanya mtoko mkifika huko ni vinywaji tu hakuna gharama ya mlo na wakiulizia mlo nawe unawauliza kwani hamkushiba ule ugali?
 
Kuna mshikaji mmoja ilimtokea ishu kama siku ya kwanza akaona isiwe noma akalipa bili, siku nyingine alipomuita akaja na wenzake wanne tena wakawa wanaagiza whisky per tot wengine wakaagiza chupa nzima ya wine, jamaa alichofanya alisubiri bili ilipofika kama 70,000 hivi akawaambia nakuja naenda chooni mara moja kumbe ndio kimoja wale wadada wamekaa imepita saa moja na nusu hawaoni mtu baadae yule dada akapokea ujumbe kwenye simu yake unasema "Siku nyingine ukome kuja na rafiki zako mimi sio ATM" wale wadada ilibidi waweke simu zao bond.
 
Hapo kuna tafsiri tatu:
1.Huenda mlengwa anapenda sifa kwa wenzie kwamba mshikaji wake anazo kwa hiyo watoke(kwa kujitambua)
2.Ushamba wa mlengwa(msichana) kutaka sifa kwa wenzie(kwa kutojitambua)
3.Wamekudiskasi na kusema jamaa anajipendekeza waje kukuchuna na ukome
Dawa ni kuzungumza na mwenzio na kumpa laivu kuwa hupendi tabia ya kuja na lundo la watu la sivyo akutaarifu kwanza kuwa anakuja na wenzie.Kama haelewi lamba wote
 
Wakija wote we anza kuwapapasa wote kana kwamba umelewa na mwisho wasifie rafiki zake ni warembo na huku ukijilaumu kwa nini hukukutana nao hao hapo kabla!
 
Nilishawahi kusema humu ndani na nitarudia tena,dawa ya watu wa hivyo ni ndogo sana,wakaribishe unapoishi hata waje kumi poa tu kisha unawasongea ugali wa nguvu unawawekea mezani,mkimaliza kula ndio unafanya mtoko mkifika huko ni vinywaji tu hakuna gharama ya mlo na wakiulizia mlo nawe unawauliza kwani hamkushiba ule ugali?

nimecheka sana. Gud idea!!!
 
Kama una 10,000/= mfukoni unaita binti baa ili iweje? Mapenzi na Mkono wa Birika haviendani - Kama huna pesa acha kusumbua mabinti zetu - Endeleaa na shule na mambo yakishakaa sawa utakuwa na uwezo wa kualika hata Baba na Mama yake binti pale Giraffe weekend moja...

Mbona watu munakuwa wakali badala ya kujibu mulichoulizwa!! Kwani amemwambia kusanya rafiki zako muje au amemwambia aende mwenyewe yawezekana anahitaji kuwa na mbadilishano wa mawazo tu lakini wakat huo wakipata hata maji ya mia tano mia tano tu maana ni bar hakusema guest?? kitu nilicho gundua wengi wetu tuna mawazo ya ngono na hatuwezi kutofautisha kati ya bar na guest! anyway mm nafikiri ndugu uwe unamwambia kuwa aje mwenyewe na sababu no financial constratints maana kama ni muelewa atakuja!

Asanteni
 
Kama anampenda amwambie tu ukweli kua aje alone hana uwezo wa kuhudumia team nzima,sasa kama ndo kujidai matawi unaumia afu unakuja kulia JF haisaidii chochote

Sawa sawa mkuu vile vile inategemea alimwita hiyo bar ni matawi ya juu au ya kawaida.

Kama alimwita samaki samaki Mlimani City basi alijionyesha kuwa yeye ni matawi.
 
Achana na wanafunzi watakusumbua sana.. Hii ndio dawa ya kudumu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom