Nimeingia choo cha kiume bila kujua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kiume bila kujua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Hun, Oct 17, 2012.

 1. H

  Hun Senior Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Nilikuwa kwenye dimbwi la mapenzi na kijana mmoja,kwa kipindi hiko nilikuwa ninampenda mnoo,ikatokea ya kuwa tunataka kuoana lakini kwa kuwa tulitofautiana imani basi ndugu zake waliweka kizuizi wakitaka mimi ndo nibadilishe dini.
  Sisi tulishaamua ya kuwa tutafunga ndoa ya bomani lakini hawakutaka hilo.

  Siku zilienda na likatujia wazo ya kuwa tuondoke tukaishi nje ya nchi,tukafanya taratibu zote za safari na wakati tuko kwenye process hizo kuna rafiki ambaye alikuwa hiyo nchi tunayoenda alitushauri ya kuwa tufunge ndoa ya bomani halafu tukabadilishe cheti kiwe 'copy of an entry' yaani international marriage certificate ili visa ikiexpire mmoja wetu ataweza kuapply kama dependant. Kwa kweli tulifanya hivyo na kila visa ikiisha mimi ndo nilikuwa na apply kama dependant.

  Sasa tatizo limekuja hivi, tangu tuanze mahusiano tuna miaka saba,tulivyofika huko kijana akapotezea maswala ya ndoa na mi nikakaa kimya sijamgusia,mwaka jana tukaamua kurudi nyumbani bado mwenzangu hagusii neno ila maswahiba ya hapa na pale ndo mengi. Ikafikia kipindi nikajianalyse na nini nataka maishani nikamwambia kila mtu ashike ustaarabu wake,haa!!mwenzangu hataki kuamini kuwa namuacha maana alikuwa anajua ninampenda kuliko kitu chochote na alikuwa akifanya maujinga yake anadiriki kusema kuwa siwezi kumwacha nikimwacha yeye sitopata mwanaume mzuri na mwenye maendeleo kama yeye. sasa hivi ananitishia kuwa hata nikiolewa nitapata shida maana bado ana cheti cha ndoa atanifanyia fujo nisiwe na amani. Mwe!!nimeingia choo cha kiume bila kujijua, na sijui natokaje.Huruma mie Hun jamani looh!
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  nice story
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Labda uwe muwazi shida ni nini haswa?
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Unataka umwache mmeo?? afu ukafunge ndoa na mme mwingine??

  Maliage bana!
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Shida visa yake imekuwa dependant

   
 6. H

  Hun Senior Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  it's actually a true story. i just don't know how to get off it
   
 7. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dear Hun, kwanza kabisa Username yako nimeipenda. kwa Ki-danish maana yake ni mtoto wa mwanamke. ..wakati wa mtoto wa kiume ni Han. Pili, pole sana na yaliyokukuta.Labda mwenzako huyo hajui maana ya neno "NDOA" wala umuhimu wa wewe ku-aplly kama dependant.
   
 8. H

  Hun Senior Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  shida ni kwamba amekuwa ananiabuse physically and emotionally,nimevumilia ila nimefika mwisho.sasa nimeamua kila mtu aanze maisha upya,anasema nimempotezea muda hatakubali kuniacha kirahisi itanicost forever mana atatumia kile cheti
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  so hakupendi tena? Umeongea nae kuhusu mapenzi au mpo kicheti zaidi?
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  Kongosho nyie wenye ndoa zenye utata mpeni maushauri bi dada.
   
 11. H

  Hun Senior Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  wakati wote akinipiga na kuniabuse emotionally nilikuwa namwambia kuhusu mapenzi na nini.kwanza hatujawahi kuongelea habari cha cheti mpaka yeye jana ndo kaniambia kuwa atanikomoa.sijui najinasuaje sasa nimeloba stepu uuwii
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  twende taratibu isiwe wewe ndo una makosa..mnaishije? mnalala wote? mnashirikiana kiuchumi? mna watoto? maana hapa unaongelea upande wa mabaya tu
   
 13. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Haueleweki bi dada! Sasa unataka kufunga ndoa ya pili? Si uombe talaka kwanza halafu ndo uendelee?

  Au mi sijaelewa?
   
 14. H

  Hun Senior Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  okaay,ni hivi.ile ndoa tulifunga kwasababu tu ya mambo ya visa na vitu kama hivyo tutakapofika huko nje,na ilibaki kuwa siri yangu na yake tu.hakuna mtu anayetuhusu anajua.

  Kila mtu anaishi kivyake, na hatuna watoto.kila mtu ana kazi yake ila mambo ya maendeleo tunashirikiana.
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  bado bado sijakupata...so mlikuwa hamna feelings za kimapenzi sio? i mean ilikuwa ni ndoa ya makaratasi tu but no any other string attached ama?
   
 16. H

  Hun Senior Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  tulikuwa ni wapenzi na tulikuwa na mipango ya kuoana,hiyo ya cheti ilikuja tu ili kurahisisha mambo ya visa na nini. ila baada ya kukaa muda mwenzangu akanibadilikia akawa kitu kidogo ananigombeza ananipiga na hata kuongea na wanawake zake mbele yangu.sasa nimevumilia nimechoka ndo nimemwacha lakini yeye ndo anataka kutumia cheti.

  Smile hapa nimeeleweka mpendwa?
   
 17. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,460
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  pole de bora K,za UKonga?
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ndugu za mwanaume waliweka kizuizi kwa sababu ya dini, lakini hasemi kama ndugu zake yeye hawakuweka kizuizi. Bila shaka hakutaka ushauri mwanzoni, now she has learned her lesson.
   
 19. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  Dada yangu una umri wa miaka mingapi? Halafu elewa kukwaluzana kwenye doa kupo tu. Kinachoonekana hapa wewe unamajibu mabaya kwa jamaa yako. Ogea naye vizuri, vilevile hata wewe hutaki kujenga ndoa unataka muachane.

  Sister angalia kauli zako huenda wewe ndio chanzo. Hapa inavyoonekana jamaa anakupenda ndio maana anakufuatilia ila kulingana na majibu yako na namna unavyojihisi kuwa hakupendi ndio matokeo yake hayo.

  Mwite muongee, achana na mambo ya cheti angalia uhusiano.

  Poa?
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Omba divorce kisheria, au unataka kuondoka kinyemela??

  Wazazi bana wakikataa kitu sometimes, labda tu walisema dini ila waliona hakifai

  Ila, kila mahusiano yana matatizo yake.

  Mshangao: Wee ndio uko kwenye mikakati ya kuachana na mmeo afu tayari ushapata njemba ya kukuoa??
   
Loading...