Nimeingia choo cha kiume bila kujua

tulikuwa ni wapenzi na tulikuwa na mipango ya kuoana,hiyo ya cheti ilikuja tu ili kurahisisha mambo ya visa na nini. ila baada ya kukaa muda mwenzangu akanibadilikia akawa kitu kidogo ananigombeza ananipiga na hata kuongea na wanawake zake mbele yangu.sasa nimevumilia nimechoka ndo nimemwacha lakini yeye ndo anataka kutumia cheti.

Smile hapa nimeeleweka mpendwa?
kweli umeingia choo cha wazee? sasa anakutakia nini wakati hakupendi si akuache uende zako?
 
Omba divorce kisheria, au unataka kuondoka kinyemela??

Wazazi bana wakikataa kitu sometimes, labda tu walisema dini ila waliona hakifai

Ila, kila mahusiano yana matatizo yake.

Mshangao: Wee ndio uko kwenye mikakati ya kuachana na mmeo afu tayari ushapata njemba ya kukuoa??

Hapana sina njemba ya kunioa ,hahah umenifanya nicheke..yeye ndo anasema ya kuwa hata ikitokea nikiolewa atanifanyia fujo labda nikae single.
 
Hun kama sijakuelewa vizuri nisahihishe!
-mlifunga ndoa ili mpate visa au ili mpate kuishi pamoja kama mke na mume japo ni dini tofauti?
-miaka 7 umeishi na mwanaume amabye hakutaki tena au we ndo humtaki tena?
-zaidi ya kuona hataki mfunge ndoa kwa imani ya mmoja wenu huyo mumeo ana shida gani nyingine?
-mambo ya maendeleo mliyoshirikiana mlishirikiana kama mke na mume sio?sasa huoni kama unataka kuachana nae ukijaribu kusema hakuwa mumeo utakuwa umejikosesha haki zako za kimsingi?
-zipo taratibu za kufuatwa kama unataka kutalikiwa that means hicho cheti kinatumika,sasa kama hutaki kitumike hizo taratibu zitafuatwa vipi?
hebu tuweke sawa hapa tukusaidie!
 
Last edited by a moderator:
ndugu za mwanaume waliweka kizuizi kwa sababu ya dini, lakini hasemi kama ndugu zake yeye hawakuweka kizuizi. Bila shaka hakutaka ushauri mwanzoni, now she has learned her lesson.

ndugu zake walitaka mimi nibadili dini hawakutaka hata ndoa ya bomani,ndugu zangu mie hawakutaka nibadili dini ila ndoa ya bomani hawakuwa na tatizo.najua nimefanya makosa nachohitaji ni kujinasua kwenye hili
 
Dada yangu una umri wa miaka mingapi? Halafu elewa kukwaluzana kwenye doa kupo tu. Kinachoonekana hapa wewe unamajibu mabaya kwa jamaa yako. Ogea naye vizuri, vilevile hata wewe hutaki kujenga ndoa unataka muachane.

Sister angalia kauli zako huenda wewe ndio chanzo. Hapa inavyoonekana jamaa anakupenda ndio maana anakufuatilia ila kulingana na majibu yako na namna unavyojihisi kuwa hakupendi ndio matokeo yake hayo.

Mwite muongee, achana na mambo ya cheti angalia uhusiano.

Poa?

Kusema ukweli sina tabia ya kumjibiza,sina kauli mbaya hata kidogo.tunakwaruzana mara nyingi kwa sababu ya jinsi anavyonitreat, saa nyingine anaweza kuniongelesha vibaya mbele ya ndugu zake mpaka wanamshangaa,lakini navumilia. lakini kila jambo lina mwisho wake.
nimeongea nae zaidi ya mara kumi atajirekebisha for two days then anaanza upya.
 
Ndugu zake walisha kukataa wewe ukajifanya kenge na kuingia kichwa kichwa ona sasa yamekukuta rudi bomani uulize jinsi ya kuvunja ndoa.
 
ndugu zake walitaka mimi nibadili dini hawakutaka hata ndoa ya bomani,ndugu zangu mie hawakutaka nibadili dini ila ndoa ya bomani hawakuwa na tatizo.najua nimefanya makosa nachohitaji ni kujinasua kwenye hili

Hukusikia ushauri wa wakubwa ona sasa mpige talaka huyo mme.
 
Hun kama sijakuelewa vizuri nisahihishe!
-mlifunga ndoa ili mpate visa au ili mpate kuishi pamoja kama mke na mume japo ni dini tofauti?
-miaka 7 umeishi na mwanaume amabye hakutaki tena au we ndo humtaki tena?
-zaidi ya kuona hataki mfunge ndoa kwa imani ya mmoja wenu huyo mumeo ana shida gani nyingine?
-mambo ya maendeleo mliyoshirikiana mlishirikiana kama mke na mume sio?sasa huoni kama unataka kuachana nae ukijaribu kusema hakuwa mumeo utakuwa umejikosesha haki zako za kimsingi?
-zipo taratibu za kufuatwa kama unataka kutalikiwa that means hicho cheti kinatumika,sasa kama hutaki kitumike hizo taratibu zitafuatwa vipi?
hebu tuweke sawa hapa tukusaidie!

snowhite naomba nikujibu kama ifuatavyo;

- ili tupate visa
- kwa huko nje tuliishi pamoja, kwa hapa kwetu bongo kila mmoja anaishi kivyake,mimi bado niko kwa wazazi.mimi ndo simtaki tena
-yeye hana tatizo la dini hata kubadili dini anaweza ila ndugu zake ndo hawataki yeye afunge bomani.shida aliyonayo ni kunipiga, hajali hisia zangu, hampendi mama yangu ana kazi ya kumtumia msg na kumwambia yeye ndo kasababisha mimi nimwache,ni selfish - kwao kukiwa na shida tutatue ila kwangu kukiwa na tatizo anapotezea nk nk nk
-tulishirikiana kama wapenzi
-ni taratibu zipi nifwate na ndugu wasijue?maana hakuna anayejua sisi tulifunga ndoa na ndo mana kila mmoja anaishi kivyake
 
Huyo ni mume wako wa ndoa na unatakiwa uheshimu hilo,kama mna tofauti basi zimalizeni na muendelee na maisha.

Inaonekana mapenzi yako yote yapo kwenye ndoa ambayo unataka kila mtu ajue bila kujali unaishije na mwenza wako,maisha ni mapambano na kila mtu anapambana kivyake,wote humu tunayo matatizo na tunajaribu kuyasolve kulingana na maisha yetu yalivyo hivyo suala la kuachana si suluhisho la matatizo yako bali angalia chanzo cha tatizo.

Kumbuka ndoa ni ya watu wawili na kama mlifunga basi ndio ndoa yenu.
 
okaay,ni hivi.ile ndoa tulifunga kwasababu tu ya mambo ya visa na vitu kama hivyo tutakapofika huko nje,na ilibaki kuwa siri yangu na yake tu.hakuna mtu anayetuhusu anajua.

Kila mtu anaishi kivyake, na hatuna watoto.kila mtu ana kazi yake ila mambo ya maendeleo tunashirikiana.

unatuchanganya sana mama hapo mwanzo ulisema mlikuwa mnapendana sana tatizo lililozuia ndoa lilikuwa dini . baadae mkakubariana na mwezako mwende nje na mkfunga ndo ya bomani mpaka hapo inaonyesha ulikuwa mke wake halali. sasa inakuwaje unasema kila mtu anaishi kivyake kuna sehemu ya mkanda umeruka.
 
labda sijaeleweka vizuri.hiyo ndoa ya bomani tuliifungia hapa nyumbani na tukaenda nje na international marriage certificate.na makusudi yalikuwa ili ituwie sisi rahisi kupata visa na si vinginevyo.makubaliano yalikuwa hapo baadae tutakuja kufunga ndo ya ukweli sasa tupate na baraka kutoka kwa wazazi.
 
snowhite naomba nikujibu kama ifuatavyo;

- ili tupate visa
- kwa huko nje tuliishi pamoja, kwa hapa kwetu bongo kila mmoja anaishi kivyake,mimi bado niko kwa wazazi.mimi ndo simtaki tena
-yeye hana tatizo la dini hata kubadili dini anaweza ila ndugu zake ndo hawataki yeye afunge bomani.shida aliyonayo ni kunipiga, hajali hisia zangu, hampendi mama yangu ana kazi ya kumtumia msg na kumwambia yeye ndo kasababisha mimi nimwache,ni selfish - kwao kukiwa na shida tutatue ila kwangu kukiwa na tatizo anapotezea nk nk nk
-tulishirikiana kama wapenzi
-ni taratibu zipi nifwate na ndugu wasijue?maana hakuna anayejua sisi tulifunga ndoa na ndo mana kila mmoja anaishi kivyake

Nimesomaa huu uzi sasa ndo kwa mbaali napata picha, kumbe ulienda nje kupitia mgogo wake a.k.a ndoa ya makaratasi!!!!! Ha ha haaaa, jamaa lazima awe na hasira na wewe tu, hata hajakufaidi vizuri unataka kusepa.... hicho choo ulichoingia ni cha wachawi, kaa tayari kurogwa mrembo....:focus: Kama umechoshwa nae dai talaka mahakamani, hakuna shortcut hapo, uko ndani ya ndoa kwa mujibu wa sheria, pole sana!!!!
 
  • Thanks
Reactions: Hun
Hamja totoa hata kinda kimoja? kama vipo navyo viangalia kwa wakambo noomaa!
 
labda sijaeleweka vizuri.hiyo ndoa ya bomani tuliifungia hapa nyumbani na tukaenda nje na international marriage certificate.na makusudi yalikuwa ili ituwie sisi rahisi kupata visa na si vinginevyo.makubaliano yalikuwa hapo baadae tutakuja kufunga ndo ya ukweli sasa tupate na baraka kutoka kwa wazazi.

kwa hiyo inamaana baada ya kufika huko majuu hamjawahi kufanya mapenzi ila mnasubili ndoa yenye baraka kutoka kwa wazazi?
 
Pole bi dada, nakumbuka umesema kuna rafiki aliyewashauri mfunge ndoa kwa bomani,
sasa basi ushawahi kumweleza hayo matatizo maana huenda ni jamaa ake wa karibu aweza zungumza nae
mkasolve hilo tatizo.
 
  • Thanks
Reactions: Hun
Back
Top Bottom