Nimeingia choo cha kike .........! (3)

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Nikiwa ktk hali ya sintofahamu, ghafla nilistuliwa na mlio wa gari nyuma yangu. Iddy Mtimkavu alishuka kwa kasi kwenye land cruiser DFP mali ya ofisi akanifuata kwa kasi. Dereva huyu alinizoea sana maana mara nyingi nilikuwa nasafiri naye kwenye safari zangu za kitafiti huko vijijini. “Chief salama?” Alinisalimia kwa furaha. ‘Kiasi”. Nilimjibu kwa utulivu. “Kulikoni?” Aliuliza kwa mshangao “Au ni verossa?” aliongeza. “Exactly. You are right; imenitenda.” Niliropoka. Na nina haraka within five minutes natakiwa kuwa sehemu!” “Usijali ngoja nikuwahishe. … .” Sikumsubiri amalizie sentensi, niliruka kwenye siti ya mbele kushoto na kumuamuru kuondoa gari kwa kasi.
Ilituchukua dakika sita tu kufika Sweet Easy. Nilishuka kwa kasi kuelekea ndani lakini kabla sijafikisha hata hatua tatu sms iliingia. “Nimetoka, kama nilivyokwambia nina haraka, nitafute jioni saa moja Brajec Pub, Mwenge Mlalakuwa” . Sikuwa na ujanja, mbio na juhudi zangu ziliishia hapo.

Kumi na mbili unusu nilikuwa Brajec Pub. Sikuwa mwenyeji sana wa eneo hili, ila ili kutokutaka kuaibika niliamua kuwahi kuyazoea mazingira yote kwa ujumla na kujenga confidence. Nusu saa baadaye Angel aliingia. Kwa mara nyingine tena, moyo ulinilipuka. Sikuwahi kukumbwa na hii hali ktk maisha yangu hapo kabla, ila nilishangaa kwa haya yaliyonikuta. Nilinyanyuka kwa haraka kumfuata na kumpokea ….

“Anajuwa kukeep time” Nilimchokoza. “Yeah nafahamu kuwa wakati ni mali, zamani watu hawakujali muda ila kwa sasa muda unaheshima yake” Ni kweli nilijibu huku nikijapanga vzr. Utapendelea nini … Nilimuuliza huku nikimuuita mhudumu kwa ishara. Kwa haraka mhudumu alimhudumia na kuondoka.

Tulianza kwa porojo za hapa na pale kutafuta kasi ya mazungumzo na mwishowe lengo la kukutana likafikia. “Nimefurahi sana kupata nafasi hii, nimekuwa nikiitafuta kwa muda mrefu” Nilianza. “Mhhh, muda mrefu? nini kilikuzuia usiongee name wakati kila siku tunaonana ofisini?” Aliuliza. “nafikiri ni wakati wake ulikuwa haujafika, ila sasa naona umefika” Nilimjibu. “Kama niivyokwambia, nisingependa kuwa muongo au pengine kudanganyana kama watoto wadogo wanavyofanya wanapokutana …, mimi ni muwazi sana Angel … Kwa kifupi ninakupenda sana na pia ….” “Ehhee jamani kuniita siku moja tu tayari umenipenda?” Alihamaki. “Hapana, kama nilivyosema hapo awali, nafikiri wakati ulikuwa haujafika, na sasa ndiyo umefika.” Nilimjibu kwa utulivu. “Mhhh, haya una maanisha nini?” “Umewahi kuona mtoto anazaliwa halafu bila kutambaa anarukia kukimbia?” Nilimuuliza. “Hapana” alijibu. Sasa ninachomaanisha stage ya kutambaa, kujifunza kuinuka na kutembea zote tunaziruka …. I mean tunakimbila kwenye ndoa moja kwa moja bila urafiki wala uchumba!” “Mhh hii sijapata kusikia” Alijibu. “ndiyo hivyo nilivyoamua”. “Sikiliza HP usitake kunishangaza, ina maana huna mtu kwa umri huu?” “Sina sababu ya kukuficha, niliwahi kuwa naye ila yalinikuta ni makubwa, nafikiri nitakusimulia vzr zaidi siku nyingine. Leo nilihitaji kumaliza mazungumzo na wewe.” “Siamini!”. “Ni lazima uamini Angel, mimi si kama hao, sijaja kuutesa wala kuumiza moyo wako, niko kwa ajili ya kukuburudisha na kukufanya uione dunia hii kuwa ni paradiso! Niamini mamaaa, mimi si fisadi wa mapenzi” nililalama. “Oh noo nyie ni waongo sana, wanaume wa siku hizi wote maneno yenu ni yale yale” “Siyo wote, tupo wachache wakweli ….niamini” nilijibu. “Ngoja nikwambie, huna haja ya kusema mengi ……. Mimi ninakufahamu vzr HP pengine kuliko hata unavyofikiria ….. ila acha nikueleze ukweli, mwenzio nina mtu siku nyingi!”

Kauli yake hiyo, kwangu ilikuwa kama mkuki moyoni. Kwa jinsi nilivyomfahamu na mwenendo wake kazini, sikuweza kuamini kama alikuwa na mtu. Nilijaribu kutafakari kwa kina sana hiyo kauli yake na kujikuta nimeropoka “ Are you siriaz?” “Kabisa HP, sipendi kukupotezea muda, ila nakuheshimu sana na nisingependa kukutesa” Alisisitiza kuwa ana mtu, tena wa muda mrefu na asingependa kumkwaza. Ongea yake haikuonyesha upinzani wa kunikataa kama ningemng’ang’ani, ila kulikuwa na ukweli Fulani ndani ya sura yake uliogusa moyo na hisia zake kila alipotamka habari za kuwa na mtu! Nilifahamu maana yake nini kutendwa, na kamwe nisingependa mimi mwenyewe kutendewa wala kumtenda mtu kwa namna hii. Uchungu wa kutendwa niliufahamu vizuri sana, na nilihisi harafu ya mateso yake ikinizunguka. Kwa takriban dakika mbili nilijiinamia chini nikitafakari nini cha kukufanya. Nilifahamu ningeweza kutumia techniques nyingi tu za kumnasa, lakini nilijaribu kumfikiria na huyo aliyemtaja …. Nafsi yangu ilinisuta sana …. Nikakukukmbuka usemi wa babu, “asiyekubali kushindwa si mshindani “ ….. Nikafikia uamuzi, naam ni uamuzi mzito…. Pamoja na kila sifa aliyonayo, niliona ni bora niachie ngazi! “Hapana, hapana HP, hapana aiseee, inawezekana ni mtego na pia kumbuka kuwa wanawake walio wengi wakifuatwa siku ya kwanza huwa wanakataa. Ni kitu cha kawaida kukupotezea, usikate tamaa, mpe muda” Nilihisi kitu kikizungumza ndani ya masikio yangu.


********** Itaendelea, mkono umechoka ku-type ***************
 
Hiyo ni sawa na unataka kupiz afu unasukumwa kifuani mbona utatamani ulie, hebu malizia part2 yake haraka bwana kubwa.
 
duh pole sana maana haraka haraka nayo ina matatizo
 
Dah,kumbe napenda story hivi!Mkuu ukishindwa malizia mi ntaiungia!teh teh teh!
 
ukianza sentensi ya kwanza tu, mwanamke huwa tayari anajua unaelekea wapi...sasa sijui nyimbo ndefu hivyo huwa zinakuwa za nini...
 
ukianza sentensi ya kwanza tu, mwanamke huwa tayari anajua unaelekea wapi...sasa sijui nyimbo ndefu hivyo huwa zinakuwa za nini...
Sio sentesi,ukimwambia tu muonane sehemu faragha kwa mazungumzo anakuwa tayari ameshagundua mchezo mzima!Hivi sijui kwanini wanaume wengi mpaka wanazeeka lakini hawajui kupiga sound!Kha!
 
Siku nyingi sijasoma story kama hizi, umeitoa kama tamthiliya za kifilipino ukimaliza episode unatamani nyingine ifuate pale pale. !!!!!
 
Hata mimi nimechoka kusoma ila sijapenda iishe! afadhali ulinipa break. . tuendelee sasa.
 
Back
Top Bottom