toto zuli
JF-Expert Member
- Aug 20, 2012
- 265
- 278
Awali ya yote napenda niwatakie heri ya mwaka mpya wapedwa wote na wana jf wote .
Kwa kweli ndugu zangu nimeingia mwaka 2018 nikiwa na majonzi ya baba yangu mzazi ambaye kwa sasa amekimbia familia yetu na kwenda kuishi na mwanamke na kumuacha mama na wadogo zangu tukiwa na majonzi sana.
Kiukweli hii hali hatukuizoea na miaka yote tulikuwa kila mwaka tunasherekea pamoja sasa hivi hayupo tena nyumbani anaishi sehemu nyingine.
Kilichotokea ni kwamba baada ya kustaafu kazi akiwa ni mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda flani cha saruji hapa mjini kipindi cha december kilichotokea ni kwamba baada ya kupokea mafao yake baada ya siku mbili alikimbia familia yetu na kwenda kuishi na kuanzisha maisha na mwanamke mwingine baada kupata pesa zake za NSSF .
kiukweli hili jambo linaniuma sana mpka limenifanya nimchukie sana baba yangu na kumlaani uko alipo .
Nakumbuka kabla ya kustaafu aliwahi kutuita watoto wake na kutuuliza kila mmoja aseme ni kitu gani anachokitaka kila mtu akazungumza ya kwake.
Lakini kilichokuja kutokea ni mzee kuikimbia familia na kuanzisha maisha mengine kiukweli hadi sasa napitia magumu sana.
Naombeni ushauli kipindi hiki roho inaniuma sana nimeingia mwaka mpya lakini bado nina majonzi ya mwaka jana