Nimeikumbuka hii pasi jamani nzuri.........

Nimeikumbuka hii pasi jamani nzuri.........

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,955
546816_308881835894776_1482015291_n.jpg
 
...hiki kitu tatizo lake ilikuwa haina vipimo,nakumbuka enzi zile za mwalim iliniunguziaga suruali yangu ya mchele mchele...


hahaha suruali ya mchele mchele jamani tumetoka mbali lakini kipindi kile tulikuwa vizuri kwa sasa vyote chinese
 
Kakangu Kaizer aunguziwe sarawili yake ya mchelemchele na shati la tonela, pangechimbika aisee! Pole. Unapasia kwenye gazeti kwanza.
...hiki kitu tatizo lake ilikuwa haina vipimo,nakumbuka enzi zile za mwalim iliniunguziaga suruali yangu ya mchele mchele...
 
Last edited by a moderator:

MziziMkzvu,Ah! utaniliza bana! yani enzi hizo sina majukumu kabisaaa! mi nikiamka nauliza tu,"mama tayari?" naambiwa ndio,najongea mezeni nalamba tea,nawahi skonga, nimeshanyoosha shati langu mpaka ule upanga unauwezo wa kumgawa inzi vipande viwili! j,pili jioni nawahi "Boogie disco" ah jamaniee!
 
Last edited by a moderator:
Ukipasi dk tano unatoka nje kupepea na kupuliza aisee. Ulikuwa mvivu. Jivu kama lina moto unapata kitobo.
nakumbuka ilinichafulia shati langu jeupe la shule kwa jivu lililotokea kwenye matundu yapembeni nikasusa kwenda shule
 
Ili kupunguza moto ilikua unadumbukiza kwenye beseni la maji. By the time unamaliza kupasi maji yanakua yamotooooo moja kwa moja bafuni.....two in one ya ukweeeee
 
Watu tunatofautiana. Wakati wengine hii makitu mmeiweka chumba ya makumbusho ,mi nimetoka kuitumia sasa hivi.Hiyo pasi ya umeme ya nini huku kwetu mbwinde,zilikopita nguzo za umeme zikiwapelekea nishati watanzania.Saloon yetu chini ya mbuyu,kitu ya topaz,full sterile no contamination.Unalipia 200 uko smart.
 
Back
Top Bottom