Nimeikubali ACT, sinilaumu bilashi

Nimeikubali ACT, sinilaumu bilashi

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286

007.JPG

Fikiri upime sana, sinilaumu bilashi,
Fikiri pasi sonona, uwe bora mtumishi,
Fikiri na tulizana, katu usiende joshi,
Fikiri hafidhina, njia zako hazitoshi.

Fikiri upate jua, sikia we mkundaji,
Fikiri waja gundua, dunia yote si maji,
Fikiri waja tambua, taifa lakuhitaji,
Fikiri waja ng'amua, barafu pia ni maji.

Rauka raia mwema, uvivu si jambo jema,
Rauka hima hima, chombo chaenda mrama,
Rauka ewe mjima, konde limejaa kima,
Rauka acha koroma, kujenga nchi lazima.

Rauka jionee, nchi ilivyozizima,
Rauka utembee, uone tulipo kwama,
Rauka jijengee, ule mji wa waroma.
Rauka ujiombee, kwa mola wetu Karima.

Tazama kule angani, nambie waona nini?
Tazama tena angani, pana nyota si utani,
Tazama ACT angani, nyota ya matumaini,
Tazama nyota angani, pigo la nyoka nchini.

Tazama upate jua, CCM ni shetani,
Tazama utagundua, pepo hatoi shetani,
Tazama waja ng'amua, mapepo yapo kazini,
Tazama waja tambua, ACT ni tumaini.

Wino wa zafarani,Umeisha si utani,
Ya manjano zafarani, hamna tone chupani,
Kuandika natamani, wino sinao jamani,
Loo!!! niko tamatini,wana jamvi kwahereni

Njano5.
0784845394.
 
Nchi yetu haitakombolewa na wingi wa vyama vya siasa,ni uroho wenu wa madaraka,siasa na umarufu vinawasumbua tu.Wapinzani wote mnapaswa kujiunga pamoja ili mtengeneze cabinet imara ya kuking'oa ccm kama kweli mna nia ya kutukomboa,tatizo mnawaza RUZUKU na MISAADA mwisho vyama vitazidi idadi ya watanzania.Hivi hamuoni jinsi wananchi wanavyowapotezea?wapiga kura ni wengi kuliko wanavyama,hapo hampaoni?
 
View attachment 146559

Fikiri upime sana, sinilaumu bilashi,
Fikiri pasi sonona, uwe bora mtumishi,
Fikiri na tulizana, katu usiende joshi,
Fikiri hafidhina, njia zako hazitoshi.

Fikiri upate jua, sikia we kuku maji,
Fikiri waja gundua, dunia yote si maji,
Fikiri waja tambua, taifa lakuhitaji,
Fikiri waja ng'amua, barafu pia ni maji.

Rauka raia mwema, uvivu si jambo jema,
Rauka hima hima, chombo chaenda mrama,
Rauka ewe mjima, konde limejaa kima,
Rauka acha koroma, kujenga nchi lazima.

Rauka jionee, nchi ilivyozizima,
Rauka utembee, uone tulipo kwama,
Rauka jijengee, ule mji wa waroma.
Rauka ujiombee, kwa mola wetu Karima.

Tazama kule angani, nambie waona nini?
Tazama tena angani, pana nyota si utani,
Tazama ACT angani, nyota ya matumaini,
Tazama nyota angani, pigo la nyoka nchini.

Tazama upate jua, CCM ni shetani,
Tazama utagundua, pepo hatoi shetani,
Tazama waja ng'amua, mapepo yapo kazini,
Tazama waja tambua, ACT ni tumaini.

Wino wa zafarani,Umeisha si utani,
Ya manjano zafarani, hamna tone chupani,
Kuandika natamani, wino sinao jamani,
Loo!!! niko tamatini,wana jamvi kwahereni

Njano5.
0784845394.

utajitahidi sana kukipigia debe chama CHAMA CHENU CHA KIISLAM lakini hakita kuja kuwa na mvuto kamwe!! Tangia lini msaliti akawa na mvuto kwa jamii??then waambie wenzio wangeweka na mwezi kabisa hapo kwenye bendera ,nyota peke yake haitoshi.BIG NO!! TO ISLAMIC PART 'ACT'
 
Tutolee uchafu wako hapa,watu tunaumiza kichwa baada ya matumaini yetu ya tanzania tuitakayo kupitia katiba kufifia wewe unakuja na upuuzi wako?kama ni mavyama tz yapo zaidi ya 20 hivyo usitujazie topics kwa kutuletea mavyama uchwara ambayo hata hivyo bado yameandikwa kwa wino wa penseli kwa msajiri wa vyama vya siasa.
 
Ebu ondoa ugoro wako apa unatuchafulia jukwaa tu, upuuzi mtupu sijui na uchovu wa kushindia na kulalia mataputapu au ni njaa tu inakusumbua, peleka ujinga huu mwandiga misikitini
 
unaangaika na nini?? wewe huu muda unotumia ugeliwekeza kwenye kilimo ungekuwa mbali sana kiuchumi, nakupa ushauri wa bure hauwezi fanikiwa na hilo lichama lako, ambalo limeanzishwa kwa maelekezo toka lumumba,
 
utajitahidi sana kukipigia debe chama chama chenu cha kiislam lakini hakita kuja kuwa na mvuto kamwe!! Tangia lini msaliti akawa na mvuto kwa jamii??then waambie wenzio wangeweka na mwezi kabisa hapo kwenye bendera ,nyota peke yake haitoshi.big no!! To islamic part 'act'
kwa hiyo mwenyekiti lucas, katibu samson, misingi usawa uwazi, uwajibikaji na demokrasia ya kweli, halafu conclusion ni chama cha kiislam? Halafu wewe unajinasibisha na chama fulani ukiambiwa wewe na chama chako mnabagua na mna chuki na dini fulani utalalamika?
 
kama lema na dr.slaaa???
mkuu usikubali kuingia kwenye mtego wa matusi.hata ukitukanwa; wewe jitahidi kujikita kwenye mambo unayodhani ni ya msingi.na wewe ukianza matusi, itakuwa inaturudisha kule kule.jiepushe sana kuingia kwenye mtego huo.
 
utajitahidi sana kukipigia debe chama CHAMA CHENU CHA KIISLAM lakini hakita kuja kuwa na mvuto kamwe!! Tangia lini msaliti akawa na mvuto kwa jamii??then waambie wenzio wangeweka na mwezi kabisa hapo kwenye bendera ,nyota peke yake haitoshi.BIG NO!! TO ISLAMIC PART 'ACT'

Mbona chadema hamjaweka msalaba! chama cha Mapadri na Wachungaji, chalii mwisho wa ubaya ni aibu.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
utajitahidi sana kukipigia debe chama CHAMA CHENU CHA KIISLAM lakini hakita kuja kuwa na mvuto kamwe!! Tangia lini msaliti akawa na mvuto kwa jamii??then waambie wenzio wangeweka na mwezi kabisa hapo kwenye bendera ,nyota peke yake haitoshi.BIG NO!! TO ISLAMIC PART 'ACT'

mkuu hata kigoma wenyewe wameshawashtukia gea waliongilia ni ya ukabila na udini baadala ya kupigana dudu ccm wao wanataka kupambana na cdm.poor act(agriculture council of tanzani)
 
mkuu usikubali kuingia kwenye mtego wa matusi.hata ukitukanwa; wewe jitahidi kujikita kwenye mambo unayodhani ni ya msingi.na wewe ukianza matusi, itakuwa inaturudisha kule kule.jiepushe sana kuingia kwenye mtego huo.

mkuu unanifurahisha sana na hoja zako.
 
mkuu usikubali kuingia kwenye mtego wa matusi.hata ukitukanwa; wewe jitahidi kujikita kwenye mambo unayodhani ni ya msingi.na wewe ukianza matusi, itakuwa inaturudisha kule kule.jiepushe sana kuingia kwenye mtego huo.

asante sana,,,nimetegeka,,,lengo wanitoe kwenye mstari,,,hili halitatokea tena,,,mungu akubariki.
 
Tutolee uchafu wako hapa,watu tunaumiza kichwa baada ya matumaini yetu ya tanzania tuitakayo kupitia katiba kufifia wewe unakuja na upuuzi wako?kama ni mavyama tz yapo zaidi ya 20 hivyo usitujazie topics kwa kutuletea mavyama uchwara ambayo hata hivyo bado yameandikwa kwa wino wa penseli kwa msajiri wa vyama vya siasa.

Ndugu sasa dharau za nini hapa??? ina maana kuanzisha chama mwiko?? mbona watz tuna ---- za ajabu???
 
ACT-TANZANIA
Mwanzailishi/Waanzilishi wa chama chenu ni nani, kwa sera yenu ya uwazi kwanini mnashindwa jambo dogo la kutuambia chama chenu wasisi ni akina nani,
Je unatuakikishia vipi kwenye cash flow ya chama imtaweka wazi kama mmeshindwa jambo dogo namna hii
 
Ndugu sasa dharau za nini hapa??? ina maana kuanzisha chama mwiko?? mbona watz tuna ---- za ajabu???

wanakutukana kwasababu unaleta pumba
  1. watu wanapambana kutoa nchi kwenye mikataba mibovu, wewe unapigania ubunge wa Zitto
  2. watu wanatafuta kuitoa taifa kwenye ufisadi uliopindukia, nyie mnatafuta kuwa mwenyekiti wa chadema
  3. watu wanapambana na katiba mpya , wewe unaleta mashairi yaliyojaa kejeli
  4. watu wapanda uzalendo kwa watanzania wewe unaleta udini

kwa mambo hayo lazima wakutukane

ushauri wangu kwako Pambana na CCM na sio Chadema hiyo kazi CCM wameshinda who are you to win this war ........................we need changes and not chama

if you think you need to be transparency that is not the right track for you because mpaka sasa washashindwa kutoa jina la founder

hicho sio chama cha majambazi, sio genge la wauni, sio wauza unga , watanzania tunahitaji kuwajua waanzilishi wa chama chenui this is how transparency start
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom