logician mkuu
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 792
- 221
Hapa ni baadhi ya mashairi ya ACT Tanzania kwa walioboreka mnaweza pata burudani.
ACT Tanzania tumekuja na namna mpya ya kujenga chama chetu kwa mashairi....
Chama cha wenye akili kubwa waliokimbia kuongozwa na akili ndogo..
Tuna mpango wa kuandika kitabu cha mashairi
ACT Tanzania tumekuja na namna mpya ya kujenga chama chetu kwa mashairi....
Chama cha wenye akili kubwa waliokimbia kuongozwa na akili ndogo..
NYARAKA ZA SIRI(JIBU)
Nimeketi nafikiri, rasi imejichokea,
Kuisaka tafasiri, alotaka Zephania,
Yupi aliye safiri, jibu kujitafutia,
Yupo kijana mahiri, kivuliche kukimbia?
Yano taka tafakuri,wazee kuwatupia?
Wazee kuwatupia,yano taka taamuli?
Vijana twajiendea,rasini tuna kufuli?
Ewe Bwana Zephania,omba radhi tafadhali,
Jua umetukosea,vijana kila mahali,
Wazee kuwatupia, kila kitu sikubali.
Kila kitu sikubali,na ubishi si fahari,
Kwa ruhusa ya Jalali, nina anza tafakari,
Nimeiwasha kandili, kuisaka hino siri,
Ili nichaji akili,vema nishibe futari,
Kisha ndio nijadili, neno nyaraka za siri.
Neno nyaraka za siri, habari za kilingeni,
Inapofanywa sihiri,nguo huwekwa pembeni,
Mwenye kuitaka siri, avue nguo jamani,
Ndipo apate habari, za wachawi kilingeni,
Neno nyaraka za siri, si neno la hadharani.
Si neno la hadharani, kama mtungi na kata,
Kuna vingi mtungini, avijuaye ni kata,
Wataka yalo mtungini? livae joho la kata,
Ila yataka makini,kuvaa joho la kata,
Siri ni kisu ghalani, tazama kitakukata.
Tazama kitakukata, kijana nakuambia,
Ruyagwa yali mkuta, kilinge kukivamia,
Aliuruka ukuta,wachawi kuwagumia,
Kishindo kikampata, sasa ameshaumia,
Wachawi ukiwakuta,vua nguo nausia.
Vua nguo nausia,kama hutaki mashaka,
Nguo ukijivalia, ya Kabwe yatakufika,
Tena ukisimulia, ka Wangwe utadondoka,
Wanga wamejiapia, ya kwao kuyafutika,
Katu hawataridhia, mdoya kunusurika.
Mdoya kunusurika, kitu hatari kwa siri,
Yapo yanayofanyika, kulinda mambo ya siri,
Waja wana tajirika, kwapani wako na siri,
Serikali, mashirika, wameifuta hanjari,
Kiapo wamekishika, kutunza mambo ya siri.
Kutunza mambo ya siri,kuna taka tahadhari,
Kulinda mambo yasiri, kuna taka tadbiri,
Kufanya jambo ni siri, kuna taka tabasuri,
Wazo la kutoa siri,lahitaji tafakuri,
Ghalibu mtoa siri,huinunua hatari.
Huinunua hatari, kwa wenye nyaraka zao,
Hizo nyaraka za siri, hazipo kwa mitandao,
Ikivujishwa kwa siri, na wenye nyaraka zao,
Haiwezi kuwa siri,bali huwa hila zao,
Ile nyaraka ya siri, wahafidhina hila yao.
Wahafidhina hila yao, kumshukia mwenzao,
Kimegeuka kibao, zimekwisha hila zao,
Hawataki jina lao, chazama kihori chao,
Kata tatu ndio zao, hilo ndio pato lao,
Walimfanyia mwao, sasa imekula kwao.
Sasa imekula kwao, wasaka pakutokea,
Huu ni mwisho wao, mwenzenu najionea,
Kila usiku uchao, naona wanapotea,
Hata zile ngome zao, naona za chechemea,
Wapi makamanda wao, si wote wamelegea?
Si wote wamelegea, hivi nawasingizia?
CUF yaning'inia, CHADEMA yadidimia,
MAGEUZI yajifia, wote waangamia,
Kuti walo jishikia, siriye nawaibia,
Kavu ninawaambia, shindo mwajalisikia.
Shindo mwajalisikia, kwa mtaka tafasiri,
Jibu limemfikia, hajazima kibatari,
Nimekesha nawambia, jibu kutafakari,
Neno la ndani sikia, neno nyaraka za siri,
Muhali kulisikia, nje ya chumba cha siri.
Nje ya chumba chasiri, pana kufuli jadidi,
Neno nyaraka zasiri, nimelijibu kistadi,
Juma mpeni habari, nishatimiza ahadi,
Hakijazimwa kibatari, Zephania ni shahidi,
Neno nyaraka za siri, beti ya nne mrudi.
REJEA SHAIRI LA INNOCENT ZEPHANIA LA TAREHE 29/05/2014, NIMELIAMBATANISHA HAPO CHINI PAMOJA NA LINKI YAKE.
https://www.facebook.com/innocent.z...81666?comment_id=646228115452549¬if_t=like
NYARAKA ZA SIRI
Tumekosa tafasiri,viunga vya ujanani
Tukaona tusafiri,kutaka ya uzeeni
Tumeshindwa tunakiri,jama tusaidieni
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Tumekesha kufikiri,mengi tukayakabaini
kutimu alfajiri,yakawa tele kichwani
Hatutaki kubashiri,kwani vibaya kudhani
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Tumekuja na futari,ishara kuwathamini
Pia na madaftari,kufanyia tathmini
Nyuso zetu zaashiri,msaada kutamani
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Sisi tumetahayari,kwa mawazo ya kijani
Na sasa tupo tayari, kulihoji kiundani
Tumepiga mstari,fasili yetu mezani
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Tufunzeni kwa hadhari,ndo maana ya makani
Mpitie tahariri,tuwape ya ujanani
Hatujaja kukariri,sisi vijana makini
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Tunapenda bilauri,nje kuonyesha ndani
Kikataa ushauri,mwazua ya ubishani
Tena mwaitoa ari,kujadili kwa amani
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Ima fa Ima washari,tuondoke mashakani
Tumejawa tafakuri,tumeuchoka utani
Tunasema kwa kiburi,katu haiwezekani
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
Twagonga na msumari,kamusi tulobaini
Tutazima kibatari,ndani ya siku sabini
Wachama ago twanyeri,hatutaki ya darini
Neno nyaraka za siri,maana yake ni nini?
© Innocent Zephania.
Leo nimempa jibu kabla ya siku sabini alizotoa, na hilo shairi kwanza juu ndio jibu lenyewe.
Njano5.
0784845394
NAWAOMBA WASHAIRI NA WASWAHILI WAJE HAPA. TUJADILI FANI NA MAUDHUI. SIASA WEKA KANDO.
CCM NI SHETANI, PEPO HUTOA SHETANI?
Fikiri upime sana, sinilaumu bilashi,
Fikiri pasi sonona, uwe bora mtumishi,
Fikiri na tulizana, katu usiende joshi,
Fikiri hafidhina, njia zako hazitoshi.
Fikiri upate jua, sikia we kuku maji,
Fikiri waja gundua, dunia yote si maji,
Fikiri waja tambua, taifa lakuhitaji,
Fikiri waja ng'amua, barafu pia ni maji.
Rauka raia mwema, uvivu si jambo jema,
Rauka hima hima, chombo chaenda mrama,
Rauka ewe mjima, konde limejaa kima,
Rauka acha koroma, kujenga nchi lazima.
Rauka jionee, nchi ilivyozizima,
Rauka utembee, uone tulipo kwama,
Rauka jijengee, ule mji wa waroma.
Rauka ujiombee, kwa mola wetu Karima.
Tazama kule angani, nambie waona nini?
Tazama tena angani, pana nyota si utani,
Tazama ACT angani, nyota ya matumaini,
Tazama nyota angani, pigo la nyoka nchini.
Tazama upate jua, CCM ni shetani,
Tazama utagundua, pepo hatoi shetani,
Tazama waja ng'amua, mapepo yapo kazini,
Tazama waja tambua, ACT ni tumaini.
Wino wa zafarani,Umeisha si utani,
Ya manjano zafarani, hamna tone chupani,
Kuandika natamani, wino sinao jamani,
Loo!!! niko tamatini,wana jamvi kwahereni
Mchungaji Njano5.
0784845394.
View attachment 146559
Fikiri upime sana, sinilaumu bilashi,
Fikiri pasi sonona, uwe bora mtumishi,
Fikiri na tulizana, katu usiende joshi,
Fikiri hafidhina, njia zako hazitoshi.
Fikiri upate jua, sikia we mkundaji,
Fikiri waja gundua, dunia yote si maji,
Fikiri waja tambua, taifa lakuhitaji,
Fikiri waja ng'amua, barafu pia ni maji.
Rauka raia mwema, uvivu si jambo jema,
Rauka hima hima, chombo chaenda mrama,
Rauka ewe mjima, konde limejaa kima,
Rauka acha koroma, kujenga nchi lazima.
Rauka jionee, nchi ilivyozizima,
Rauka utembee, uone tulipo kwama,
Rauka jijengee, ule mji wa waroma.
Rauka ujiombee, kwa mola wetu Karima.
Tazama kule angani, nambie waona nini?
Tazama tena angani, pana nyota si utani,
Tazama ACT angani, nyota ya matumaini,
Tazama nyota angani, pigo la nyoka nchini.
Tazama upate jua, CCM ni shetani,
Tazama utagundua, pepo hatoi shetani,
Tazama waja ng'amua, mapepo yapo kazini,
Tazama waja tambua, ACT ni tumaini.
Wino wa zafarani,Umeisha si utani,
Ya manjano zafarani, hamna tone chupani,
Kuandika natamani, wino sinao jamani,
Loo!!! niko tamatini,wana jamvi kwahereni
Njano5.
0784845394.
RAIS WANGU, SI TETEMESHWI NA KUNI, UTAPAMBANA NA MOTO JIKONI.
View attachment 154155
JWTZ katika maadhimisho ya MUUNGANO
Wakitafuta kiama, kanisa walikimbia,
Vile waja huchutama, stara ikiwakimbia,
CCM wanalalama, hamnazo wajitia.
Chungu kimevuja nyama, mchuzi umebakia,
Mchuzi bila nyama, mlaji apata nini?
Tumbo litajaa sima, bila ladha ulimini,
Ndipo zazuka lawama, sima hino sima gani,
Niitwe maamuma, chungu chetu mtihani.
Mchuzi aweza tosha, bila vitomo chunguni?
Fujo zimewaondosha, hawarudi chunguni?
Vituko vinachokesha, nawambia si utani
Mpishi naye atisha, jeshi kutinga jikoni.
Komba mwana wa nani? atokea pori gani?
Komba huyu komba gani, komba mlala porini,
Ameizua tafrani, na nduguye wa Ismani,
Hali tete ya chunguni, ni zao la uhayawani.
Nyama zirudi chunguni, mchuzi upate kuwa,
Mpishi bange za nini, wakati waaminiwa,
Machafuko kitangani, nani aja laumiwa?
Pakanga i chakulani, mpishi waja zomewa.
Chakula ni muafaka, wa mpishi na mlaji,
Mlaji hato ridhika, kama mchuzi ni maji,
Nani atatosheka, mchuzi uso mkundaji,
Moyoni nasononeka, warejee waendaji.
Sitetemeshwi na kuni, mwaja pambana na moto,
Mnafanya ushindani, ujinga hauna pato,
Msijifanye hamuoni, Fikra zangu zi moto,
UKAWA sasa rudini, au mwangojea wito?
UKAWA muwe makini, msifanye mambo kitoto,
Mbili ya tatu n'nini? sio kigingi kizito?
Kisu hushikwa mpini, enyi viumbe wazito,
Unga kishika nchani, kitakutia mkato.
Nimefikia mwishoni, mjifunze kwa mapito,
Mjue ninasema nini, mjukuu ni majuto,
Vitendo vyenu jamani, nawambia ni mtoto,
Mwatia guu njiani, kama ng'ombe aso kwato.
Mchungaji Njano5.
0784845394
SIASA MJUE NJIA, MAAMUZI KUFIKIA.
SIASA MNYAMA GANI(JIBU)
Nimezama mwituni, kumtafuta mnyama,
Mwenye nguvu duniani, leo na keshokiama,
Atajwa msikitini, kanisani wa msema,
Haliwi jambo mwituni, bila ya huyomnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Naanzia shuleni, watoto wanaposoma,
Wanao soma vyuoni, na shahada za heshima,
Ngumbaru ipo kundini, unyago akina mama,
Elimu yetu nchini, huongozwa na mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Uende hospitalini, na walipo wakulima,
Kwenye sekta ya madini, na kwa wapiga ngoma,
Utalii wa mbugani, na uchezaji wa sinema,
Kote huko tambueni, mratibu ni mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Siasa ndio mnyama, Lutumbo katuambia,
Siasa ni kitu chema, katika yetu dunia,
Siasa njia ya umma, maamuzi kufikia,
Siasa si kama sima, bali maji nawaambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Siasa kitu lazima, katu huwezi kimbia,
Waweza ikacha sima, maji huwezi susia,
Hata ngazi ya boma, siasa waitumia,
Siasa ukiitema, jua umeangamia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Kuna siasa ya chama, kimoja nawaambia,
Kila shauri la umma, chama hujiamulia,
Bunge huwa maamuma, muhuri hushikilia,
Jambo lipite kwa Chama, bunge lalishadidia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Zipoza demokrasia, vyama vingi nawambia,
Mfano za Tanzania, na uingereza pia,
Vyama hushindania, magogoni kuingia,
Rais kwa Tanzania, waziri kwa malikia
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Siasa ndani ya vyama, huko hazikuanzia,
Ilianza toka zama, kabla ya hino dunia,
Furkani nimeisoma, sikuiacha biblia,
Malaika na Karima, pia wanaitumia,
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Siasa za huko ahera, kiongozi ni Jalia,
Huongoza msafara, waja wakafuatia,
Mwenye kufanya harara, jeuri akajitia,
Atakuwa ni asira, wa shetani nawambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Muumba ndio kinara, wa mbinguni nadunia,
Maisha huyachora, na njia hutupangia,
Hupata njema ijara, mwenye kumsujudia,
Hupata kubwa hasara, mwenye kupuuzia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Muumba ndio kinara, wa mbinguni nadunia,
Maisha huyachora, na njia hutupangia,
Hupata njema ijara, mwenye kumsujudia,
Hupata kubwa hasara, mwenye kupuuzia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Nani alipiga kura? Munguwe kumchagua,
Mjibu pasi kufura, kweli mpate ijua,
Hapana si masihara, si punde mtagundua,
Tena sifanye papara, siasa kuchambua.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Siasa za kifalme, mfano za Saudia,
Mwana hasa wa kiume, kiti ndio hukalia,
Koo iloshika kome, dola huishikilia,
Mfalme ndio sime, na pia huwa pazia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Zipo za kidikteta, kama zile za Mobutu,
Wengine panga huzifuta, pia wapo wa mtutu,
Umma wote hufyata, mbele ya miungu watu,
Kila mwenye kutukuta, ni mbwa mbele yachatu.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Dikteta awe katili, mbona mtaumwa sana,
Siombe awe jahili, mtapoteza amana,
Tena akiwa bahili, wananchi hukondeana,
Kiongozi bahaluli, asiaminiwe tena.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Samaki awape nyoka, mkate awape mawe,
Nani kashindwa ondoka, kisa halina mauwe?
Ya msingi wanataka, viongozi waelewe,
Wakichoka kuboboka, watawapopoa mawe.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Dikteta awe rahimu, ndipo mtanufaika,
Rasini awe timamu, na tena mshaurika,
Mtakula keki tamu, mafurushi mtashika,
Tripoli yajilaumu, Gaddafi kudondoka.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
Nikitazama chupani, sioni kitu jamani,
Wino wangu wa thamani, ya manjano zafarani,
Niko mengi rasini, wino umetufitini,
Mwenye nao sinihini, naomba niuzieni
Mmeshindwa nidhamini, kwa kifupi kwaherini.
Njano5
0784845394
Kwa kifupi shairi ni matokeo ya shairi la Abbas Lutumbo alilopost ter 1 ya mwez huu ktk wall yke.
Haku muumba kilema, aka mkosesha mwendo,
Huyo ni Mola Karima, mfalme wa vishindo,
Usijifanye yatima, fungua yako mafundo,
Rauka fanya hima, nyumbani haliji windo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Mwenye kupewa ukwasi, katu hakupendelewa,
Masikini hasiasi, wallahi hakuonewa,
Mitihani ya Qudusi, mola wa majaliwa,
Alichopewa pungusi, chaa hakuruzukiwa.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Rauka wahi kazini, upate yako ijara,
Changamoto za windoni, na zikufanye imara,
Toa simanzi moyoni, tena sifanye harara,
Bosi avimbe kichwani, tuli sipoteze dira.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Ukiri Lutumbo kiri, hebu acha kusonona,
Wazoee waajiri, kama wataka kunona,
Shetwani asikughuri, ingawa dhiki waona,
Subiri kakasubiri, lisilo mwisho hakuna.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Niseme nawaajiri, wenye pembe vichwani,
Wana kifanya kiburi, hawana heri moyoni,
Mbaya hawana habari, shida haina maskani,
Tabu hainatajiri, wala si ya masikini.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Ewe ndugu mwajiriwa, sema na wako moyo,
Jukumu ulilopewa, litimize pasi choyo,
Ridhika na unachopewa, huno wangu mgogoyo,
Rushwa katusi ngekewa, yataka ushinda moyo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
Wote wategemeana, mwajiri na mwajiriwa,
Kubwa kuheshimiana, mwerevu kanielewa,
Pia mkiaminiana, kazi haitachezewa,
Tara mkifanyiana, lengo halitafikiwa,
Riziki ni majaliwa, kuipata si ngekewa.
Njano5.
0784845394
Tuna mpango wa kuandika kitabu cha mashairi