Nimeibiwa pesa kwenye akaunti yangu ya NBC

Nimeibiwa pesa kwenye akaunti yangu ya NBC

Bors wewe umepewa siku hizo. Mimi CRDB walishanifanyia huo umafia wkt nilikuwa na ukata mbaya sana. Winiibia kama miliobi mbili hivi, na rekodi zao zilionyesha kwamba ni kadi yangu ndiyo ilitumika wakt wanasema hivyo transaction ya kwanza ilirekodiwa mm nikiwa angani kwenda SA, na nilipokuwa SA nilifanya Visa payment moja na withdrawal moja wao wakarekodi withdrawal s 4. Ku challenge ile rekodi yao wakasema hiyo ni Visa siyo wao na hii nyingine ni mimi so wao hawawajibiki. Wkt nafuatilia nilikutana na jamaa naye walimpiga 8m kwa njia hiyo hiyo. Toka siku hiyo CRDB nawasikia tu aisee! Pole sana
 
Mkuu pole sana. Ilishatolewa elimu humu jamvini. Kuibiwa hela kwa njia hii huitwa card skimming. Hakuna benki iko salama. Cha msingi ni kuwa makini tu unapotumia ATM card hasa kwa wale mnaopenda ku-swap kwenye manunuzi yenu. Wezi kwa njia hizi sasa hivi ni wengi mno.
Kama staff anahusika pia ni rahisi kumkamata we vuta subira
Hizo 45 days ni kwa sababu uchunguzi utawahusisha mastercard/visa na ndo utaratibu waliowekeana.
Uchunguzi unakuwa rahisi pale inapotokea hela inatoka na cents ama inatoka kuzidi kiwango cha kawaida cha kutoa pesa kwa ATM kwa siku
 
Pole mkuu. Mimi hayo yalinikuta na benki ya KCB. Waliiba pesa yangu kupitia ATM kwenye tawi moja Nairobi, tawi ambalo sikuwahi kwenda hata siku moja na kwa siku ambayo sikuitumia ATM wala kadi kuchukua pesa. Walipofanya uchunguzi wao wakanijibu kwamba the system were not tempered hivyo most likely hiyo pesa niliichukua mwenyewe au kuna mtu nilimpa password yangu.

Nilivyokasirika, siku hiyo hiyo niliifunga hiyo account. Ni hatari zaidi kuunganisha account yako ya benki na simu ya mkononi labda kama huweki hela nyingi kwenye hiyo account. Wengi wamelizwa hata huko NMB.

Tiba
 
Kwa kutumia CRDB simbank nililipia DSTV miezi miwili premium aiseee nilikatwa pesa na wala sikupata iyo huduma ya DSTV huu mwezi wa 4 sasa pia kuna wakati uwa nikicheki salio naambiwa kiwango changu ni kidogo siwezi ku withdraw pesa ila nakuwa na pesa nyingi tu , hii uwa inanipa wasiwasi sana
 
Benki za tanzania sii salama kutunza fedha,usumbufu mwingi,mikopo tabu kupata,hata ukipata riba kubwa tabu tupu
 
Bors wewe umepewa siku hizo. Mimi CRDB walishanifanyia huo umafia wkt nilikuwa na ukata mbaya sana. Winiibia kama miliobi mbili hivi, na rekodi zao zilionyesha kwamba ni kadi yangu ndiyo ilitumika wakt wanasema hivyo transaction ya kwanza ilirekodiwa mm nikiwa angani kwenda SA, na nilipokuwa SA nilifanya Visa payment moja na withdrawal moja wao wakarekodi withdrawal s 4. Ku challenge ile rekodi yao wakasema hiyo ni Visa siyo wao na hii nyingine ni mimi so wao hawawajibiki. Wkt nafuatilia nilikutana na jamaa naye walimpiga 8m kwa njia hiyo hiyo. Toka siku hiyo CRDB nawasikia tu aisee! Pole sana

Hizi bank ni tatizo,kuna jamaa yangu mmoja mwezi wa pili huu unaisha haeajamrudishia hela yake, saiv wanamfuata hadi ofisini kwake mara nyingi na kumueleza hela yake itarudi. Bado sijawa na uhakika ni bank gani ina unafuu.binafsi CRDB watasubiri sana
 
Mkuu pole sana. Ilishatolewa elimu humu jamvini. Kuibiwa hela kwa njia hii huitwa card skimming. Hakuna benki iko salama. Cha msingi ni kuwa makini tu unapotumia ATM card hasa kwa wale mnaopenda ku-swap kwenye manunuzi yenu. Wezi kwa njia hizi sasa hivi ni wengi mno.
Kama staff anahusika pia ni rahisi kumkamata we vuta subira
Hizo 45 days ni kwa sababu uchunguzi utawahusisha mastercard/visa na ndo utaratibu waliowekeana.
Uchunguzi unakuwa rahisi pale inapotokea hela inatoka na cents ama inatoka kuzidi kiwango cha kawaida cha kutoa pesa kwa ATM kwa siku
Mkuu,bank statement inaonyesha pesa yote imetolewa kwenye ATM sio yao
 
Pigana mpaka upewe pesa yako. Wakisha kurudishia, funga hiyo account. Kamwe usifungue account NBC.

Watanznia wote, fungeni account zenu NBC.
Naenda kufunga leo, kila siku nilikuwa na mawazo ya kufunga account huko kwa kuwa siiamini hii benki, leo nitafanya hivyo.
 
Mimi pia leo nimegundua laki 4 haipo kwenye account yangu nakwenda kesho kuulizia
 
mkuu,bank statement inaonyesha pesa yote imetolewa kwenye atm sio yao
itakua ni skimming hio. Na wageni ndo wafanyaji wa hayo. Hujawahi kuskia kuna raia wa kigeni wanakamatwa na kadi mpaka 60? Hao ndo wanotuliza, sasa kama mtu haelewi anabaki kuiambia bank ndo imemuibia. Pole sana mkuu
 
Pole imewahi Nikita hiyo ni balaaa. Yaani siku 45 uchunguzi na baada ya hapo ndo uwekwe kwenye list ya kulipwa so hesabu siku Mbele tens. Hizo ni shida za kadi za master card au visa wanaiba sana sana. Huenda umeibiwa nchi za nje huko wamefanikiwa kunasa namba za kadi
 
Broo wangu kalizwa kama laki nane hivi wiki iliyopita,anawiki sasa katika siku 45 za uchunguzi.pole sana ukipata shukuru.
 
Jmosi 08/11/14 niliangalia salio la akaunti ya NBC kwenye simu yangu na kukuta kimetolewa kiasi kinachofikia Tshs.2,100,000/=. Ilibidi nipige simu kwenye namba yao iliyopo kwenye kadi ya ATM niwaeleze tatizo la akaunti na kuiblock akaunti,wakaniambia niende moja kwa moja nilipofungua akaunti.
Siku ya leo nimeenda nikaomba bank statement,nikaona bank statement inaonyesha nilitoa pesa tarehe 07/11/14 hadi 08/11/14. Change kunishangaza mnamo wa hizo tarehe nilikuwa nimejipumzisha nyumbani peke yangu na mara ya mwisho kutoa pesa ilikuwa tarehe 04/11/14. Nikaipinga bank statement,wakaniuliza maswali yao na kuandika barua ya malalamiko.Wameniambia nikae siku 45 niondoe siku za wikiendi na sikukuu kwa ajili ya uchunguzi.
Nina wasiwasi na wafanyakazi wa benki wenyewe,hamna mtu yeyote anajua kama nina akaunti NBC zaidi ya wenyewe.Kuna mtu yeyote kishamtokea kitu kama hiki?

Kwani siku uliyoshtuka kuwa hela imepungua ulijuaje? na hukupata notification kuwa hela imetolewa, tupe mazingira ya tukio yalivyokuwa ili tusiwe na maswali zaidi.
 
Mie nimekutaa wamedraw elfu 50,000/ na hivi sijaitumia muda mrefu nilichofanya ni kuhamisha visenti vyangu vilivyobaki.
 
Akaunti nimeifunga nasikilizia huo uchunguzi wao hadi utakapokamilika.Ubaya wao NBC ukiweka pesa au kutoa pesa hawakupi taarifa kwa njia ya simu kama benki zingine
watatoaje taarifa wakati wanatengeneza mazingira ya kuwaibia wateja wao?
 
Pole sana............mi mdogo wangu aliibiwa 2.5m stanbic bank na mpaka leo hawajarudisha.
 
Back
Top Bottom