medisonmuta
JF-Expert Member
- Oct 10, 2014
- 2,446
- 1,534
Jmosi 08/11/14 niliangalia salio la akaunti ya NBC kwenye simu yangu na kukuta kimetolewa kiasi kinachofikia Tshs.2,100,000/=. Ilibidi nipige simu kwenye namba yao iliyopo kwenye kadi ya ATM niwaeleze tatizo la akaunti na kuiblock akaunti,wakaniambia niende moja kwa moja nilipofungua akaunti.
Siku ya leo nimeenda nikaomba bank statement,nikaona bank statement inaonyesha nilitoa pesa tarehe 07/11/14 hadi 08/11/14. Change kunishangaza mnamo wa hizo tarehe nilikuwa nimejipumzisha nyumbani peke yangu na mara ya mwisho kutoa pesa ilikuwa tarehe 04/11/14. Nikaipinga bank statement,wakaniuliza maswali yao na kuandika barua ya malalamiko.Wameniambia nikae siku 45 niondoe siku za wikiendi na sikukuu kwa ajili ya uchunguzi.
Nina wasiwasi na wafanyakazi wa benki wenyewe,hamna mtu yeyote anajua kama nina akaunti NBC zaidi ya wenyewe.Kuna mtu yeyote kishamtokea kitu kama hiki?