Nimeharibiwa ndoa na ndugu yangu!!

ABEDNEGO

Senior Member
Aug 20, 2009
109
30
Wajemeni Salaam Aleikum,

Nilisafiri katika kutafuta maisha miaka kama miwili,Na kumwaacha mansapu akiendesha miradi yetu ya hapa home.Nimerudi nimekuta kila kimmoja kimepita njia yake hata watoto wana dalili za kwarkoo.

Kudadisi nikaambiwa ndugu yangu ambaye ni jirani kabisa alikuwa anachakachua mansap kwa kwenda mbele.Mama hatulii home kila kukicha mguu na njia anarudi anapoona,Watoto walale njaa hana habari.

House girl mwenyewe kachoka,Vijana kwenye miradi waliifanya yao na kuchukua walichoona.Sasa mie sina chochote gari niloacha ni mkweche ambao hata kulipiwa road licence tangu nimeondoka.

Sasa kumfukuza nashindwa kwani tuna watoto watatu nae,ndoa ya kanisani,nk Nimfanye nini huyu ndugu yangu ?
 
Mlaumu mkeo ndugu yangu angekuwa anakupenda ni kwa dhiki na Faraja. Hakufai huyo
 
pole sana.....nitarudi baadae kwa ajili ya ushauri....
 
kwa akili zako ulikuwa humfahamu mkeo baba??????????????anghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Hawaminiki hawa wa2 Best! Mrekebishe2! Maana ukisema kumtafuta mwingine ni hasara2.
 
pole sana,jipange upya uanze moja...kama bado unampenda mpime ngoma uendelee naye,ila hakikisha unamchunguza msimamo wake juu ya uhusiano wenu kwanza.....
 
wakati unajiuliza ufanyeje kuhusu sijui nini (kama kulipia mkweche road licence,ama kufufua miradi etc),ni muhimu kupima afya zenu eeh.pole,bt remember advice is what we ask for when we know exactly what we should do bt dont want to.
 
Hii ishu ni ngumu kidogo ila ni vyema ukawa bayana uamuzi wako ni nini kabla hatujatoa wa kwetu...pole sana kaka!
 
Ya nini maluuumbano ya nini manenooo........................................
Jasiri haachi ..................................
 
Pole sana mkuu hayo ni masahibu makubwa sana. Si mwaminifu yeye na hata huyo ndugu yako. Mwenye maamuzi ni wewe kaka, kusuka au kunyoa. Ukiamua kumwacha ewalaaaaaaaa anastahili. ukiamua kusamehe usamehe kweli sio nusunusu, na usahau kabisa ili lisiwe doa moyoni mwako. Ndo Maisha mkuu
 
Kuna jamaa yangu pia alikuwa na tatizo linakaribiana na lako. Yeye alimsamehe mkewe kwa madai kuwa miaka miwili ni mingi na mkewe ni binadamu hivyo alimsaliti baada ya uvumilivu wa kukosa "ile kitu" kumshinda. Mkewe alikiri usaliti, wameanza moja na maisha yanaendelea kama kawaida. Sema walipima afya na miezi mitatu ya kwanza jamaa alikuwa muangalifu sana asijeambukizwa gonjwa na mkewe. Kwa sasa wana mtoto mmoja ana miaka sita na wanaenjoy maisha.

Kaa chini uongee na mkeo ujue msimamo wake, manake hata ukioa mwanamke mwingine haimaanishi hatakusaliti. Unaweza jikuta unaoa kila siku na kuacha mwishowe unachanyikiwa. Nakutakia kila la kheri, pia msisahau kumshirikisha Mungu katika hili.
 
Wajemeni Salaam Aleikum,

Nilisafiri katika kutafuta maisha miaka kama miwili,Na kumwaacha mansapu akiendesha miradi yetu ya hapa home.Nimerudi nimekuta kila kimmoja kimepita njia yake hata watoto wana dalili za kwarkoo.Kudadisi nikaambiwa ndugu yangu ambaye ni jirani kabisa alikuwa anachakachua mansap kwa kwenda mbele.Mama hatulii home kila kukicha mguu na njia anarudi anapoona,Watoto walale njaa hana habari.House girl mwenyewe kachoka,Vijana kwenye miradi waliifanya yao na kuchukua walichoona.Sasa mie sina chochote gari niloacha ni mkweche ambao hata kulipiwa road licence tangu nimeondoka!! Sasa kumfukuza nashindwa kwani tuna watoto watatu nae,ndoa ya kanisani,nk Nimfanye nini huyu ndugu yangu ?

Miaka miwili ya kutengana na familia yako katika kutafuta maisha hukuambulia chochote? maana kwa maelezo yako umerudi ukitegemea vile ulivyoacha, huko ulikokuwa umetoka kapa au na wewe nyumba ndogo ilikangua kila kitu? Ukiwa na majibu chanya ya maswali haya mawili utapata jibu la nini umfanyie mkeo
 
Ongea nae kama anarekebishika muanze upya!!!

Kama hatojirekebisha usitumie watoto ambao hata hawajali kama kigezo cha kubaki nae...atakuletea tu presha kama sio Ukimwi!!!
 
Wajemeni Salaam Aleikum,

Nilisafiri katika kutafuta maisha miaka kama miwili,Na kumwaacha mansapu akiendesha miradi yetu ya hapa home.Nimerudi nimekuta kila kimmoja kimepita njia yake hata watoto wana dalili za kwarkoo.Kudadisi nikaambiwa ndugu yangu ambaye ni jirani kabisa alikuwa anachakachua mansap kwa kwenda mbele.Mama hatulii home kila kukicha mguu na njia anarudi anapoona,Watoto walale njaa hana habari.House girl mwenyewe kachoka,Vijana kwenye miradi waliifanya yao na kuchukua walichoona.Sasa mie sina chochote gari niloacha ni mkweche ambao hata kulipiwa road licence tangu nimeondoka!! Sasa kumfukuza nashindwa kwani tuna watoto watatu nae,ndoa ya kanisani,nk Nimfanye nini huyu ndugu yangu ?

hapo badili dini. Ingia katika dini inayofuata sheria alizoleta Mungu na si dini ya sheria zilizotungwa na watu. otherwise hapo huna cha kufanya mpaka ima afe au ufe wewe ndio biashara zingine zitaendelea. vinginevyo ukioa na bado umeshikilia sheria za watu
 
Wajemeni Salaam Aleikum,

Nilisafiri katika kutafuta maisha miaka kama miwili,Na kumwaacha mansapu akiendesha miradi yetu ya hapa home.Nimerudi nimekuta kila kimmoja kimepita njia yake hata watoto wana dalili za kwarkoo.Kudadisi nikaambiwa ndugu yangu ambaye ni jirani kabisa alikuwa anachakachua mansap kwa kwenda mbele.Mama hatulii home kila kukicha mguu na njia anarudi anapoona,Watoto walale njaa hana habari.House girl mwenyewe kachoka,Vijana kwenye miradi waliifanya yao na kuchukua walichoona.Sasa mie sina chochote gari niloacha ni mkweche ambao hata kulipiwa road licence tangu nimeondoka!! Sasa kumfukuza nashindwa kwani tuna watoto watatu nae,ndoa ya kanisani,nk Nimfanye nini huyu ndugu yangu ?

ndugu yako hana tatizo kabisa na ukikaanae vizuri anaweza kupa siri nzito juu ya mkeo na pengine ukachanganyikiwa zaidi..la maana mkabidhi vyake mpeleke kwa ndugu wake wa karibu kuna hawa jamaa wnaitwa MPESA AAMA TIGO PESA SIJUI ANA LAINI GANI ..KAULIZIE TKT YAA KWENDA KWAO SH NGAPI ONYO BEI ZIMEBADILIKA..USIMTESE KAKATE TKT MTUMIE KA 30 CHA MAZIROZIRO MA TATU KWENYE MPESA USIWASILIANE NAE TENA...
 
Back
Top Bottom