Nimeharibiwa ndoa na ndugu yangu!!

pole sana,jiulize kama bado unampenda mkeo na uko tayari kusamehe aliyofanya ili muanze upya,chunguza kama mkeo ana msimamo gani kuhusu wewe na familia yenu kama anakiri alikosea nayupo tayari kushirikiana na wewe tena mpe nafasi nyengine ila mpime ukimwi kabla hamjaanza kuwa na mahusiano mengine:A S-rose:
 
Kuanza upya si ujinga mjomba nashangaa bado unae na unajishauri kumwacha coz of watoto....????
fanya maamuzi ya kiume kidogo...Hata vitabu vya dini vyote vinaibariki kabisa uamuzi wa kumwaga...
 
Pole mkuu ulioa msichana na siyo mwanamke. Chakufanya mbadilishe awe mwanamke.
 
je huyo mke wako bado ana mapenzi na wewe?miaka 2 sio mingi kwa kutokuonja hiyo kitu.kafanya vibaya mno kutembea na ndugu yako.kiufupi wewe ndio unajua mnavyoishi na mke wako.jamani saa nyengine haijalishi kama ndoa ni ya. kanisani unaweza ukapata furaha kuliko kung'ang'ania ndoa isiyokuwa na furaha.yapo matatizo mnaweza mkayasuluhisha,na yapo matatizo ambayo,utatuliwaji wake ni bora kila mtu aanze maisha yake kivyake,kuliko kufurahisha jamii.mwanzo inauma,baadae unakuwa nafuraha.nina amini wapo wanawake wazuri tu kitabia na wanaume ambao wanajiheshimu na kujali ndoa zao
 
Wajemeni Salaam Aleikum,

Nilisafiri katika kutafuta maisha miaka kama miwili,Na kumwaacha mansapu akiendesha miradi yetu ya hapa home.Nimerudi nimekuta kila kimmoja kimepita njia yake hata watoto wana dalili za kwarkoo.

Kudadisi nikaambiwa ndugu yangu ambaye ni jirani kabisa alikuwa anachakachua mansap kwa kwenda mbele.Mama hatulii home kila kukicha mguu na njia anarudi anapoona,Watoto walale njaa hana habari.

House girl mwenyewe kachoka,Vijana kwenye miradi waliifanya yao na kuchukua walichoona.Sasa mie sina chochote gari niloacha ni mkweche ambao hata kulipiwa road licence tangu nimeondoka.

Sasa kumfukuza nashindwa kwani tuna watoto watatu nae,ndoa ya kanisani,nk Nimfanye nini huyu ndugu yangu ?


Mkuu acha utani wewe....hii fix kwenda mbele...ndoa ya kanisani mwanzoni salamu ya Kiislamu...usitanie kanisa mkuu...tena koma kabisa.
 
Achana nae njoo unioe mimi tulee watoto, mimi ninagari inavibali vyote ntakupa utumie eeeh baba. Ustafute maisha muda mrefu hivyo sawa eeh pole eti eeh.
 
Kwanza kabisa kapime afya yako na yake ili mjue mmesimamia wapi, pili mkalishe chini huyo mke umuulize ilifikia vipi akaamua kufanya hilo. tatu unaweza msamehe ila jiulize mwenyewe unaweza ishi nae na kusahau yaliyopita? As you said mna watoto watatu unajua wazazi mkiachana watoto wanavyoteseka. Ishi nae mpe nafasi ya pili ila ukiona unamshindwa piga chini tu usijilazimishe saaana wakati roho imesha chafuka.
Hivi nashangaa wanawake wenzangu, ni penzi gani linakufanya unashindwa kuangalia watoto wako? hapo kama unashindwa kuangalia wa kwako utaweza mwangalia hata huyo mwanaume unayemkimbilia? na hisi si wewe tu umemchukia hata watoto wamemchukia sana huyu mama.Mi nikiangalia sana huyu mama hakufai kabisa
 
Back
Top Bottom