Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,648
- 75,732
Mimi ni mmoja wa Waafrika wengi tulioguswa na kifo cha Hayati Magufuli. Kusema kweli hakuna kiongozi yeyote aliyepata kufariki kuanzia 2000 aliyepata kunigusa ukimuondoa Magufuli...Gadafi kidogo...
Magufuli alikuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwangu na kwako. Alikuwa kiongozi anayeendana na mahitaji ya Tanzania/Afrika ya wakati huu.
Tanzania/Afrika ya sasa tunahitaji viongozi wathubutu, wanaojali watu wa chini, wanaoelewa Afrika inachohitaji.
Nimefurahi kuona watu wa chini wameguswa saana na kututoka kwake. Ila kwa hapa JF wengi wamefurahi uzuri naelewa kwanini wanafurahia.
Lakini ni hawa hawa watu baada ya miaka miwili tu wataanza kulalama kiongozi aliyepo madarakani hayafanyi aliyokuwa anayafanya Magufuli.
Maendeleo sio jambo jepesi...yanahitaji kujitoa..unapotaka maendeleo unahitaji kupoteza baadhi ya vitu. Hiki ndicho Magufuli alifanya. Aliamua kuminya baadhi ya vitu. Hili sio kwa nchi tu hata maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Naumia saana kuona wengi wanamuita Hayati Magufuli Dikteta , mwizi na hakufanya chochote. Niwaambie tu kuna siku mtamlilia.
Kwaherini nitarudi JF baada ya miaka miwili. 2023.
Mnadhani tutakuja kupata kiongozi mfuata demokrasia ya Ulaya, Atakayejenga miundombinu ya Ulaya na kutupa maisha ya Ulaya ndani ya miaka 5???
Kama kwenye akili zenu mnadhania hivi basi mtakufa bila kumpata....kwaherini.