Nimeguswa sana na maoni ya wanaJF kuhusu kifo cha Hayati Magufuli

Ni sawa kwa mtazamo wako Wala siwezi kukupinga maana ndivyo umeona wewe na ibaki kuwa hivyo haina tatizo, naheshimu sana mtazamo wa mtu.

Na Mimi nina mtazamo mwingine kabisa juu ya JPM na ibaki kuwa hivyo pia.

Hizo hoja zimeshajadiliwa sana humu na haitasaidia kubadili mawazo ya mmoja wetu yoyote.
JPM hakuwa malaika tuseme hakufanya makosa, na bahati mbaya makosa hayo yamekuathiri wewe zaidi.
Bahati nzuri mimi sijaathirika na makosa yake, ndio maana naangalia mambo yake mazuri zaidi ya mabaya.

Mlio umizwa na JPM poleni, ila sisi wengine tutaendelea kumuenzi kwa mazuri aliyoyafanya.
mkuu huo sio mtazamo wangu. Hivyo ndivyo vigezo vya kwamba alijali utu ama lah. Huwezi kufanya kuyaacha hayo halafu ukasemwa ulijali utu. Hata kama angekuwa ananipa mkate na siagi kila asubuhi,kama ameyaacha hayo basi sio mpenda utu. Utu ni kujali watu. Utu hauwezi kuwa compansated na madaraja. haaa haaa
 
Watu wengi wanaolia, kugalagala na kusikitika wako Kwenye TV.

Mtaani huku kila mtu ana mishe zake.

Ishtoshe, usilazimishe kila mtu asikitike.

Hukulia pamoja pamoja na:

Mke wa Azory Gwanda,

Ndugu wa Kanguye,

Ndugu wa Lwajabe,

Wazazi wa Akwilina Akwilina.

Wala hukuwa pamoja na watu wakiotukanwa, kuteswa na kubomolewa nyuma.

Maisha ni two way traffic. Unataka wewe ufurahi siku zote wewe nani ??

Ulifurahi Tundu Lissu alivyovurumishiwa risasi 32 mchana kweupe, leo sikitika na wewe.

Leo unalazimisha kila mtu aomboleze na wewe ??

Binadamu wote ni SAWA.

Hakuna binadamu BORA ZAIDI kuliko binadamu mwingine.

Uhai wa Magu ni SAWA na Akwilina Akwilina au Uhai wa walio okotwa koko beach.

Kila mtu anamhitaji mpendwa wake kama wewe unavyomtaka wa kwako.

Waafrika wengi tunaishi kinafiki, tutalia sana na kusikitika kwenye camera, ila ikiondolewa wenyewe tunapika pilau.

Magu kawaasalimie tu uliowatanguliza.

Kazi ya kutoa uhai ni ya Mungu na haina makosa.
Asijisahaulishe mwamba Palamagamba amewalazimika kutafuta mwitikio wa watu kushangilia uwanjani kwa kuhimiza mara 3.
 
Mimi ni mmoja wa Waafrika wengi tulioguswa na kifo cha Hayati Magufuli. Kusema kweli hakuna kiongozi yeyote aliyepata kufariki kuanzia 2000 aliyepata kunigusa ukimuondoa Magufuli...Gadafi kidogo...

Magufuli alikuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwangu na kwako. Alikuwa kiongozi anayeendana na mahitaji ya Tanzania/Afrika ya wakati huu.

Tanzania/Afrika ya sasa tunahitaji viongozi wathubutu, wanaojali watu wa chini, wanaoelewa Afrika inachohitaji.

Nimefurahi kuona watu wa chini wameguswa saana na kututoka kwake. Ila kwa hapa JF wengi wamefurahi uzuri naelewa kwanini wanafurahia.

Lakini ni hawa hawa watu baada ya miaka miwili tu wataanza kulalama kiongozi aliyepo madarakani hayafanyi aliyokuwa anayafanya Magufuli.

Maendeleo sio jambo jepesi...yanahitaji kujitoa..unapotaka maendeleo unahitaji kupoteza baadhi ya vitu. Hiki ndicho Magufuli alifanya. Aliamua kuminya baadhi ya vitu. Hili sio kwa nchi tu hata maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Naumia saana kuona wengi wanamuita Hayati Magufuli Dikteta , mwizi na hakufanya chochote. Niwaambie tu kuna siku mtamlilia.

Kwaherini nitarudi JF baada ya miaka miwili. 2023.

Mnadhani tutakuja kupata kiongozi mfuata demokrasia ya Ulaya, Atakayejenga miundombinu ya Ulaya na kutupa maisha ya Ulaya ndani ya miaka 5???

Kama kwenye akili zenu mnadhania hivi basi mtakufa bila kumpata....kwaherini.
Daby umenitangulia kuyasema hayo japo nilikwisha kutoa maoni yangu kuhusu uwezo wa Hayati Magufuli.

Nami naungana na wewe kutokuongelea siasa humu JF tena hadi kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025. Sababu kubwa JF imejaa mashabiki na wafuasi wa upinzani ambao hawana jipya zaidi ya kulalamika, kuzua uwongo na unafikk
 
mkuu huo sio mtazamo wangu. Hivyo ndivyo vigezo vya kwamba alijali utu ama lah. Huwezi kufanya kuyaacha hayo halafu ukasemwa ulijali utu. Hata kama angekuwa ananipa mkate na siagi kila asubuhi,kama ameyaacha hayo basi sio mpenda utu. Utu ni kujali watu. Utu hauwezi kuwa compansated na madaraja. haaa haaa
Watu unaowazungumzia ni kina nani? Unayosema ni sawa, hakuwajali baadhi ya watu..na baadhi aliwajali. Sasa iweje ulazimishe alio wajali wamchukie?
Sisi ambao alitujali tuache tusikitike, na nyie ambao mlitendewa vibaya ni haki yenu kumchukia.
Na sasa hayupo tena basi tegemeeni huyu wa sasa hivi atawajali.
 
Basi ili msiwe WANAFIKI mngetulia kwanza.
Ili muone atafanya nini.
Ili baadae msije mkamgeuka na kuonekana wanafiki.
Ila kama samia atawaita NENDENI MKAMSIKILIZE.
Kuna chama kimesema ni rafiki wa Samia zaidi ya CCM wenyewe? Kama ataendeleza ubabe na unyama wa mtangulizi wake atapigwa tu.
 
Pole sana.
1.Hata mtu awe mzuri sana, anatenda mema hawezi kupendwa na kila mtu.
2.Hata mtu awe mbaya sana, anayetenda mabaya, hawezi kuchukiwa na kila mtu.

Nataka kusema hivi, kwenye ulimwengu wa mitandao kuna kila kitu. Unavyopenda kuvisikia na usivyopenda kuvisikia.
Habari nzuri ni kwamba, kila jambo ambalo unalipenda na unatamani kulisikia muda wote kuna mahali utalipata. Sasa wewe unakosea mahali pa kuyapata unayotamani kuyasikia.

Kuna social media platforms ukiisoma au tv channels unaweza kuamini kitu fulani hakipendwi na watu kabisa na kuna ambayo ukisoma/kuangalia utashangaa namna ambavyo hicho kitu kinavopendwa na watu. Kwahiyo ni wewe ujue ni kitu gani unapenda kukisikia na ni wapi ambao utakipata. Wala hautaumia maana hautajua hata kama kuna watu wanamsema vibaya.
Dada kwishaolewa weye? Ujengaji wako hoja huwa unanibariki mno...uishi miaka ya kutosha km mzee Mwinyi
 
RIP JOHN MAGUFULI... Uko sahihi sana brother tunamshukuru magu kwa nafasi yake ametenda mpaka hapa alipofikia..... Ila tumuombee Mama samia awe jasiri sana mabadiliko atayoyafanya wasipo muandama hawa masela wa CCM mama atatufikisha mahali!!!! Wanawake wakiwa kwenye nafasi kubwa ni wazuri kwenye uongozi ila ndo hawapendi strees sasa kwaiyo tumuombee sana Raisi samia.... Pumzika kwa amani Magufuli tunashukuru kwa hapa ulipo tuacha tumejifunza mengi" mimi kama kijana nimejifunza kutokata tamaa na kutokubali kushindwa nikupambana mpaka dakika ya mwisho..
Mimi ni mmoja wa Waafrika wengi tulioguswa na kifo cha Hayati Magufuli. Kusema kweli hakuna kiongozi yeyote aliyepata kufariki kuanzia 2000 aliyepata kunigusa ukimuondoa Magufuli...Gadafi kidogo...

Magufuli alikuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwangu na kwako. Alikuwa kiongozi anayeendana na mahitaji ya Tanzania/Afrika ya wakati huu.

Tanzania/Afrika ya sasa tunahitaji viongozi wathubutu, wanaojali watu wa chini, wanaoelewa Afrika inachohitaji.

Nimefurahi kuona watu wa chini wameguswa saana na kututoka kwake. Ila kwa hapa JF wengi wamefurahi uzuri naelewa kwanini wanafurahia.

Lakini ni hawa hawa watu baada ya miaka miwili tu wataanza kulalama kiongozi aliyepo madarakani hayafanyi aliyokuwa anayafanya Magufuli.

Maendeleo sio jambo jepesi...yanahitaji kujitoa..unapotaka maendeleo unahitaji kupoteza baadhi ya vitu. Hiki ndicho Magufuli alifanya. Aliamua kuminya baadhi ya vitu. Hili sio kwa nchi tu hata maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Naumia saana kuona wengi wanamuita Hayati Magufuli Dikteta , mwizi na hakufanya chochote. Niwaambie tu kuna siku mtamlilia.

Kwaherini nitarudi JF baada ya miaka miwili. 2023.

Mnadhani tutakuja kupata kiongozi mfuata demokrasia ya Ulaya, Atakayejenga miundombinu ya Ulaya na kutupa maisha ya Ulaya ndani ya miaka 5???

Kama kwenye akili zenu mnadhania hivi basi mtakufa bila kumpata....kwaherini.
 
Basi ili msiwe WANAFIKI mngetulia kwanza.
Ili muone atafanya nini.
Ili baadae msije mkamgeuka na kuonekana wanafiki.
Ila kama samia atawaita NENDENI MKAMSIKILIZE.
Wapinzani wako tayari kumsikiliza yeyote. Mbowe akiwa Mwanza 2020 alimwambia Magufuli wapinzani wako tayari kukutana na wewe na kurejesha mshikamano halisi wa nchi yetu uliozoeleka. Binafsi na narudia binafsi naamini Magufuli alikuwa na mazuri mengi, lakini kwangu kasoro kubwa aliyokuwa nayo inamwondolea sifa ya kuwa Rais bora, Ukatili, ubabe, kuamini yeye hakosei na kutojali thamani ya uhai wa Watanzania wenzake.
 
Vizuri .basi kwa sasa muacheni samia.
AAMUE akiona inafaa ataonesha ushirikiano na nyie.
Ni wazi kuna mambo ambayo yalikuwa yanawakera hayawezi kubadilika.
Asaa kipindi cha UCHAGUZI maana ccm na wizi wa kura wana undugu.
Je mtafurahi mkiona hayo si lazma mtamchukia samia?
Wapinzani wako tayari kumsikiliza yeyote. Mbowe akiwa Mwanza 2020 alimwambia Magufuli wapinzani wako tayari kukutana na wewe na kurejesha mshikamano halisi wa nchi yetu uliozoeleka. Binafsi na narudia binafsi naamini Magufuli alikuwa na mazuri mengi, lakini kwangu kasoro kubwa aliyokuwa nayo inamwondolea sifa ya kuwa Rais bora, Ukatili, ubabe, kuamini yeye hakosei na kutojali thamani ya uhai wa Watanzania wenzake.
 
Mimi ni mmoja wa Waafrika wengi tulioguswa na kifo cha Hayati Magufuli. Kusema kweli hakuna kiongozi yeyote aliyepata kufariki kuanzia 2000 aliyepata kunigusa ukimuondoa Magufuli...Gadafi kidogo...

Magufuli alikuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwangu na kwako. Alikuwa kiongozi anayeendana na mahitaji ya Tanzania/Afrika ya wakati huu.

Tanzania/Afrika ya sasa tunahitaji viongozi wathubutu, wanaojali watu wa chini, wanaoelewa Afrika inachohitaji.

Nimefurahi kuona watu wa chini wameguswa saana na kututoka kwake. Ila kwa hapa JF wengi wamefurahi uzuri naelewa kwanini wanafurahia.

Lakini ni hawa hawa watu baada ya miaka miwili tu wataanza kulalama kiongozi aliyepo madarakani hayafanyi aliyokuwa anayafanya Magufuli.

Maendeleo sio jambo jepesi...yanahitaji kujitoa..unapotaka maendeleo unahitaji kupoteza baadhi ya vitu. Hiki ndicho Magufuli alifanya. Aliamua kuminya baadhi ya vitu. Hili sio kwa nchi tu hata maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Naumia saana kuona wengi wanamuita Hayati Magufuli Dikteta , mwizi na hakufanya chochote. Niwaambie tu kuna siku mtamlilia.

Kwaherini nitarudi JF baada ya miaka miwili. 2023.

Mnadhani tutakuja kupata kiongozi mfuata demokrasia ya Ulaya, Atakayejenga miundombinu ya Ulaya na kutupa maisha ya Ulaya ndani ya miaka 5???

Kama kwenye akili zenu mnadhania hivi basi mtakufa bila kumpata....kwaherini.
Akhsante ,umenena vyema.
(Tutamkumbuka shujaa wa Afrika JPM.)
 
Back
Top Bottom