Nimegundua utajiri upo shambani

Nimegundua utajiri upo shambani

Hii risk inayoonekana kwenye kilimo ndio nzuri kwa maproffesionals na wataalam kutengeneza fedha.

..Go fight
 
Umechunguza ukajua hawa mama ntilie wanaingisza shingapi kibindoni?
Unajua faiada ya mchoma mahindi pale stend, chuoni au shuleni?
Umejiuliza wale wanaoza mandazi, keki, bagia, sambusa, chapatti n.k shuleni wanaingiza shingapi?
Mkuu fanya deep analysis ndipo uje utoe kauli hapa?
Watu tumejiridhisha ndio maana tunataka tujitoe kwenye utumwa wa ajira za kusubiri miaka na miaka.
Naamini hizi analysis umefanyia Dar kwa sana. Lakini Dar hakuna mashamba ndgu,😊😊
 
Naona kabisa Mtu atakavyoangukia pua kuhusu hilo, Kilimo kinachosha, kinazeesha, kinatia huzuni na simanzi sana pia kinaweza kukupa presha na mwisho wa siku utajikuta unaongea peke yako tu, na sababu za hayo yote ni Mkulima kutokuthaminiwa, kupangiwa bei, kupewa masharti namna ya kuuza mazao yake na kubwa zaidi kutokupata soko la uhakika, hapo bado hujasumbuliwa na hali ya hewa(mvua nyingi au kuwa na mvua kiduchu mpk mazao kama Mahindi kuzalia chini kama karanga)
 
Fanya kwanza utafiti vzr ujue na masoko ya mazao yako yalivyo maana kuna watu wengi humu wameshalalamika kupoteza pesa kwny shughuli za kilimo kwa kuingia kichwa kichwa
 
Halahala kilimo sio office kuingia uko mpaka uwe na miradi iliyosimama sasa kwa pesa umbazo ukizipoteza unalia sio za kuzi direct huko

NB:kilimo sio office ya uhakika.
Ngoja aende ataleta mrejesho!

Kilimo cha internet kitamu sana, anahisi fukara walioko shambani hawana mawazo haya!
 
Siwezi jilaumu kwanini nilisoma kwani elimu inafaida yake kubwa sana.
Baada ya kusoma sasaa nataka nitumie ujuzi wangu huu kujipatia kipato halali.
Nimeamua kwenda shamba kulima na kufuga ngombe na kuku.
Baadhi ya mazao ya shamba kama mahindi, mboga, maharagwe, matunda(Maembe, machungwa, matikiti, ndizi, nanasi n.k) nitauza mengine ntatumia mgahawani kwangu kuuza kama chakula (Nimegundua biashara ya chakula inalipa sana hasa ukiwa na wateja wa kuaminika kulingana na eneo ulilopo kama vyuoni, eneo lenye wapiti njia biashara nyingi).
-Mahindi ya kuchoma uanalipa.
-Chipsi zinalipa.
-Wali, ugali, vitafunwa vya hasubuhi kama mandazi na chapatti vinalipa.

Fiada za kuku na ngombe.
-Mimi nataka ngombe watatu au wane hawa wanatosha kunipa maziwa ya kutosha nikawa nauza mgahawani kama chai au maziwa mgando.
-Kuku kama 200 wanatosha kwaajili ya mayai tuu yakuuza.
-Mbalea itokayo kwa kuku na ngombe nitaitumia kupandia bustani za mboga na mazao mengine.


Faida za shamba
-Unakuwa huru! Hakuna wakukupelekesha wala kuwa kibaraka wa Fulani.
-Unaweza fanya kazi nyingi Zaidi hivyo kukuongezea kipatao chako kuliko kuajiriwa ambapo unapaswa uweo ofisini muda wote.
-Unakuwa na muda mwingi wa kufanya mambo yako kwa Amani.
-Hakuna makato yani pesa unayoipata ndio inayoingia mfukoni moja kwa moja.

Plan
-Kutafuta eneo lenye shughuli nyingi za watu hao watu ni mtaji wangu.
-Inategemea naweza nunua uwanja nijenge mgahawa au nikodishe mgahawa.
-Kujifunza kupika vyakula vitamu ili niteke soko plus chakula cha kutosha ili nipate raia wengi. Hii ni faida kisoko kwa sababu unapotoa huduma nzuri ndipo watu wanavutiwa kuja.
-Kodi ya mgahawa nitajipanga siku zote mwanzo ni mgumu.


NB: Bye bye kutembeza bahasha... naweza pata pesa nyingi namna hii Zaidi ya laki nane kwa mwezi hapo bado makato ya HESLB, sijui wapo huko mwishowe take home inakaribia kali tano kwa siku 30 hapo sijala, sijalipia kodi ya nyuba, usafiri, sijaumwa, sijanunua vocha, sijasaidia ndugu kwa laki 5 hapo ni kudanganyana.
Inapendeza kufikiri nje ya boki. Huku ndiko kujiajiri japo watu wengi hudharau sana wasomi sasa mimi nataka ni wa prove wrong.
Mawazo mazuri sana...
 
Utalima mwisho wa siku utakosa pa kuuzia mazao yako au utauza kwa hasara
 
Utalima mwisho wa siku utakosa pa kuuzia mazao yako au utauza kwa hasara

Kweli mwaya!
Awaulize walolima mbaazi kilichowakuta!
Sanasana Kwa baadhi ya mazao ataambiwa apeleke Kwenye stakabadhi ghalani ambapo bei utachoka mwenyewe na saingine kukopwa!
 
Lengo la kukueleza Haya ni kutaka uweze kuwa na ufahamu mapema (awareness is empowering)!
Ili utakapokutana na hizo changamoto ujue namna ya kuzikabili pasipo kukata tama!
Enterprenuers wengi ni risk takers Kwa hiyo wala usijali
Inawekana kutoka Kwa njia ya kilimo hapa nchini isipokuwa siyo rahisi lakini kutokuwa rahisi haina maana Kwamba haiwezikani la hasha inawezekana kabisa!
 
Kweli mwaya!
Awaulize walolima mbaazi kilichowakuta!
Sanasana Kwa baadhi ya mazao ataambiwa apeleke Kwenye stakabadhi ghalani ambapo bei utachoka mwenyewe na saingine kukopwa!
Nililima mbaazi mie nilivyokutana na bei ya Tshs 150 per kg. Nkaongoa miche yote nkaendelea na zao jingine
 
Unaanza kidogo kidogo mkuu vitu haviji kwa pupa hivyo kama unavyofikiri.kweli mkuu kwenye jambo lolote uvumilivu wa hali ya juuu unahusika sana
 
Naona kabisa Mtu atakavyoangukia pua kuhusu hilo, Kilimo kinachosha, kinazeesha, kinatia huzuni na simanzi sana pia kinaweza kukupa presha na mwisho wa siku utajikuta unaongea peke yako tu, na sababu za hayo yote ni Mkulima kutokuthaminiwa, kupangiwa bei, kupewa masharti namna ya kuuza mazao yake na kubwa zaidi kutokupata soko la uhakika, hapo bado hujasumbuliwa na hali ya hewa(mvua nyingi au kuwa na mvua kiduchu mpk mazao kama Mahindi kuzalia chini kama karanga)
Yote uliyoyasema hpo ni excuses ambazo kwa mtu ambaye ni enterpreneur minded anaweza kuzi overcome .....na ukishaingia kwenye kilimo inabidi ujiepushe sana na mazao ambayo serikali inayakontrol na hta ukilima lima kiasi either kwa matumizi yako binafsi au biashara kwa mlengo km mleta ambae atalima kwa ajili ya mgahawa wake....inshort nikuwa ukiwa uko strategically sio serikali wala mtu yoyote anaweza kuzuia wewe kufanikiwa
 
Nililima mbaazi mie nilivyokutana na bei ya Tshs 150 per kg. Nkaongoa miche yote nkaendelea na zao jingine

Aisee?!
Halafu waTZ wengi hawajui kula mbaazi sijui kwanini!
Mbaazi na jamii ya mikunde zinafaida nyingi kula kuliko nyama!
Yani Hivi msimu wa mbaazi mbichi unavyoishia nanunua kiloba kizima tunachambua nyumbani usiku na mchana kisha tunaweka Kwenye vikontena tunaweka Kwenye deep freezer tutakuwa tunatumia Kwa miezi hadi 3 !
Wenzetu wazungu ukiwaona wananunua nyama ni Kwaajili ya wageni maana wanajua wabongo tunapenda kula nyama!
Wao ukienda jikoni kwao utakuta vikopo vya maharagwe, kunde, choroko, mbaazi, njegere, njugu mawe n.k
Sana sana labda Kuku na Samaki!
 
Back
Top Bottom