Nimegundua utajiri upo shambani

Nimegundua utajiri upo shambani

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Siwezi jilaumu kwanini nilisoma kwani elimu inafaida yake kubwa sana.
Baada ya kusoma sasaa nataka nitumie ujuzi wangu huu kujipatia kipato halali.
Nimeamua kwenda shamba kulima na kufuga ngombe na kuku.
Baadhi ya mazao ya shamba kama mahindi, mboga, maharagwe, matunda(Maembe, machungwa, matikiti, ndizi, nanasi n.k) nitauza mengine ntatumia mgahawani kwangu kuuza kama chakula (Nimegundua biashara ya chakula inalipa sana hasa ukiwa na wateja wa kuaminika kulingana na eneo ulilopo kama vyuoni, eneo lenye wapiti njia biashara nyingi).
-Mahindi ya kuchoma uanalipa.
-Chipsi zinalipa.
-Wali, ugali, vitafunwa vya hasubuhi kama mandazi na chapatti vinalipa.

Fiada za kuku na ngombe.
-Mimi nataka ngombe watatu au wane hawa wanatosha kunipa maziwa ya kutosha nikawa nauza mgahawani kama chai au maziwa mgando.
-Kuku kama 200 wanatosha kwaajili ya mayai tuu yakuuza.
-Mbalea itokayo kwa kuku na ngombe nitaitumia kupandia bustani za mboga na mazao mengine.


Faida za shamba
-Unakuwa huru! Hakuna wakukupelekesha wala kuwa kibaraka wa Fulani.
-Unaweza fanya kazi nyingi Zaidi hivyo kukuongezea kipatao chako kuliko kuajiriwa ambapo unapaswa uweo ofisini muda wote.
-Unakuwa na muda mwingi wa kufanya mambo yako kwa Amani.
-Hakuna makato yani pesa unayoipata ndio inayoingia mfukoni moja kwa moja.

Plan
-Kutafuta eneo lenye shughuli nyingi za watu hao watu ni mtaji wangu.
-Inategemea naweza nunua uwanja nijenge mgahawa au nikodishe mgahawa.
-Kujifunza kupika vyakula vitamu ili niteke soko plus chakula cha kutosha ili nipate raia wengi. Hii ni faida kisoko kwa sababu unapotoa huduma nzuri ndipo watu wanavutiwa kuja.
-Kodi ya mgahawa nitajipanga siku zote mwanzo ni mgumu.


NB: Bye bye kutembeza bahasha... naweza pata pesa nyingi namna hii Zaidi ya laki nane kwa mwezi hapo bado makato ya HESLB, sijui wapo huko mwishowe take home inakaribia kali tano kwa siku 30 hapo sijala, sijalipia kodi ya nyuba, usafiri, sijaumwa, sijanunua vocha, sijasaidia ndugu kwa laki 5 hapo ni kudanganyana.
Inapendeza kufikiri nje ya boki. Huku ndiko kujiajiri japo watu wengi hudharau sana wasomi sasa mimi nataka ni wa prove wrong.
 
Kalime ndio utajua utajiri haupo shamani
Umechunguza ukajua hawa mama ntilie wanaingiza shingapi kibindoni?
Unajua faida ya mchoma mahindi pale stend, chuoni au shuleni?
Umejiuliza wale wanaoza mandazi, keki, bagia, sambusa, chapatti n.k shuleni wanaingiza shingapi?
Mkuu fanya deep analysis ndipo uje utoe kauli hapa?
Watu tumejiridhisha ndio maana tunataka tujitoe kwenye utumwa wa ajira za kusubiri miaka na miaka.
 
Umechunguza ukajiua hawa mama ntilie wanaingisza shingapi kibindoni?
Unajua faiada ya mchoma mahindi pale stend, chuoni au shuleni?
Umejiuliza wale wanaoza mandazi, keki, bagia, sambusa, chapatti n.k shuleni wanaingiza shingapi?
Mkuu fanya deep analysis ndipo uje utoe kauli hapa?
Watu tumejiridhisha ndio maana tunataka tujitoe kwenye utumwa wa ajira za kusubiri miaka na miaka.

Naunga mkonyo hoja
 
Halahala kilimo sio office kuingia uko mpaka uwe na miradi iliyosimama sasa kwa pesa umbazo ukizipoteza unalia sio za kuzi direct huko

NB:kilimo sio office ya uhakika.
 
Inahitajika kufanya tafiti ya kitaalamu ya kilimo husika, kama soil analysis etc..kufanya kilimo kitaalamu, elimu uliyosoma iwe msaada
Kabisa mkuu utafiti kwanza ndilo la muhimu then ndipo ulime bila kusahau utafiti wa soko na wateja.
 
Ni rahisi sana kinadharia! Ila kivitendo sina uhakika sana.
Vitu huanzia kichwani kama wazo ndipo implementation inaanza.
Kwanza kabla sijaanza rasi kilimo, ufugani na biashara ya chakula napaswa kutafiti eneo lenye udongo mzuri na maji liwe supportive kwa kilimo na mifugo pili napaswa nitafiti soko kwa maana ya eneo wateja.
Huo ni mwanzo tuu
 
Utajiri upo popote ni masuala ya ubunifu tu juhudi na bahati pia.
Ndio maana wapo waliotajirikia kwenye kilimo na ufugaji na wapo pia waliofilisikia huko huko.
Wapo matajiri ambao hawajawah kulima na wapo masikini ambao wanalima na ambao hawajaw kulima.
 
Halahala kilimo sio office kuingia uko mpaka uwe na miradi iliyosimama sasa kwa pesa umbazo ukizipoteza unalia sio za kuzi direct huko

NB:kilimo sio office ya uhakika.
Tuchulie wewe umezaliwa kijijini wazee wako wana mashamba ya kutosha je huwei fanya kitu?
Hata yule ambae hana kitu hawezi jipanga azama shamba baada ya kufanya research za kutosha?
Tatizo lenu nyinyi watu huwaga mnaenda kama kuku tuu pasipokujali hasara, faida na possible outcomes kwa ujumla.
Siku hizi ili tufanye jambo ni lazima tujue na yatakayotokea hatufanyi kazi kwa kubahatisha!!111 huu ni ulimwengu mwingine babu pengine elimu yako itakusaidia kuwa tofauti na wengine wanaotegemea bahati nasibu shambani.
 
Ukiwa sehemu ambayo ipo well watered, kilimo ni dili lakini sehemu kubwa ya nchi mifumo ya maji ni shida.
Ni mikoa gani inayoongoza kwa kuzalisha maindi tz?
Tuanze hapo.
 
Back
Top Bottom