Siwezi jilaumu kwanini nilisoma kwani elimu inafaida yake kubwa sana.
Baada ya kusoma sasaa nataka nitumie ujuzi wangu huu kujipatia kipato halali.
Nimeamua kwenda shamba kulima na kufuga ngombe na kuku.
Baadhi ya mazao ya shamba kama mahindi, mboga, maharagwe, matunda(Maembe, machungwa, matikiti, ndizi, nanasi n.k) nitauza mengine ntatumia mgahawani kwangu kuuza kama chakula (Nimegundua biashara ya chakula inalipa sana hasa ukiwa na wateja wa kuaminika kulingana na eneo ulilopo kama vyuoni, eneo lenye wapiti njia biashara nyingi).
-Mahindi ya kuchoma uanalipa.
-Chipsi zinalipa.
-Wali, ugali, vitafunwa vya hasubuhi kama mandazi na chapatti vinalipa.
Fiada za kuku na ngombe.
-Mimi nataka ngombe watatu au wane hawa wanatosha kunipa maziwa ya kutosha nikawa nauza mgahawani kama chai au maziwa mgando.
-Kuku kama 200 wanatosha kwaajili ya mayai tuu yakuuza.
-Mbalea itokayo kwa kuku na ngombe nitaitumia kupandia bustani za mboga na mazao mengine.
Faida za shamba
-Unakuwa huru! Hakuna wakukupelekesha wala kuwa kibaraka wa Fulani.
-Unaweza fanya kazi nyingi Zaidi hivyo kukuongezea kipatao chako kuliko kuajiriwa ambapo unapaswa uweo ofisini muda wote.
-Unakuwa na muda mwingi wa kufanya mambo yako kwa Amani.
-Hakuna makato yani pesa unayoipata ndio inayoingia mfukoni moja kwa moja.
Plan
-Kutafuta eneo lenye shughuli nyingi za watu hao watu ni mtaji wangu.
-Inategemea naweza nunua uwanja nijenge mgahawa au nikodishe mgahawa.
-Kujifunza kupika vyakula vitamu ili niteke soko plus chakula cha kutosha ili nipate raia wengi. Hii ni faida kisoko kwa sababu unapotoa huduma nzuri ndipo watu wanavutiwa kuja.
-Kodi ya mgahawa nitajipanga siku zote mwanzo ni mgumu.
NB: Bye bye kutembeza bahasha... naweza pata pesa nyingi namna hii Zaidi ya laki nane kwa mwezi hapo bado makato ya HESLB, sijui wapo huko mwishowe take home inakaribia kali tano kwa siku 30 hapo sijala, sijalipia kodi ya nyuba, usafiri, sijaumwa, sijanunua vocha, sijasaidia ndugu kwa laki 5 hapo ni kudanganyana.
Inapendeza kufikiri nje ya boki. Huku ndiko kujiajiri japo watu wengi hudharau sana wasomi sasa mimi nataka ni wa prove wrong.