Nimegundua simu yangu ni feki. Daaaah!

Hulda-Tamarri

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
1,196
1,292
Kwanza kabisa nimshukuru member anayeitwa Chief-Mkwawa pamoja na wadau wote wa technolojia waliochangia kwenye ile thread inayohusu kujihadhari na simu za mitandao ya kikorea, China na marekani....asanteni kwa kunifumbua macho!

Nilinunua Samsung s8 active ikawa haiperforme vizuri, inaganda tu apps zinastopp mara kwa mara. Nikaamua kugoogle ili nijue tatizo na suluhisho lake ndio nikaiona hiyo thread nikasoma vizuri nikafuata maelezo hatimae nikagundua simu yangu ni feki hata imei number haiendani na muundo wa simu daaaaah sijui naifanyaje maana kahela kangu kananiuma mweeeeeh!! Nikifikiria kuwa TCRA wanazifungia ndo nachoka kabisaaaa! Alafu simu yenyewe niliinunua kwenye mnada.......hivi naweza kuirudisha kwa hao jamaa kweli?

Nimecheck kwa ile namba ya TCRA pamoja na Imei info naletewa NONY 312 wakati simu ni S8 active khaaaaa!! Internal memory inasoma 128 GB alafu nikatumia 3Gb tu simu imejaaa hahahaaa wacha tu nijicheke maana sijui hata naifanyaje!!!

1. Je, inaweza kufanyiwa ujanja wowote nikaendelea kuitumia kama kawaida bila matatizo yeyote na TCRA wasiizime?
2. Any other option? Maoni yenu wadau maana nishachanganyikiwa naogopa hata kumuuzia mtu asije akagundua akanishitaki bure!

N.B tusiozijua simu vizuri nashauri turudi tu kwenye tecno. Tecno hata mikoani wana matawi yao ila hizi simu zingine brand kubwa kubwa ni maumivu tu hata ukienda dukani changa la macho ni la kufikia!
 
Nenda polisi tu mkuu uone watakusaidia nini..
Wakishindwa tafuta jeshi lako uende kulipiza kisasi.. njoo PM kama unataka kunikodi niwe mercenary lakini gharama za kunitoa Tarime nilipo ni juu yako
 
Kwanza kabisa nimshukuru member anayeitwa Chief-Mkwawa pamoja na wadau wote wa technolojia waliochangia kwenye ile thread inayohusu simu feki za mitandao ya kikorea, China na marekani....asanteni kwa kunifumbua macho!

Nilinunua Samsung s8 active ikawa haiperforme vizuri, inaganda tu apps zinastopp mara kwa mara. Nikaamua kugoogle ili nijue tatizo na suluhisho lake ndio nikaiona hiyo thread nikasoma vizuri nikafuata maelezo hatimae nikagundua simu yangu ni feki hata imei number haiendani na muundo wa simu daaaaah sijui naifanyaje maana kahela kangu kananiuma mweeeeeh!! Nikifikiria kuwa TCRA wanazifungia ndo nachoka kabisaaaa! Alafu simu yenyewe niliinunua kwenye mnada.......hivi naweza kuirudisha kwa hao jamaa kweli? Maana wao ni madalali japo nina risiti

Nimecheck kwa ile namba ya TCRA pamoja na Imei info naletewa NONY 312 wakati simu ni S8 active khaaaaa!! Internal memory inasoma 128 GB alafu nikatumia 3Gb tu simu imejaaa hahahaaa wacha tu nijicheke maana sijui hata naifanyaje!!!

1. Je, inaweza kufanyiwa ujanja wowote nikaendelea kuitumia kama kawaida bila matatizo yeyote na TCRA wasiizime?
2. Nina risiti ya brokers, Je naweza kuwarudishia simu wakaipokea wakakubali kunirudishia hela yangu?
3. Any other option? Maoni yenu wadau maana nishachanganyikiwa naogopa hata kumuuzia mtu asije akagundua akanishitaki bure!

N.B tusiozijua simu vizuri nashauri turudi tu kwenye tecno. Tecno hata mikoani wana matawi yao ila hizi simu zingine brand kubwa kubwa ni maumivu tu hata ukienda dukani changa la macho ni la kufikia!
kama risiti unayo nenda mahali uliponunua uwaelezee tatz lako
wakileta fyoko fyoko
nenda zako Tcra au polisi kawashitaki kwa kuleta bidhaa fake coz n moja ya kuhujumu...
uzuri wake unayo risiti
 
Uliinunua shingapi???tatizo ndio linaanzia hapo.
kama risiti unayo nenda mahali uliponunua uwaelezee tatz lako
wakileta fyoko fyoko
nenda zako Tcra au polisi kawashitaki kwa kuleta bidhaa fake coz n moja ya kuhujumu...
uzuri wake unayo risiti

Tatizo niliinunua kwenye mnada 180k, mtu alifilisiwa duka. Hao madalali wanaweza kushitakiwa kweli? Hofu yangu ndo hiyo, ingekuwa dukani ningeshairudisha tangu asubuhi
 
Nenda polisi tu mkuu uone watakusaidia nini..
Wakishindwa tafuta jeshi lako uende kulipiza kisasi.. njoo PM kama unataka kunikodi niwe mercenary lakini gharama za kunitoa Tarime nilipo ni juu yako

Kinachonikatisha tamaa ni vile simu niliinunua kwenye mnada. Je, madalali wanashitakiwa? Sheria inasemaje! 180k ni bei ndogo kwa simu za Samsung ila kwa hali ya sasa ya uchimu kuipoteza hiyo ni maumivu makali aiseee!
 
sasa S8 ukachukua kwa 180k
seriously ulidhani ni Og????
hapo kama huna shida sanaaa
ipige chini achana nayo tafut nyingine

Mazingira ya uuzwaji ndio yalonifanya nikanunua.
Alafu kama kitu hukijui mkuu sio rahisi kugundua, sijawahi kutumia Samsung pia ndio maana nikaliwa kiboya aiseee hahaaa nacheka kama mazuri ila karoho kananiuma! Hapo kwa hiyo 180k ningejipatia ka tecno pop 1 masikini ya Mungu nikasukumia maisha.
 
Kinachonikatisha tamaa ni vile simu niliinunua kwenye mnada. Je, madalali wanashitakiwa? Sheria inasemaje! 180k ni bei ndogo kwa simu za Samsung ila kwa hali ya sasa ya uchimu kuipoteza hiyo ni maumivu makali aiseee!
Duh kama ulichukua kwa 180k itumie kama calculator tu maana bei ya s8 ni kuanzia laki nane kwenda juu..

Sasa kama ulichukua kwa 180k its obvious kuwa simu ilikua ni fake.. kwahio wewe komaa tu au utafute msukuma umuuzie uondokane na mzigo huo..

Polisi hawatakusaidia kitu chochote hata wakikusaidia gharama zitazidi 180k
 
Hii ndo inaitwa kupatwa kwa Samsung!!
Hapa nilipo naomba mluga luga ajisogeze nimchomekee! Au niende kwa mafundi nikaiuze angalau nipate kifuta jasho
 
Mazingira ya uuzwaji ndio yalonifanya nikanunua.
Alafu kama kitu hukijui mkuu sio rahisi kugundua, sijawahi kutumia Samsung pia ndio maana nikaliwa kiboya aiseee hahaaa nacheka kama mazuri ila karoho kananiuma! Hapo kwa hiyo 180k ningejipatia ka tecno pop 1 masikini ya Mungu nikasukumia maisha.
unaonesha wewe ni Ke
kama.ni Ke siyo kosa lako lakini kama Ni Me basi daaah
Muhimu achana nayo mbambikizie MTU hata kwa 100K upunguze machungu
 
Back
Top Bottom